Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,634
- 697,845
Mwaka 1896 Kampuni ya kikoloni ya serikali ya ujerumani ya Germany East Africa Plantation (Deutsche-Ostafrikanische Plantagenge Schellshaft) walianzisha shamba la majaribio ya kilimo cha kahawa kwenye eneo ambalo kwa sasa linajulikana kwa jina la Irente.
Mashamba mengine ambayo yalianzishwa kipindi hicho ni Gare, Maweni, Sakharani na Mazumbai. Kusudi lilikuwa ni kufanya jaribio la zao hili lakini kutokana na ukosefu wa rotuba ya udongo zao la kahawa lilitelekezwa mwaka 1914.
Baada ya Ujerumani kupoteza koloni lake kwa Mwingereza mwaka 1918 shamba hili lilimikiwa na raia kutoka Ugiriki, Bwana W.J Tamé. Na baada ya uhuru wa Tanganyika mwaka 1961 shamba hili liliuzwa kwa Kanisa la Kilutheri Tanzania (Tanzania Lutheran Church).
Inasemekana neno Irente Farm lilitokana na kirai (phrase) "I rented a Farm" na hivyo jina Irente likatokana na jina "I rented". Kutokana na mazungumzo ya lugha ya kingereza wakati huo baadhi ya Waswahili walibadilisha "I rented" kuwa ‘Irente’.
Jr