''Tunapenda kuwasisitizia watanzania waendelee kumpuuza mtu huyu kwani kwa sasa amevurugwa ndio maana anahamishahamisha mijadala na kiasi cha kumhusisha Waziri Mkuu, Baraza la Mawaziri huku akijua ESCROW ni jambo la kisheria na si la kisiasa na yalikuwa malipo halali kwa IPTL/PAP na huo ndio ukweli na utaendelea kuwa hivyo, na ningemshauri Kafulila ajifunze nini maana ya ESCROW hata kwa njia ya mtandao
ili siku nyingine asiendelee kulishwa ujinga wa namna hii bila kujua ukweli wa ndani kufanya hivyo ni kufedhehesha watanzania kwamba wanawachagua wabunge wenye uelewa mdogo kama Kafulila''. ilisema taarifa hiyo.
Ilisema uelewa finyu huu wa Kafulila unamsababisha ashindwe kutofautisha kati ya mali ya umma na mali binafsi, fedha za umma zilizopo BoT na uwakala wa ESCROW wa BoT, kazi za serikali na kazi za mbunge kazi za IPTL/PAP na kazi za TANESCO tunasisitiza IPTL/PAP sio shirika la Umma wala mali ya serikali,
Kafulila na wenzake waelekeze nguvu katika mashirika ya umma yanayofilisika kila kukicha huku na yeye akiwa sehemu ya ufilisi huo, Watanzania tuwapuuze wabunge vibiriti fitini kama Kafulila na wenzake waliokubali kuweka pembeni uelewa wao na kutumika na makampuni shindani dhidi yetu pamoja Standard Chartered, vinginevyo ajiseme hadharani yeye ni mbia wa Standard Chartered.
Hivyo, tunawahakikishia watanzania tutaendelea kuzalisha na kuwauzia umeme wa uhakika na kwa bei nafuu na mchakato wetu wa kushusha bei ya umeme kutoka 450 ya sasa kwa uniti mpaka sh. 80 uko mbioni kukamilika ili watanzania wafurahie huduma ya umeme na wachagize maendeleo yao japo kina Kafulila na wapinzani wetu wa kibiashara hawapendi watanzania wafaidi matunda yao