Hakuna atakayepona kama vita itatokea pale Ghuba ya Uajemi. Nadhani unasahau kwamba suala siyo kutunza mafuta miezi mitatu, suala ni kwamba makampuni yanayoongoza kuuza mafuta ndiyo yaleyale The Six Sisters kama The Royal Dutch Shell, British Petroleum, Exon Mobil, Chevron na Total n.k
Pipa la mafuta likipanda hadi kufika dola 100 hadi 150 unadhani soko la hisa litakuwa salama ?? Suala jingine ni kwamba siasa za ufalme wa Saudi Arabia ni kama lose canon kama wakiingia kwenye vita na Iran wakati ndani ya nchi yao kuna mtafaturuku basi huenda huu ndiyo utakuwa mwanzo wa anguko lao ambao unaeweza kupelekea hata machafuko ya kisiasa.
Suali jingine: Kama Saudi Arabia na UAE wamewashindwa waasi wa kihouthi kule Yemen pamoja na silaha zote zile, unadhani watawaweza wairani kweli ???
Kabla ya kuporomoka kwa bei ya mafuta yalikuwa yamefika $120 per barrel if not $125.
Unajua sababu ni nani? US kuamua ku encourage shale drilling ndani kwao na kupunguza import reliance.
US pekee waliweza kufanya kuwe na oversupply ya mafuta yakashuka mpaka $20 dollars per barrel.
Waarabu walijaribu kushusha bei wakitegemea shale drilling watawashinda kwenye cost of production kwa kufurisha soko kwa mafuta wakashindwa uwezi shindana na marekani akiamua kwenye maswala ya uchumi.
Tatu siasa za mafuta zimebadilika sana since Yom Kippur war, Israel tu pekee alikuwa keshafika mpaka Cairo atoe uongozi wote wa Middle East kilichowaokoa waarabu ni S.A kukata mafuta kwa West na madhara yalikuwa makubwa, kiasi kwamba US wakawasii waache kwanza kibano, since then somo lao West walilipata hapo ndio chanzo cha kuanzisha IEA.
Hiyo 3 months reserves usidhani imewekwa kwa bahati mbaya lengo lake ni kujipa muda ikiwa wakipambana tena na waarabu au ikitokea conflict kwenye hiyo region wawe na mafuta ya kutosha kuweza kubadili logistics na sera nyingine ilikuwa kutafuta vyanzo nje ya hizo nchi ambavyo kwa sasa ni vingi.
Watumiaji wa mafuta yanayopita hapo Strait of Hormuz ni Asia kwa asilimia kubwa sio West, yes mafuta yatapanda lakini sio kuwa na madhara makubwa kwao na watu makini kwa sasa wanajipanga kwa logistic kwa hiki kinachoendelea.
Na mwisho seven sisters wa 1930’s sio wa leo, duniani sasa hivi largest oil companies ni host nations corporates like Aramco, China Oil, Petrobas etc.
Bado kuna madhara lakini west washajua namna ya ku minimise risks zao likitokea lakutokea hiyo region, it is not ideal kuivamia Iran. Lakini ukishaleta ubabe kwa hawa watu aminitishi na ukawapa sababu expect hell to follow.