Duh!
Ipy daima tutakukumbuka yaani nakumbuka tulionana muda mfupi kabla ya mauti kukufika, nakumbuka ulitokea kwenye mkutano uliokuchagua kuwa Mwenyekiti wa UVCCM siku ya jumamosi ukaja Mgulani JKT hall kwenye harusi ya rafiki yetu sote tukakushangilia na ukahaidi kuwafuata maharusi hotelini asubui ukawape supu kwani ulitaka kuchinja mbuzi asubui yake ilikuwa mida ya saa 6:30 usiku sitokaa ni sahau asubui yake tukapigiwa simu kuwa umetutoka, wengi wetu kwenye ile group yetu hatukuaamini tulidhani ni uongo lakini tulipofika upanga tukakuta ni kweli umetangulia mbele ya haki, ni vigumu sana kuamini kuwa ulitutoka ingawa yalisemwa mengi sana juu ya kifo cha Ipy ila Mwenyezi Mungu pekee ndie ajuae.
:rip: Ipy.... RIP Brother daima tunakukumbuka miaka 10 imepita ila ni kama juzi umetutoka,
Mwenyezi Mungu ailaze roho yako mahala pepma peponi Amen.