mfalmeselemani
Member
- Sep 30, 2014
- 95
- 47
Hao IPTL wezi tu Kafulila yupo sahihi kama sio wezi kwanini wahisani wamekataa kutoa pesa mpaka uchunguzi wa jambo hili ukamilike
Mataifa wahisani wamechelewesha msaada wa kuipiga jeki bajeti ya Tanzania hadi pale uchunguzi kuhusu madai ya ufisadi katika sekta ya nishati utakapotolewa na hatua muafaka kuchukuliwa. Kundi la wahisani hao linalojumuisha Finland, Ujerumani, Uingereza, Norway, Sweden, Denmark, Kamisheni ya Umoja wa Ulaya, Ireland, Canada, Japan, Benki ya Dunia na Benki ya Maendeleo ya Afrika, hadi sasa wametoa kiasi cha dola milioni 69 kama sehemu ya ahadi ya msaada wa dola milioni 558 kukidhi mahitaji katika bajeti ya Tanzania. Je, unaunga mkono hatua hiyo ya wahisani?
Chanzo:DW (Kiswahili) ya tarehe 13 Octoba
Mjinga pekee ndo ataumia kusikia Wahisani wamekataa kutoa pesa,..Ndo mana maisha yetu tumeaachia wahisani hakuna kutukuza juhudi za ndani kuliendeleza Taifa kwa nguvu zetu wenyewe.Hao wamekataa kwa kuwa hawajajua kinachoendelea,hawajajua uhalisia upo vp kwenye hilo sakata,ndo mana wamepisha uchunguzi sio kwamba wamekatisha hiyo misaada mnayoitegemea..Ukweli unabakia pale pale,hakuna pesa ya umma inayowekwa kwenye ESCROW account, hizo ni pesa za malipo ya chochote inayohifadhiwa kupisha mgogoro unaoendelea,wala sio mali ya serikali..