Irani yakamata Meli ya mafuta ya UK

Irani yakamata Meli ya mafuta ya UK

Mkuu ni vema kusoma nyakati na huo mgogoro wa mashariki ya kati kwa undani,USA akimgusa tu irani jua ndio vita ya 3 ya dunia hiyo na USA atakuwa sio superpower tena wa dunia,najua historia unaijua vizuri maana urusi yupo venezuela china ndio huyo wana mgogoro wa kibiashara anasubiri mu take advantage.
Man to man USA ana uwezo mkubwa tena sana wakumpiga irani,tatizo ni kwamba akiamua kumpiga nae ndio unaweza kuwa mwisho wake.
Kinachomlinda Iran mkuu ni sehemu nchi ilipo ni of very strategic importance katika bidhaa muhimu duniani. Na anaweza leta disruption kubwa through proxy war.

Tusuburi how events will unfold with this saga maana tunachojadili ni mitazamo tu, majibu tutayapata with time.
 
Hakuna sehemu nimesema Iran is an Arab state.

Hakuna sehemu nimesema UK ataenda pekee, zaidi ya kutoa mfano Falkland alipotumia ubabe usikii dunia ikizungumza uonevu wakati ni tukio recent, tofauti na US ilipovamia Vietnam peke yake mpaka leo dunia inatafsiri uonevu.

Ni hivi maswala ya kuzitwanga hizi nchi zilizokuwa nje ya West zinahitaji support ya jumuiya ya kamataifa be it that equates to western support.

Na US ajashindwa militarily kumtwanga Iran kama umefuatilia bali kutoa justification ya kuivamia Iran; hii ni nchi ambayo ukiivamia kama unaelewa maswala ya energy security kuna madhara makubwa sana ya kuichumi kuivamia inabidi upate support kubwa sana, hapo ndipo walipokwama.
Inamaana kwa tafsiri rahisi nikwamba USA hamuwez iran basi ama ?!

Maana bila support tena

Kwan yy c super power mzee ama kashakua super poda ?!
 
Inamaana kwa tafsiri rahisi nikwamba USA hamuwez iran basi ama ?!

Maana bila support tena

Kwan yy c super power mzee ama kashakua super poda ?!
Support aina maana ya military, bali go ahead blessings pia.
 
Muingereza ni sungura mjanja anajua kujipanga kutokana na nafasi yake, anaelewa nguvu zake kama world super power zilipotea kwa sasa yeye kajikita kwenye influence na allies but Britian is not militarly slouch by any means.

Europe nor UK hakuna mwenye appetite ya kuivamia Iran; kosa la Iran ni kuwatishia nyau waingereza sasa kama unawajua tabia zao wanapotishiwa throughout history they won’t take that kindly.

Mgogoro wa Scotland hizo ni siasa zingine, so is the BREXIT na hiyo backstop conundrum ambazo story zake nindefu.

Lakini hawa wanatabia moja wanapolumbana wao kwa wao akitokea adui wa nje wanapose wanamalizana na huyo alien kwa pamoja halafu wanarudi tena kuendelea na migogoro yao.
Wametishiwa nyau na nani mkuu wkata wameteka meli ya wa2 na yao imetekwa mpaka ss moja moja no any respond nakuhakikishia Britain hawana lakusema asee unawatetea 2 kashindwa Us whos GB
 
Complicated kidogo yes Iran aitakiwi kufuata ata Grace1 si meli ya Iran bali ni ya Panama wote hao sanctions za EU aziwahusu.

Kesi yao ni kwamba hiyo meli ilikuwa inapita ndani ya mipaka ya EU kwa nia ya kupeleka mafuta nchi ambayo ina sanctions za EU kwa hiyo wanauhalali wa kuizuia.

Ukitaka kujua ukoloni umeisha au la ngoja kwanza Iran akatae kuitoa hiyo meli kwa njia za diplomasia halafu uone watavyomfanya.
Aitakiwi = Haitakiwi
Aziwahusu = Haziwahusu
 
That was deemed agressive behaviour ni US ndio aliefuta nuclear deal na ni US ndio alikuwa anailazimisha Iran kuongea nao kwa ubabe hakuna mtu ata support hiyo vita.

This is a separate incident ni Iran ndio imeichokoza na kuitunisha misuli UK.

Swala la Grace1 pamoja na kwamba UK wamekamata ndani ya himaya za EU lakini bado kuna legal wrangles za definitions za EU Regulation 36/2012 kama ni sahihi kwa tukio lenyewe ndio maana jumuiya ipo kimya pamoja na kwamba mahakama ya Gibraltor imeidhinisha meli imekamtwa kwa kuvunja masharti ya EU sanctions.

Sasa kukamata meli zao ni dharau kubwa kutoka Iran kama ni message basi UK unitishi and trust they won’t like that hawa ni watu wanapambana na mighty Russia kwa madai ya kwamba wame commit acts of crime nchini kwao na kupata support ya EU kutoa sanctions tena mtu mwenyewe alieuwawa ni raia wa Russia wala sio wao; sasa tena ukamate resources zilizokuwa chini ya bendera yao si muda EU utasikia inatoa support kwa UK.

Tusibishane sana Iran keshaambiwa aachie hiyo meli kwa amani or else.
Haya 2kubaliane hapa ina maana kama haja achia wataka nambia iran atapigwa
 
Complicated kidogo yes Iran aitakiwi kufuata ata Grace1 si meli ya Iran bali ni ya Panama wote hao sanctions za EU aziwahusu.

Kesi yao ni kwamba hiyo meli ilikuwa inapita ndani ya mipaka ya EU kwa nia ya kupeleka mafuta nchi ambayo ina sanctions za EU kwa hiyo wanauhalali wa kuizuia.

Ukitaka kujua ukoloni umeisha au la ngoja kwanza Iran akatae kuitoa hiyo meli kwa njia za diplomasia halafu uone watavyomfanya.
Hawana lakumfanyaaaa
 
Kabla ya kuporomoka kwa bei ya mafuta yalikuwa yamefika $120 per barrel if not $125.

Unajua sababu ni nani? US kuamua ku encourage shale drilling ndani kwao na kupunguza import reliance.

US pekee waliweza kufanya kuwe na oversupply ya mafuta yakashuka mpaka $20 dollars per barrel.

Waarabu walijaribu kushusha bei wakitegemea shale drilling watawashinda kwenye cost of production kwa kufurisha soko kwa mafuta wakashindwa uwezi shindana na marekani akiamua kwenye maswala ya uchumi.

Tatu siasa za mafuta zimebadilika sana since Yom Kippur war, Israel tu pekee alikuwa keshafika mpaka Cairo atoe uongozi wote wa Middle East kilichowaokoa waarabu ni S.A kukata mafuta kwa West na madhara yalikuwa makubwa, kiasi kwamba US wakawasii waache kwanza kibano, since then somo lao West walilipata hapo ndio chanzo cha kuanzisha IEA.

Hiyo 3 months reserves usidhani imewekwa kwa bahati mbaya lengo lake ni kujipa muda ikiwa wakipambana tena na waarabu au ikitokea conflict kwenye hiyo region wawe na mafuta ya kutosha kuweza kubadili logistics na sera nyingine ilikuwa kutafuta vyanzo nje ya hizo nchi ambavyo kwa sasa ni vingi.

Watumiaji wa mafuta yanayopita hapo Strait of Hormuz ni Asia kwa asilimia kubwa sio West, yes mafuta yatapanda lakini sio kuwa na madhara makubwa kwao na watu makini kwa sasa wanajipanga kwa logistic kwa hiki kinachoendelea.

Na mwisho seven sisters wa 1930’s sio wa leo, duniani sasa hivi largest oil companies ni host nations corporates like Aramco, China Oil, Petrobas etc.

Bado kuna madhara lakini west washajua namna ya ku minimise risks zao likitokea lakutokea hiyo region, it is not ideal kuivamia Iran. Lakini ukishaleta ubabe kwa hawa watu aminitishi na ukawapa sababu expect hell to follow.

Bwana Kilatha nakupa hongera kwa kujenga hoja nzuri na iliyotulia. Lakini bado nachelea kusema kwamba hoja yako haina usahihi sana hivyo tusipoiangalia kwa makini inaweza kupoteza mwelekeo mzima wa huu mjadala wetu:

Mosi, umetoa takwimu kwamba mafuta kabla ya The Shale Revolution yalikuwa ni dola $120-125 kwa pipa, mimi nakanusha maana katika takwimu za miaka kumi hakuna sehemu mafuta yaliwahi kufika bei hiyo. Bei za juu kabisa za mafuta katika kipindi cha nyuma ni hizi hapa. Mwaka 2008 pipa moja lilifika dola 145, mwaka 2011 pipa moja lilifika dola 133, mwaka 2013 pipa moja lilifika dola 118. Katika hili naomba tuweke kumbukumbu sawa kabisa.

Pili, OPEC huwa hawaamui kujipandishia tu bei za mafuta kama wewe unavyosema hapa, huwa kuna sababu ambazo zinahalalisha upandishwaji wa bei za mafuta. Mara nyingi sababu kubwa huwa ni hali ya kisiasa ya eneo au majanga mbalimbali. Hebu tuangalie sasa kwanini bei za mafuta zilikuwa juu sana kabla ya The Shale Revolution ya mwaka 2014.

Mwaka 2008 mafuta yalipanda hadi kufika dola 143 kwa pipa kwasababu ya mtikisiko wa kiuchumi: Mwaka 2011 mafuta yalipanda hadi kufika dola 113 kwa pipa kwasababu ya machafuko yaliyoikuta nchi ya Libya: Mwaka 2013 January mafuta yalipanda bei sana hadi kufika dola 119 kwa pipa kwasababu jeshi la Iran lilikuwa linafanya mazoezi kwenye mfereji wa Hormuz: Mwaka 2013 July mafuta yakapanda tena bei na kufika dola 109 kwa pipa kwasababu ya machafuko ya Misri ya kumtoa Raisi Morsi ambayo yalileta hofu ya kufungwa kwa mfereji wa Hormuz.

Kiufupi kile kilichoitwa The Arab Spring and The Rise of ISIS kilipelekea mlipuko wa bei za mafuta kwa kiwango cha juu sana kwasababu gharama za uzalishaji zinakuwa juu na nchi wazalishaji hujikuta kwenye machafuko. OPEC huwa hawamki tu na kuamua kupandisha bei ya mafuta, japo upandishaji mara nyingine upandishaji wao huibua maswali.

Sasa hivi umejiuliza, siku Iran, Saudi Arabia, UAE na Marekani wanaingia vitani yale mapipa milioni 17 yanayopiya Hormuz kwa siku nani atayafidia ???

Tatu, umeongelea nchi za Magharibi kuwa na sera ya kutunza mafuta kwa miezi mitatu, mimi nasema vyema kabisa lakini nadhani hujalitazama hili jambo katika ukubwa wake. Mafuta kazi yake siyo kuendesha mitambo tu, Asilimia 13% ya mafuta huenda kwenye Petrochemicals ambazo hutumika kuzalisha mbolea, madawa ya binadamu na plastiki. Ndiyo maana mafuta ya kutoka Ghuba ya Uajemi yanaenda kwa wingi barani Asia.

Gharama za uzalishaji wa mafuta zikiwa juu na za shida inamaana gharama za usafirishaji lazima zitakuwa juu tu, hivyo mbolea na vyakula lazima vitapanda bei, hapo bado hujagusa sekta ya afya. Unadhani hayo mafuta ya miezi mitatu yatasaidia ??? Sidhani hata kidogo.......

Nne, hoja yako ya kusema kwamba makampuni ya Magharibi hayana nguvu tena na kwamba makampuni ya nyumbani kama Saudi Aramco ndiyo habari mpya, nadhani haijafanyiwa uchunguzi wa kina. Saudi Aramco ni kampuni kubwa sana duniani lakini kitu ambacho hukijui ni kwamba lipo kwenye ubia mkubwa na haya makampuni ambayo wewe umesema biashara yake iliisha mwaka 1930's, hebu tuangalia kwa undani kidogo:

SAMREF ndiyo kinu kikubwa cha mafuta kule mashariki ya kati ambacho ni sehemu ya Saudi Aramco, lakini ambacho wengi hamjui ni kwamba ni uwekezaji wa pamoja baina ya Saudi Aramco na Exon Mobil ya Marekani.

SATORP nayo ni mkono wa kampuni la Saudi Aramco lakini ni uwekezaji wa pamoja baina ya Saudi Aramco na Total ambalo linamilikiwa na Serikali ya Ufaransa.

SASREF nao ni mkono mwingine wa kampuni la Saudi Aramco lakini ni uwekezaji wa pamoja baina ya Saudi Aramco na The Royal Dutch Shell la Uholanzi.

YASREF nao ni mkono mwingone wa kampuni la Saudi Aramco lakini ni uwekezaji wa pamoja baina ya Saudi Aramco na Sinopec la Uchina.

Hapa utaniambiaje kwamba makampuni ya Magharibi habari yake iliisha miaka ya 1930's ??? Hebu naomba tulijadili hili vizuri.

NB: Kuna kitu kwenye sheria kinaitwa Anti-Trust Law au The Law of Competition, ambapo makampuni makubwa kama Saudi Aramco huwa hayaruhusiwi kutawala biashara ya mafuta peke yao kwasababu ya kuogopa kutengeneza Monopoly ambayo ni hatari kwa afya ya biashara za kimataifa. Refer case ya Standard Oil mwaka 1911...

Makampuni ya Magharibi bado yako kule Mashariki ya kati yakishirikiana na makampuni ya wazawa, katika kuchimba mafuta. Hili linamaanisha yakitokea machafuko pale basi lazima na yenyewe yatatetereka sana.

Mwisho kabisa, kwa siku mapipa milioni tano yanapita mfereji wa Hormuz kuelekea barani Ulaya pekee, utasemaje mtumiaji wa ule mfereji ni Asia peke yake ??? Hebu nieleweshe....
 
NB: Kuna kitu kwenye sheria kinaitwa Anti-Trust Law au The Law of Competition, ambapo makampuni makubwa kama Saudi Aramco huwa hayaruhusiwi kutawala biashara ya mafuta kwasababu ya kuogopa kutengeneza Monopoly ambayo ni hatari kwa afya ya biashara za kimataifa.

Makampuni ya Magharibi bado yako kule Mashariki ya kati yakishirikiana na makampuni ya wazawa, katika kuchimba mafuta. Hili linamaanisha yakitokea machafuko pale basi lazima na yenyewe yatatetereka sana.

Mwisho kabisa, kwa siku mapipa milioni tano yanapita mfereji wa Hormuz kuelekea barani Ulaya pekee, utasemaje mtumiaji wa ule mfereji ni Asia peke yake ??? Hebu nieleweshe....
Basically mafuta yanapanda na kushuka all the time why the historical data za 2013/14 matters so much and the shale revolution kwa sababu mafuta kama bidhaa yoyote yanasukumwa na demand and supply foremost, then the other economic variables. Lakini tangia yashuke kuanzia 2014 ayajarudi kwenye bei hiyo mpaka sasa.

Ni kwa namna gani OPEC inaweza influence prices za mafuta, as a monopoly together they own almost 80% of the global oil. Na wanapangiana kila mtu azalishe kiasi gani in normal circustances ili kuwe na stable supply as well as prices based on demand. Wakitaka kushusha bei wanaongeza supply na wakitaka yapande bei wanapunguza supply; that’s how they control prices.

Ndio maana unaona S.A amesema Iran akifungiwa kuuza kabisa wao wata stabilize supply kwa kuongeza output.

Of course yanapokuja maswala ya production kwenye uchumi kuna other variables ambazo zinaweza affect supply, demand and price kwa upande wa mafuta ni kasi ya ukuaji wa uchumi wa dunia, natural disaster, weather etc kama ulizozitaja; lakini main issues ni supply and demand ambazo OPEC ina control pretty much.

Sasa how did shale revolution impact price, chimbuko lake lilisasabisha uwingi wa mafuta na oversupply ambayo OPEC awawezi ku control, kumbuka wao wanaweza influence nchi zilizo wanachama tu wazalishe vipi kumanage supply at reasonable prices.

Kwa sababu shale in cost kubwa kuzalisha per barrel compared to drilling, na kila bidhaa ina break even point. OPEC kupambana na shale impact wakaamua kuongeza uzalishaji kwa lengo la kwamba mafuta yashuke bei mpaka shale asiwe na faida ya break even kutokana na bei ndogo ya sokoni.

Kilichotokea makampuni ya shale nayo yalivumilia hasara mpaka mapato ya nchi za OPEC kuanza kuathirika kutokana bei ndogo ya mafuta waarabu wenyewe wakakubali yaishe kwa kuamua kupunguza production hili walau bei ziongezeke.

Katika huo mpito na waopia wamejifunza umuhimu wa ku diversify uchumi wao, usitegemee mapato ya mafuta (that is another topic).

Hao Seven Sister’s, Importance ya mafuta kwenye uchumi, ukubwa wa host nations company nitaendelea.... alamsiki kwa sasa kichwa hoi nibaki msomaji wa majungu ya jukwa la siasa nicheke na vijembe vya kule kabla sijazima.
 
Mkuu ni vema kusoma nyakati na huo mgogoro wa mashariki ya kati kwa undani,USA akimgusa tu irani jua ndio vita ya 3 ya dunia hiyo na USA atakuwa sio superpower tena wa dunia,najua historia unaijua vizuri maana urusi yupo venezuela china ndio huyo wana mgogoro wa kibiashara anasubiri mu take advantage.
Man to man USA ana uwezo mkubwa tena sana wakumpiga irani,tatizo ni kwamba akiamua kumpiga nae ndio unaweza kuwa mwisho wake.
Haitakuwa vita vya dunia Iran hana support ya Mrusi na certainly USA akiamua kumtandika Iran, itakuwa mwisho wa utawala huu wa Iran. History ni kama neno lenyewe, history.
 
Back
Top Bottom