Kimbunga
Platinum Member
- Oct 4, 2007
- 14,952
- 10,037
Alishagombea na kupata uongozi wa ccm vijana,lakini tukiwa kwenye maandalizi ya party ya kumpongeza tuliyoiandaa pale leaders club ambayo ilikua aje kuwa mgeni rasmi,yeye alipitia pahala kwenye shughuli za kichama asubuhi ya siku ile,sasa akarejea nyumbani akabadili magwanda yao yale ya ccm ndio aje kwenye party akiwa "ameoga",akiongozana na msafara wake yeye pamoja an katibu wake ccm vijana,walipita nyumbani kwake,akawaacha wengine chini akapanda juu kwenda kubadili nguo...hakushuka tena mpaka leo...kufuatia tukio lile kuna watu walitajwa tajwa kuhusika na kifo chake akiwemo Londa,meya wa zamani wa kinondoni na watu wengine waliosemekana kukerwa na ippy kupata nafasi hiyo huku akiwaacha watu waliokimbiza sana mwenge..na waliosotea chama kitambo
Mkuu ahsante sana kwa ufahamisho huu. Nilikuwa na kumbukumbu tu kwamba alikuwa na mchakato kumbe ulikuwa umesha na ameshinda. Mkuu enzi hizo nilikuwa busy kwenye vyama vyetu hivi vipya kwa hiyo mambo ya CCM nilikuwa nayasikia kwa mbali mbali ndio maana kumbukumbu zangu zikawa mbali kidogo!!!
Kwa hiyo huenda kulikuwa na kamchezo kachafu? Najua mzee pia alisononeka sana manake jamaa alikuwa Jembe lake!