Ipo siku Ustaadhi Ilunga atasababisha damu imwagike nchini!

Ipo siku Ustaadhi Ilunga atasababisha damu imwagike nchini!

Status
Not open for further replies.
Akiuwawa shehe kamata Askofu, Kardinal Padri na Walei uwa; unaweza uwa kwa kificho au hadharani;

Waislamu wanalia na Kanisa linalia;

Mkiuwa kama wanne hivi watakuwa wanaheshima;

Akiuwawa Muislam msichome matairi wala kuharibu maduka mtakuwa mnakosea uhai wenu ni kulipa kisasi kwa kukumata askofu au padri na kumuua;

Ushauri kwa vyombo vya usalama


1. Police inatakiwa kuanza uchunguzi wake kwa kumkamata aliyetoa kauli hii na kuipandikiza kwa Waislam wakati inachunguza na kufatilia wauwaji wa Father Mushi huko Zanzibar
 
uislamu umeletwa na waarabu hapa africa na ukiristo umeletwa na wamisionari wakitokea ulaya,sisi africa hatuna dini yetu au zetu?nani atanijibu hili swali?
 
hivi ile inteligensia ni kwa ajili ya kuzuia mikutano ya chadema tu au ?
maana hapa haionekani kufanya kazi kama ilivyoada yake ni kwa nini haya mambo yanatokea kwenye kipindi cha Rais huyu na si
kipindi kingine chochote lazima tujiulize haya maswali?Je alipouwawa barlow kule mwanza ilichukua muda gani kuwabaini wale waliohusika na alipotekwa Ulimboka na kuwataja mahasimu wake wamechukuliwa atua gani je ni kwa nn gazeti la mwanahalisi lifungiwe kwa kutoa habari inayoweza kutumika kuisaidia polisi kuhusu Dr.Ulimboka ?


My take :hapa kama kila mtu asipokua makini nafikiri maisha si salama tena kwani hao walio na jukumu hilo wenyewe hawajiwezi angalia Barlow
 
Ilunga sawa na akina Ponda na Uamsho wanatapatapa kutaka kumuingiza kila mtu kwenye mtego wao. Hata hivyo hawatafanikiwa kutokana na kuwa vipofu wa uhalisia wa maisha ya maeneo husika.

Watu wana shida na kuondoa umaskini siyo kutafuta utakatifu wala kuishi kwenye pepo za kufikirika wakati hapa duniani wanaishi kwenye jehanamu. Nadhani matatizo ya watu maskini hayachagui dini. Hivyo ni suala la muda tu hili wimbi la mawazo ya kigaidi na mgando litapita. Naona Kenya wanajitahidi kuwaondolea mbali wachochezi kama hawa.

Nadhani huyu mchochezi ana muda mfupi tu kufanya huo uchochezi wake. Kenya wanafanya vitu vyao kimya kimya tofauti na Tz ambapo viongozi wetu hawana msimamo wala ajenda kwa taifa zaidi kuchumia tumbo.

Huyu Ilunga anashughulika naa nn hasa?hayo anayoyafanya anatumia njia gan? redio,gazeti,video au tv?
 
duh god bless tanzania,,rais tuliyenaye ni zuzu hana maamuzi,,na anawatumia waumini wa dini yake kuvuruga amani ya nchi, kwa taarifa tu kama huyu padre angekuwa ni ni sheikh mpaka sasa tungeshuhudia mauaji ya kutisha ya wakristo
 
Asante mkuu kwa kuliona hilo,lakini nikuulize swali hili,unadhani serikali yako yenye dhamana kulinda amani ya nchi na raia wote inaliona hilo? Ponda amekuwa akihamasisha uvunjifu wa amani ,hakukamatwa mpaka walipoharibu makanisa mbagala,ILUNGA anayetoa DVD hizi pamoja na redio imani bado wanadunda mpaka tumefika hapa ambapo watu wameanza kuchinjana.Je serikali ipo au ndo maana halisi ya serikali DHAIFU?

udhaifu udhaifu wa kikwete ndio chanzo cha yote haya
 
Huyu Ustaadh Ilunga ni mtu hatari kwa utaifa wetu.

Haiingii akilini mtu mwenye hekima zinazotarajiwa kuwepo kwa kiongozi wa dini kuwa na maoni potofu kiasi hiki.
Kiongozi wa dini anatakiwa awe na hekima na busara sana.

Huu uchochezi hauna na usipewe nafasi kwa Tanzania.
 
haongei pumba yule sheikh anazo facts za kutosha mbona wale waliosema nchi haitotawalika wameachwa wanakata mitaa. Naisihi gvt yetu hii ya JMT iwe makini kutatua tatizo hili sisi tupo kama observer tunasubiri kabla ya kuchukua hatua
 
Sasa serikali ya huyu muheshimiwa DHAIFU inataka kuunda tume ya wataalamu walibobea kutafuta wahusika wa hili sakata la padre wakati mambo yote yako hadharani namna hii???
 
Katika uchaguzi wa 2010---vyama vyote (CCM, Chadema, na CUF) vilitumia udini kwenye kampeni zake. Huo ndio ukweli.

Na bado.

Ushauri kwa Chadema. Politically huwezi kumsimamisha Padre wa zamani wa kikatoliki kugombea uraisi kwenye nchi Kama Tanzania. He will never be elected. Or he will never get Muslim support. Ndio ukweli halisi.
 
Watanzania mjilaumu wenyewe kwa matukio mabaya yanayoendelea nchini kwa sasa!! Serikali ya ccm haikuingia mstuni na kutwaa madaraka bali mliipa kura kwa ushabiki wenu wenyewe!!! Hiyo ndiyo kasi mpya... na ndiyo madhara ya kupiga kura kama vipofu!!
 
Utamfanya nini? wakati anatoa maneno hayo akiwa anajua anaulinzi kamili hawezi kuguswa na mtu, dola yote iko mkononi mwake, tangu ikulu -usalama wa Taifa-jeshi la polisi-majeshi yote-wakuu wa wilaya na mikoa - makamndawa polisi mikoa na wilay wote wanamhakikishia ulinzi kwa nini asitoe maneno hayo? lakini iko siku watakubali tu, uvumilivu ukikoma.
 
Ili amani ya kweli nchi hii ipatikane kusiwe na watu wanaojiona wao wana haki zaidi ya wengine,viongozi wao wa dini waheshimike kuliko viongozi wa dini nyingine.Mfano kauli ya kadinali pengo ina nguvu na umuhimu kwa viongozi wa serikali ya nchi hii kuliko kauli ya raisi wa nchi.shame on the goverment

tatizo si jirani,mheshimu mkuu wa kaya yako kabla ya jirani.Nani atasema hapo ulipo akasikilizwa mana anapingwa ndani kwa ndani.
 
Wanasaikolojia wanasema kuwa "Mtu akisema kuwa atafanya jambo fulani, basi iko siku atalitenda"

Huyu mtu anaeitwa Hassan Ilunga wa Mwanza ni mtu muhimu sana katika upelelezi wa mauaji Padre Mushi, yeye ndiye aliehutubia waislam na kusambaza DVD kuwa waislam waue Mapadre, Maaskofu na Wachungaji iwe hadharani au kwa kujificha.

Kwa sababu yeye ndiye alitoa maagizo, kuna uwezekano wauaji walimpa taarifa kuhusu mipango ya uuaji. Kuna uwezekano Ilunga anafahamu mtandao wa kimafya, kuna taarifa kuwa kuna watu walipelekwa SOMALIA kwa ajili ya mafunzo ya uuaji (ushetani) Serikali ikimkamata huyu jamaa atasema mtandao huo.
 
..kwanza Ustadh ILUNGA KAPUNGU anafanya makosa sana kujaribu kutuhusisha wa-Tanzania na matatizo yanayotokea Kenya, particularly Mombasa.

..huko ni kujaribu kuzua tatizo hata mahali ambapo hakuna tatizo.

..halafu anakwenda mbali na kutoa kauli kwamba "akiuawa Shekhe basi tafuta Askofu umuue"!! Is he out of his mind?!!

..hebu tembeleeni link ya video niliyoweka hapo chini. unaweza kuanzia dakika ya 13. kinachosikitisha video nzima imekaa kimachafuko-chafuko tu. haya ni mambo mabaya sana kuwaaminisha wa-Tanzania.




Kwa wanaotumia simu, tembelea Ustadh Ilunga Hassan - Mauaji ya shahid Aboud Rogo na Unafiki katika sensa Part 1 - YouTube


Hawa ni al shabab, it is clear now...Al shabaab Live in Tz
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom