Ipi ni tofauti ya mwili, nafsi na roho?

Mkuu ikikuoendeza sana naomba tufundishe mambo ya Astra projection,na pia hii mada ingia ndani sana ili wengine tufunguliwe macho.
 
Roho na nafsi ni viungo na dhana za kufikirika tu.

Havipo.
Wewe ni kichaa ...nafsi ni ufahamu wa kujitambua....roho ni spirit ndiyo energy kisayansi na mwili ni matter ambayo nayo ni energy tu hivyo Energy (roho) ni kila kitu mwili pia ni energy na nafsi ni energy pia hata mungu ni energy pasipo energy hakuna mungu wala chochote.
 
MWANZO 2:7

"BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa kiumbe chenye nafsi hai"

Mkuu, kupitia nukuu iliyopo hapo juu kutoka katika maandiko utaona kuwa, mwili wa binadamu ni umbile la nje la viungo vyake vinavyooneka katika ulimwengu wa nje. Bali roho ni umbile la ndani la viungo vyake katika ulimwengu wa roho usioweza kuonekana kwa macho ya kimwili. Muunganiko wa maumbile ya nje na ndani ndiyo hukifanya kiiumbe kuonekana kuwa chenye nafsi hai katika sura ya dunia. Uwepo wa hitilafu kubwa katika mwili wa binadamu ama kiumbe chochote, na kutenganishwa na roho yake, basi nafsi yake uhesabika kuwa imekufa.

Tunaweza kupata picha nzuri kupitia kifaa chochote kile cha umeme. Kifaa hicho honekana hakifanyi kazi yake pasipo kuunganishwa katika umeme ambayo ni nishati hai. Muunganiko wa kifaa husika na umeme unaotiririka katika "components" zake za ndani ndipo kinapoonekana kuweza kufanya kazi yake iliyokusudiwa.

Muundaji wa kifaa amekipa mwili wake wa nje unao onekana, lakini pia kuna uhitaji wa mtiririko wa nishati ya umeme ndani yake ambao hauonekani kwa macho ya kibinadamu, ili kifaa cha umeme kifanye kazi zake sawasawa. Uwepo wa hitilafu kubwa katika kifaa ama pasipo kuunganishwa katika umeme, kifaa uhesabika ni kibovu, au kimekufa.
Mwili na nafsi vyote ni roho tumieni akili neno roho ni spirit ndiyo energy kisayansi....kwenye biblia mungu ana bainisha ukuu wa neno roho kwa kusema hata yeye ni roho na ufalme wake wote ni ufalme wa roho(energy) hivyo mwili na nafsi vyote ni roho
 
Mwili ni jumba
Roho ni nishati
Nafsi ni muunganiko wa mwili na roho
Utendaji Kazi
Mwili ni kibebeo cha roho.. Roho sio yabisi hivyo inahitaji jumba/kituo.. Tokeo la roho ndani ya mwili huzaa utambulisho huo utambulisho ndio nafsi

Sent using Jamii Forums mobile app
Mnachanganya mambo mwili na nafsi vyote ni roho (spirit) yaani energy.......Energy ndiyo mother nature ya vitu vyote hakuna kitu chochote kisicho energy
 
Chief Unauzungumziaje huu watu wanaita Ulimwengu wa Roho? Seems huko ndo kuna kila kitu.
Utasikia ukienda kwa watumishi Nabii au hata hawa waganga wanajua kila kitu kitu katika maisha yako na hata kukutabiria na ikawa kweli au kujua mtu ayawazayo
Naitaji somo hapo.
Hapo sasa ndiyo mkubaliane na mimi .....neno roho ni kiswahili kwa kingereza ni spirit na kisayansi ni Energy....hivyo ulimwengu wa roho ni kusema ULIMWENGU WA ENERGY ni sahihi kabisa maana ndiyo ilivyo
 
Wewe ni kichaa ..
Fala wewe.
As.nafsi ni ufahamu wa kujitambua....roho ni spirit ndiyo energy kisayansi na mwili ni matter ambayo nayo ni energy tu hivyo Energy (roho) ni kila kitu mwili pia ni energy na nafsi ni energy pia hata mungu ni energy pasipo energy hakuna mungu wala chochote.
Mwili upo una onekana.

Thibitisha una Roho acha Definition uchwara uchwara.
 
Naomba kujua utofauti na uhusiano wa Mwili, Nafsi na Roho.

Vipo wapi na vinatendaje kazi katika mwili wa mwanadamu.

Nawasilisha.
Mwili container/ kibebeo cha roho na nafsi. Roho ni uhai, ni kile kinachofanya mwili uwe hai kwa kusukuma damu ambayo ndiyo inapeleka chakula,maji na hewa sehemu zote za mwili. Nafsi inahusika zaidi na cognitive domain yaani mambo ya fahamu na maamuzi ambayo mtu anafikiria na kutenda, yaani hisia ya kiakili. Kuna wakati watu tunatumia maneno haya mawili yaani roho na nafsi interchangeably. Utasikia fulani ana roho mbaya. Hapa anakusudia kusema maamuzi ya mtu huyu hayampendelei yeye. Kwangu mimi nafsi ni kituo cha maamuzi katika mwili.
 
Mwili ni HALISI..... ni kila kitu ulichonacho na kinaonekana

Mwili na Roho SI HALISI...... ni vitu ambavyo vimebuniwa na kupewa majina ili kuelezea jinsi binadamu anavyo chakata maisha

Nafsi inaelezea kuhusu tabia na fikra za binadamu wakati Roho imekaa kiimani zaidi lakini mwili upo physically
 
Mwili ni hicho kiwiliwili chako chote.

Nafsi na roho ni kitu kimoja isipokuwa kuna majukumu ya roho na kuna majukumu ya kinafsi.

Majukumu ya kiroho ya kwanza ni yale uliyopewa toka kuumbwa kwako, nafsi ni yale mapya roho yako inayojifundisha kila siku unayoishi duniani.

Unaweza kuwa na nafsi zaidi ya moja kwenye kiwiliwili chako.

Majukumu ya mwili, nafsi na roho ni "mtambuka" yana muingiliano.

Elimu ya roho Mwenyezi Mungu kawapa wachache sana na kwa uchache sana.

Kingereza Roho ni "Spirit" na Nafsi ni "Psychology".

Kiarabu nafsi ni "nafs" na roho ni "
Kwa hiyo inawezekana ikawa jukumu lako la kiroho ilikua uwe Daktari maisha yakakufundisha uwe askari kwa hiyo unakua umebeba nafsi mpya kinyume na roho yako sio yaani kuacha lile jukumu au lengo la msingi, NB:hili naona ni tatizo linalotusumbua wengi maishani kuwa na multiple self within one spirit then tunaondoka kwenye kusudi kuu lilotuleta ulimwenguni.
 
Kwa hiyo inawezekana ikawa jukumu lako la kiroho ilikua uwe Daktari maisha yakakufundisha uwe askari kwa hiyo unakua umebeba nafsi mpya kinyume na roho yako sio yaani kuacha lile jukumu au lengo la msingi, NB:hili naona ni tatizo linalotusumbua wengi maishani kuwa na multiple self within one spirit then tunaondoka kwenye kusudi kuu lilotuleta ulimwenguni.
Nenda post #59 kuna video clip ina diagrams zinafafanuwa vizuri.
 
Hapa naona kuna mitazamo miwili; mtazamo wa kiimani na ule wa kisaikologia/ kibiolojia.Kiimani bado inabakia kuwa mwili ni chombo/ container ambamo ndani yake kuna roho na nafsi.Roho ni universal maana yake ni kuwa inamuunganisha mtu(mwili) na muumba wake kwa miili yote. Nafsi ni unique/hazifanani. Kila mwili una nafsi ya peke yake. Hakuna watu wawili wenye nafsi zinazofanana. Nafsi ni pamoja na mfumo wa kiakili, tabia za mtu kwa kadiri akili yake inavyomtuma, hisia za kupenda,kuchukia,kufurahi, huruma, ukatili nk.Ni vigumu wakati mwingine kutenga nafsi na roho.Hii ni kwa sababu vyote hivi ni vya kisaikologia zaidi kuliko kibiolojia. Hivyo ni rahisi kuvitumia kwa kuvipishanisha yaani interchangeably. Kwa hivyo hakuna mpaka mzuri wa kutenga roho na nafsi. Ni vigumu kusema kipi kinaongoza kingine.Hii ni sawa na mapacha wanaofanana, tofauti yao ni ndogo sana lakini ipo.
 
Tukienda kwenye biology mwili ni physical/tangible yaani unaonekana na unagusika. Roho ni kisaikolojia zaidi kuliko kibiolojia. Roho haigusiki, haionekani. Ni mental picture.Nafsi haionekani na haigusiki vilevile. Nafsi inajitokeza kwenye matendo ya mtu.Hapo tunajua tabia yake, anachopenda,asichopenda, ubunifu, ujinga wake yaani tunajua cognitive domain ya mtu huyo. Mtu anaweza kusema kuwa mtu anaweza kuitawala nafsi yake.Sitaki kuamini kuwa mtu anaweza kuitawala roho yake.Yaonekana kwangu kuwa roho inatawala nafsi. Yangu ni hayo tu kwa leo waungwana.
 
2f3e7e1045408cd0664bffd6f02f1338.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swali zuri hili na mara nyingi tunakuwa hatuwezi kuuliza maswali kama haya kwa sababu tunajifanya tunajua kwa hio tukiuliza maswali kama haya tunajiona wajinga,kwa hio tunabakia hatuulizi ili tuwe miongoni mwa wanaojua.

Roho, nafsi na mwili ni vitu tafauti na kila kimoja kina kazi yake ili kumtimiza mwanadamu awe kamili,ukikosa kimoja kama ya hivyo vitatu, uwawadamu wako utakuwa mashakani.

Tuanze na mwili
Mwili asili yake ni hapa duniani au kwenye dimension hii au realm hii ya dunia au existence, hapa ndio pahala pekee mwili unapoweza ku-exist
Kazi ya mwili kubwa ni ku-host nafsi,yaani nafsi inauvaa mwili na kuishi kwenye mwili, yaani kama vile unapokumbwa na shetani, Anakuwa ameuvaa mwili na anajitambulisha kama yeye na sio wewe tena. Na nafsi inafanya hivyo in a permanent basis yaani kwa namna ya kudumu.
Na mwili ni kama mashine inayomfanya kazi kwa ajili ya nafsi kuweza kuishi kwenye dunia hii,realm au dimension hii.
Mwili kazi yake ni kukusanya information kupitia hisia zake kuu tano,kuona,kusikia,kuonja,kuhisi,kunusa

Sasa twende kwenye roho au kwa kiingereza soul
Soul ni kiunganishi baina ya nafsi na mwili, soul au roho ndio muezeshaji mkubwa wa nafsi, soul ndio mkalimani anaetafsiri kwa nafsi kila kitu kinachofanywa na mwili hapa duniani,
Ndani ya soul kuna emotions,intellect and will, sijui kwa Kiswahili nisemeje hapa,mi sijui tunaitaje emotions kwa Kiswahili
Mwili kupitia hisia zake kuu tano unakusanya information na kupeleka kwenye soul kwa njia ya intellect(akili)
Akili inaweza kufanya kazi upitia hisia za mwli tu bila ya hisia za mwili akili haina uwezo wa kufanya kazi,macho yakiona kitu akili ina-process na kutafsiri ni nini macho yameona kupitia kumbukumbu za akili.
Maskio yakisikia kitu akili ina-process kisha inatafsiri nini maskio yamesikia
Na hisia nyengine kazi ndio hio hio

Sasa tuingie kwenye nafsi au sprit
Sprit ndio uhai wenyewe,yaani sprit ndio mtu mwenyewe naejelewa au kujitambua,utambulisho wa mtu hautokani na mwili wala roho wala akili
Utambulisho wa mtu mimi ni nani unatokana na nafsi au sprit
Kwenye sprit au nafsi kuna mambo matatu makuu
Kuna intuition,consciousness na submission to the source au God
Intuition ni uwezo wa kujua kitu bila ya kujua umejuaje, inatokea unajua tu bila kuambiwa ua kufundishwa
Consciousness ndio uhai wenyewe na kujitambua
Na submission to the source ni kusalimu amri kwenye chanzo cha sprit au nafsi na hiki tunakiita mungu au God
Vitu hivi vyote vipo kwenye nafsi au sprit
Nafsi au sprit haiwezi kuishi hapa duniani bila ya mwili na soul(roho) ndio mana mtu akiwa mzee na mwili umechoka nafsi inaondoka na mwili unaparalaiz na haujiwezi tena na hicho ndio kifo.
Pia mwli ukipata majanga makubwa kama ajali na ukawa hauwezi tena kui-support nafsi dakika hio hio nafsi inaruka permanently na kuondoka na hicho ndio kifo
Kifo ni kufariki
Fariki maana yake ni kutenga,au tunasema kufarakana maana ni kutengana
Kwa hio maana yake ni nafsi inafarakana na mwili hio ndio kufariki au kufa

Mi nadhani niishie hapa kama kunakuwa na Shaka tutaulizana
Mada hii nlielezea kwa kina kidogo kwenye uzi huu hapa chini wa kiingereza

Umeeleza vzr sana. Kwa maneno mengine rahisi (tukianza na mwili) mwili ni hii body (housing) tunayoiona. Ambayo kiuhalisia imejaa sense organs na organs nyingine ndani kufanya mwili uwepo. (Kwenye mwili ulieleza vzr sana).

Soul ambayo ni roho, kiuhalisia ni Ile nishati iliyopo kwenye ubongo ambayo tunaita akili. Ule uwezo wa akili kuchakata taarifa na hisia zinazoletwa na mwili (sense organs) naweza kusema ndo roho. Akili iko kwenye ubongo, ubongo ni vimajimaji vyeupe vizito ambavyo ni ngumu kueleza vinafanyaje kazi.... kiufupi tafsiri ya akili ni ngumu kufafanua lkn Ile nishati iliyomo kwenye akili kupokea taarifa na hisia, kuchakata taarifa na hisia, na kuzitunza na nyingine kuzirudisha kwenye mwili naweza kusema hicho ndo kinaitwa ROHO.

Tukimalizia na nafsi, nafsi ni sehemu ndani ya akili ambapo mkusanyiko wa taarifa na hisia zilizotunzwa na ubongo toka kuumbwa zilipo. So nafsi ni zile taarifa na hisia zilizohifadhiwa na ile sehemu ambayo imezitunza hizo. Taarifa hizo na hisia hizo ndizo hutengeneza mitazamo na imani ya mtu. Ndo utu wa mtu mwenyewe. Ndo mtu huyo. Generally, scientifically roho na nafsi viko kwenye ubongo lkn havionekani ni energy, yaani nishati not physical. Nafsi kuna watu wanaiita subconscious mind.

Nafsi inatengenezwa au hutokana na roho (au ubongo). Wakati taarifa na hisia zinazochakatwa na roho hutoka kwenye mwili.

Dini (Ukristo na Uislamu) na wanadini wali- copy mawazo ya philosophers kuyahusianisha hayo na dini au Mungu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom