IPTL/PAP wamvaa David Kafulila

IPTL/PAP wamvaa David Kafulila

Watanzania ni waajabu sana wanamtetea mwizi aliyewaibia bilioni 200 kisa kapewa laki au 10. Tena ukute mtu mwenyewe ni graduate dah. Mnatutukanisha sana. Najua CAG atachepusha ripoti kama alivyofanya TAKUKURU enzi za epa na Richmond lakini mwisho wa siku itajulikana tu. Ona hata wafadhili wameona uvundo huo eti Mtanzania baba zima lililoanzia wizi pale TRA linashupaa na kuwalipa vidampa kuja kutetea na kubariki wizi!!! only in Tanzania.
 
Wakati mkijadiri escrow na IPTL kumbukeni yafuatayo;
(i) Kampuni ya IPTL ilitokana na ubia wa kampuni mbili Mechamar 70% ya hisa zote na VIPEM 30% ya hisa.
(ii) Mitambo ya ufuaji umeme ilianza kujengwa mwaka 1997 mpaka 1998.
(iii) Uzalishaji wa umeme ulianza rasmi mwaka 2002.
(iv) kuchelewa kwa uzalishaji wa umeme kulitokana na mgogoro wa IPTL na TANESCO uliotokana TANESCO kupinga gharama CAPACITY CHARGE.Mwaka 2001 mgogoro huo ulipatiwa ufumbuzi kwenye mahakama ya ICSID kwa IPTL kuamuliwa kushusha gharama za capacity charge kutoka $ 4.2 milioni mpaka $ 2.6 milioni.
(v) Siku chache baada kuanza uzalishaji Mgogoro mwingine ulizuka kati ya wabia wa IPTL ambao ni MECHMAR na VIPEM baada ya madai kuwa mmiliki mkubwa wa IPTL ambae ni MECHMAR anamdharau mwekezaji wa kizalendo VIPEM na kutumia nafasi yake vibaya kwa kufuja fedha ya kampuni na kukopa kwenye mabenki na kuto mshirikisha VIPEM ipasavyo kwenye uendeshaji wa kampuni. Kikubwa kilikuwa mgogoro wa kimaslahi.
(vi) VIPEM mwaka huohuo 2002 ilifungua kesi ya kutaka kampuni ya IPTL ifirisiwe kila mtu achuke chake.
(vii) Wakati kesi kati ya wabia hao wa IPTL ikiwa inaendelea mahakamani kampuni ya IPTL iliendelea kuzalisha umeme kama kawaida na haikuwahi kuacha kuzalisha umeme.
(viii) Kutokana ya kuwa na kesi ambayo chanzo chake ni mgogoro wa kimaslahi, VIPEM ikaomba malipo yote ya IPTL yasiendelee kutolewa kwa utaratibu uliokuwa ukitumika sababu tiyari alikuwa na mashaka na mwekezaji mkubwa ndani ya IPTL ambae ni MECHMAR.
(ix) mwaka 2006 ndio ukatoka uamuzi kuwa basi fedha hizo ambazo zilikuwa zilipwe kwa IPTL basi zitengenezewe akaunti maalum kutokana na wabia wenyewe tiyari walikuwa na mgogoro wa kimaslahi.
(x) Akaunti hiyo maalum iliitwa ESCROW akaunti na kwenye PPA inamention kipengere hiki cha kuundwa kwa akaunti maalum ya ESCROW tofauti tu ni kuwa this time mgogoro ni wa wabia wenyewe.
(xi) Mkataba wa ESCROW agreement ulifungwa rasmi july 2006 ukihusisha pande tatu ambazo ni; IPTL kama kampuni ambayo ndio ilistahili malipo hayo ambayo yanatunzwa kwenye escrow akaunti, serikali na TANESCO.

Tuendelee kujadiri sasa....
 
Tuendelee kujadiri sasa....

Sawa kabisa, tujadiLI,

Ebu na wewe jibu haya maswali saba kutoka Tanzania Daima


Maswali saba kwa Waziri Muhongo kuhusu ufisadi IPTL
04/06/2014 | Na Martin Malera | Makala | maoni 0 | wasomaji 5

IFAHAMIKE kwamba ufisadi katika Akaunti ya Baraza la Usuluhishi la Migogoro ya Kibiashara (Escrow) ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), msingi wake ni mkataba wa kifisadi wa IPTL uliosainiwa mwaka 1995 kutokana na tatizo la umeme mwaka 1994 ambapo taifa lilihitaji umeme wa dharura.

Ndipo IPTL ikasaini mkataba wa miaka 20 (1995-2015) na wamiliki wa kampuni hiyo ya IPTL walikuwa Mechmar ya Malaysia mwenye asilimia 70 na VIP ya Tanzania yenye asilimia 30.

Kwa mujibu wa mkataba wa Tanesco na IPTL, walikubaliana kuwa muamuzi wa mwisho kuhusu mgogoro baina yao ni Baraza la Usuluhishi la Migogoro ya Kiuwekezaji (International Centre for Settlement of Investment Disputes – ICSID).

Kosa la kwanza IPTL haikuweza kukamilisha mradi wake 1995 kwenye kipindi cha dharura na badala yake ikakamilisha mwaka 1998.

Baada ya kumaliza mwaka 1998 IPTL ililalamikiwa na Tanesco huko ICSID kwamba imekuza gharama za uwekezaji na hivyo kukuza gharama za umeme, mwaka 2001 uamuzi wa ICSID ukatoka ikabainika ni kweli IPTL ilikuza gharama kwa kiasi cha dola milioni 41.7. Hili ni kosa kubwa.

Mwaka 2002, IPTL ikaanza kuiuzia umeme Tanesco lakini mwaka 2004 Tanesco ikabaini kuwa IPTL ilidanganya kuhusu mtaji.

IPTL ilisema asilimia 30 ya mtaji ilikuwanao kama equity sawa na dola milioni 36 na kwamba asilimia 70 ilikopa. Lakini baada ya ukaguzi ikabainika kuwa IPTL haikuweka dola milioni 36 kama equity bali dola 50 ambapo kwa exchange rate ya wakati huo ya 1:1000, dola 50 ilikuwa sawa na sh elfu 50 ambazo hata fundi baiskeli angeweza kuwekeza.

Kutokana na kasoro hiyo, Tanesco ikataka gharama ya umeme (tarrif) ishuke kwa sababu bei ilizingatia equity ya dola milioni 36 kumbe ni sh 50,000. Mabishano yakaendelea hadi 2006.

Mwaka 2006, serikali na Tanesco ikashinikiza ifunguliwe akaunti maalumu (Escrow) ili malipo yawekwe huko hadi mgogoro utakapokwisha kuhusu bei sahihi ndipo pesa hiyo igawanywe kwa kuzingatia bei sahihi baina ya pande mbili, ndiyo maana ilikuwa kosa kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kusema pesa yote ya Escrow eti ni ya IPTL kabla ya uamuzi kuhusu bei haujafikiwa.

Mwaka 2008 IPTL iliposhindwa kujiendesha ikawekwa chini ya receivership chini ya RITA ambayo ikawa inasimamia gharama za uendeshaji.

Septemba mwaka 2013, ikatoka hukumu ya Mahakama Kuu chini ya Jaji Utamwa iliyojichanganya baada ya VIP mwenye asilimia 30 kushitaki na kutaka IPTL iondolewe chini ya receivership na mali zake zote ipewe kampuni ya PAP ya Harbinder Singh Sethi.

Hukumu hiyo ikaenda mbali na kusema Sethi mwenye rekodi mbaya ya ufisadi tangu nchini Kenya anakotuhumiwa kushiriki ufisadi mkubwa mwaka 2002 wa Goldenberg – kashfa iliyokiangusha chama cha KANU chini ya Daniel arap Moi na asiye na rekodi yoyote ya uwekezaji katika umeme, ikasema atazalisha 500MW na kwamba ataiuzia umeme Tanesco kwa bei nafuu ya dola senti 6 hadi 8 kwa unit.

Hukumu hiyo inaamua hivyo wakati ikijua kuwa mmiliki wa asilimia 70 ya IPTL yuko chini ya liquidation Malaysia na zaidi ICSID kuna kesi inayohusu mgogoro wa IPTL na serikali uliofunguliwa na Standard Chartered Bank ambayo ilinunua deni la IPTL mwaka 2005 na ikaruhusiwa kuishitaki Serikali ya Tanzania kwenye baraza hilo lenye mamlaka ya mwisho.

Hukumu ya Jaji Utamwa haikujua kuwa hoja ya biashara kwa maana ya bei na kiasi cha umeme ambao Tanesco itanunua kwa IPTL sio kazi ya mahakama bali ni makubaliano ya Tanesco kwa kutegemea mahitaji na zaidi mwanahisa mkubwa alikuwa ‘under liquidation Malaysia' na kulikuwa na kesi ICSID.

Pamoja na Jaji Utamwa kudai mali zote za IPTL ipewe kampuni ya PAP, bado ieleweke kuwa pesa za Escrow hazikuwa mali ya IPTL kwa kuwa uamuzi kuhusu mgogoro wa bei haukuwa umefanywa kokote na zaidi ulikuwa unasubiria hukumu ya ICSID.

Februari mwaka 2014, ICSID ilifanya uamuzi wa awali kwamba ni kweli IPTL ina overcharge Tanesco na kuelekeza pande mbili zikafanye hesabu upya ndani ya siku 90 zilizoisha Mei 2014.

Msingi wa hukumu ile ungesaidia kujua ni kwa kiasi gani IPTL imeiibia Tanesco tangu 2002 hadi 2013 katika bei kwa kuzidisha bei ya kununua unit ya umeme (overcharge).

Tanesco na serikali hawakutoa ushirikiano ndani ya siku 90 kutekeleza uamuzi huo ambao una faida kwa nchi kwa sababu tayari tangu Septemba 2013, fedha ya Escrow imeshaliwa. Huu ndio uzalendo?

Maswali saba ambayo Prof. Muhongo anatakiwa kujibu.

Mosi, kwanini serikali ilikimbilia kufanya malipo hayo kwa haraka?; Kuna taarifa kwamba kipindi malipo haya yanasukumwa kwa nguvu BoT itoe, aliyekuwa Waziri wa Fedha, William Mgimwa alikataa na akaanza kuumwa na wakati malipo yanafanyika Novemba 2013, tayari alikuwa amekata kauli hospitalini Afrika Kusini.

Pili, kampuni ya PAP ilikomba fedha hiyo wakati mmiliki halali ni IPTL ndio maana hadi sasa hakutoa share certificate ya yeye kuuziwa asilimia 70 za IPTL ambazo ziko chini ya Mechmar.

Kwanini serikali kwa muda mfupi imemuamini huyo Sethi bila ya kufanya utafiti wa kujiridhisha? Kama kweli alinunua asilimia 70 ya hisa za Mechmar zilizo IPTL, basi angelipa capital gain tax, lakini hakuna ushahidi huo kama alivyo na ushahidi wa kununua hisa 30 za VIP.

Ushahidi mwingine uliopo ni kwamba wakati PAP inasema iliinunua IPTL tangu 2010 ukweli ni kwamba tangu 2008 hadi 2013 IPTL ilikuwa under receivership chini ya RITA, na hivyo isingewezekana kisheria hisa zake ziuzwe. Maelezo kwa hili yanahitajika.

Ushahidi mwingine kampuni yenyewe ya Mechmar imeliandikia barua gazeti la Citizen na kwa wakili wake Tanzania Asyla Attorney kupinga kuwa haijauza hisa zake za IPTL kwa kuwa ilikuwa under liquidation na ikielekeza kuwa huyo PAP anayedai kuwa alinunua hisa hizo awaonyeshe share certificate. Maelezo ya kina yanahitajika.

Hakuna ushahidi wa malipo ambayo PAP ameonyesha alifanya kununua share za VIP kabla ya kupata pesa za Escrow.

Kwa sababu hiyo ndiyo maana mmiliki wa VIP aliandika barua BoT kulalamika kuwa Kampuni ya PAP ni ya kitapeli isilipwe kwa kuwa ilikuwa haijamlipa, wakati huo ilikuwa mwanzoni Novemba 2013, kabla pesa haijatoka Escrow.

Hii maana yake PAP alilipa VIP baada ya kuchota pesa za Escrow. Kwamba alinunua hisa baada ya kupata fedha za Escrow. Hii haikubaliki kisheria, Mwanasheria Mkuu (AG) atueleze nini kilitokea.

Kwa ujumla suala hili ni aibu nyingine kwa taifa ambalo Tanesco inadaiwa zaidi ya sh bilioni 400, leo inatapanya bilioni 200 kizembe namna hii.

Lakini zaidi liquidator wa Mechmar ataidai serikali na kulipwa, Standard Chartered ambaye alikuwa anaidai serikali na kesi haijafika mwisho naye tutamlipa.

Huyu Sethi atabaki na mitambo ya IPTL na ametudhulumu hizo bilioni 200 za Escrow pamoja na gharama ambazo IPTL ilikuwa ina overcharge ambazo zilipaswa turejeshewe zaidi ya dola milioni 150 za tangu 2002 hadi 2013. Hapa maelezo ya kina yanahitajika.

Tanzania Daima – Maswali saba kwa Waziri Muhongo kuhusu ufisadi IPTL
 
IPTL hawana kesi na TANESCO kama wanasiasa wetu uchwara wanavyodai!

Mwaka 2006 serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia Wizara ya Nishati na Madini, shirika la IPTL na Benki Kuu ya Tanzania (wakala) kutokana na Mkataba wa kuzalisha na kuuza umeme kutoka IPTL kwenda TANESCO kulianzishwa akaunti ya ESCROW.
MAtakwa ya makubaliano ya kuanzishwa na kutekelezwa kwa mradi wa kujenga, kuendesha na kuzalisha umeme wa kuuza kati ya kampuni binafsi ya IPTL na TANESCO ni kwa serikali kufungua letters of credit au kufungua akaunti ya ESCROW.

Akaunti hiyo siyo fedha za serikali bali ni fedha ambazo ziliwekwa kutokana na matakwa ya mkataba wa kuuza umeme kwa TANESCO kutoka kampuni binafsi. Katika mkataba wa kufungua akaunti ya ESCROW kuna kifungu kinasomeka, "required amount means the amount in Tshs. That the government of Tanzania shall deposit from time to time in the ESCROW account which equals not less than two months estimated tariff payments under the PPA, provided that such amount shall be adjusted annually by IPTL and TANESCO pursuant in the PPA in the article 11 hereof, and government of Tanzania will be entitled will be entitled to review independently, the calculation of the required amount pursuant to this agreement".
Tafsiri yake kwa Kiswahili ni kwamba "kiasi kinachopaswa kuingizwa na serikali katika akaunti ya ESCROW ni kile ambacho kinalingana na madai ya malipo sawa na miezi miwili ya gharama ya kuuza umeme ambazo IPTL inadai TANESCO, IPTL na TANESCO watafanya marejeo kuhusiana na kiasi cha gharama za umeme kila mwaka. Hayo ni kwa mujibu wa makubaliano ya kuuza na kununua umeme kwa mujibu wa makubaliano ya mkataba wa mauzo ya umeme (Power Purchasing Agreement) au kwa kifupi PPA na kama ilivyobainishwa kwenye kifungu cha 11. Serikali itakuwa huru kufanya tathmimini yake kuhusu gharama halisi za uzalishaji na uuzaji wa umeme kwa mujibu wa mkataba wa PPA.
Wakati akaunti ya ESCROW inafunguliwa serikali na IPTL walikuwa katika mahakama ya usuluhishi ya ICSD ambapo suala la gharama za capacity charge lilikuwa linagombewa. Hivyo serikali ya Tanzania ilikataa madai ya kulipa dola za kimarekani milioni 3.6 kwa ajili ya capacity charge.
Katika Mahakama ya Usuluhishi fedha ambazo zilikubaliwa ni dola za Kimarekani millioni 120 na hivyo gharama za capacity charge kuteremshwa kufikia dola za Kimarekani milioni 2.6. Hivyo mgogoro kati ya serikali na IPTL ukawa umekwisha.
Kumalizika kwa mgogoro huo kunamaliza utata wote wa serikali kuwa na madai katika akaunti ya ESCROW, isipokuwa yale yanayohusu kodi ambazo TRA itakuwa inadai wakati akaunti ya ESCROW itakuwa imefunguliwa kwa wahusika kwa makubaliano ya kutoa fedha au pale fedha kutoka akaunti ya ESCROW zitakuwa zimetolewa na kuwekezwa katika vitega uchumi kama inavyoelezwa katika kifungu cha 3 kinachohusu uwekezaji wa fedha katika akaunti ya ESCROW.
Inaelezwa kwamba shria za Tanzania ndiyo zitatumika katika uthibiti wa fedha za akaunti ya ESCROW. Mtazamo huu wa sheria unazingatia matakwa ya usuluhishi ya Mahakama ya kimataifa ya usuluhishi ICSID ambayo inatamka wazi kwamba wahusika wanakubali kwamba IPTL inathibitiwa na Nationals na hivyo itachukuliwa kuwa shirika la Tanzania kwa madhumuni na matakwa ya makubaliano ya mkataba wa kimataifa. Na wakala wa akaunti ya ESCROW anathibitiwa na serikali ya Tanzania na hivyo anatambuliwa kama taasisi ya kitanzania kwa madhumuni ya mkataba wa ICSID.
Hivyo alipopatikana mnunuzi PAP ambaye alikubaliana kununua hisa za VIP Engineering and Marketing shirika hilo ambalo linamiliki aslimia 30% ya hisa zote, ilikuwa sahihi aondoe kesi ya kutaka IPTL ifunge hughuli zake na wabia wagawane mali. Mahakama Kuu haikukosea kukubaliana na VIP Engineering and Marketing kuondoa kesi na hivyo kufungua milango kwa mmiliki wa hisa zote 100% kuchukua fedha zilizokuwa Benki Kuu kwenye akaunti ya ESCROW.​
 
Kafulila atakoma kuingilia mambo ya kampuni binafsi, hivi kwani hawezi kupigania viwanda vya mawese vinavyoendela kufilisika kila siku huko kigoma badala ya kuingilia kampuni ambayo iko pale kisheria
kweli we we kwikwi yan MTU anatetea maslai ya inch we we unasema anaingilia mambo ya watu binafsi
Kweli nimeamini inchi imeuzwaa hii
 
Fedha ya Tegeta Escrow account ni stahiki halali ya IPTL ya Tegeta Salasala hakuna kitakachobadirisha hili siyo ripoti, siyo Zitto, siyo kafulila.
 
Back
Top Bottom