Je, vipofu huota ndoto?

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,103
22,542
Salaam, shalom!!

Twende haraka kwenye mada, nimekuwa nikipost mada za intelligence ya Mbinguni katika jukwaa hili na zinahamishiwa majukwaa mengine,

Leo tuanze mwaka na swali hili, Je vipofu wa Kuzaliwa huota ndoto?

Kurahisisha upatikanaji wa jibu kuhusu ndoto za vipofu, tupate tafsiri ya

1. Silver cord/ Kamba ya Fedha. 2. Mtu/ Roho/ Spirit 3. NAFSI 4. Mwili. 5. NDOTO. 6. ULIMWENGU WA ROHO.


1. SILVER CORD/ KAMBA YA FEDHA.
Hiki ndicho kiunganishi kati ya MWILI wa mtu na Roho. Inapatikana katika ( Mhubiri 12:6): Or ever silver cord to be loosed. Ukisikia mtu amekata Kamba, ndo hii silver cord.

2. MTU/ Spirit/ Roho.

MTU- Ni ROHO, ANAYO NAFSI NA ANAISHI NDANI YA MWILI.

3. NAFSI./ Soul.
Mwili/ udongo ulipopuliziwa Pumzi ya uhai, ikazaliwa NAFSI. (Mwanzo 2:7) Ikumbukwe, Pumzi ya uhai ndiyo Roho.

NAFSI ndiyo inayobeba hisia, akili, uwezo wa kufanya maamuzi. Hapa ndipo panapochakata taarifa Kutoka kwenye Mwili na Kutoka kwenye Roho( mtu). Kumbuka hisia, akili, will vyote havishikiki katika mwili physical bt vipo.

4. MWILI.

Hili ni frame, kopo, vazi la mtu ambaye ni ROHO. Mwili Si mtu, Bali mwili ni vazi la mtu ambaye ni ROHO.

Katika mwili Kuna Ubongo, lakini akili Iko katika NAFSI.

Ukienda msibani, utasikia tunaenda kuaga mwili wa marehemu, marehemu na mwili ni vitu viwili tofauti.

5. NDOTO - Ni tukio halisi Si illusions kama wanasayansi wengi wanavyodhani. NDOTO ni tukio linalofanyika katika Ulimwengu wa Roho wa mwili au katika Ulimwengu wa Roho usioonekana.

NDOTO type 1- Hizi ni za Kutoka kwenye Mwili kupitia macho na mawazo ndizo ziitwazo ndoto kulingana na shughuli za Kila siku. ( Mhubiri 5:3). NDOTO huja Kwa shughuli nyingi.

NDOTO TYPE 2- Hizi ni Kutoka katika Roho, NAFSI inazipokea na akili itatunza kumbukumbu, ukiamka, utakumbuka ulichoota. NDOTO hizo ni HALISI Si imagination, ni wewe ambaye ni ROHO Huwa unaona au kwenda na kutuma taarifa katika NAFSI kupitia silver cord.

(Ayoub 33:15) katika ndoto, katika maono ya usiku, USINGIZI mzito uwajiliapo watu, katika USINGIZI kitandani.

6. ULIMWENGU WA ROHO.

Kwakuwa mtu ni ROHO anayo NAFSI na anaishi ndani ya MWILI, anapata na kutunza taarifa zote katika kitu kinachoitwa NAFSI.

Matukio yanayotengenezwa katika Ulimwengu wa mwili, NAFSI itayachakata na utayaota kupitia akili iliyo ndani ya NAFSI.

Matukio yaliyotokea kwenye Ulimwengu wa Roho, ,utayapata sababu silver cord imeungwa na mwili, NAFSI itakuletea tukio Hilo halisi kupitia ndoto, na ndoto zote ziko katika Ulimwengu wa Roho wa Nuru au Giza.


Hivyo mtu kipofu, kwakuwa Yeye ni ROHO, tutakuwa kwenye nafasi nzuri kujua ikiwa anaota ndoto au la. Na ikiwa anaota, ni Kwa mfumo upi?

MY LIFE EXPERIENCE.

Nimewahi Kutoka ndani ya MWILI wangu nikiwa mdogo na nikaenda mbali sana pazuri mno na kuona vitu ambavyo sijawahi kuviona duniani.

Swali ni je, vipofu waliotoka ndani ya miili Yao kama Mimi nilivyotoka ndani ya MWILI wangu, wanaweza kuona? Maana Mimi nilivyotoka ndani ya MWILI wangu sikutumia macho ya MWILI, kumbuka mwili niliuacha chumbani.

Cc:Sea Beast

Karibuni🙏
 
Una ushahidi?

Kuna kitu nataka tujifunze hapa.
Hahahahahaha mkuu,
Ukiwaona wakipita utahisi wapo wapo tu. Ila ukikaa nao,kwa karibu,utagundua kuna watu wenye macho,lakini hata akili zao hazifikii za hawa unaoulizia.
Binafsi nilichogundua,sehemu ya macho,walipewa sensi nyingine na inafanya kazi. Kwani unadhani mfano ukiingia ndani bila kubisha hodi haelewi kwamba kuna mtu kaingia?
Wapo vizuri sana. Wanasoma,yupo mmoja ana PHD. Sasa kwenye ndoto,huongea na watu,husimuliwa na wanavutaga picha ya simulizi. Kwa hiyo,kasoro tu macho,maisha mengine ni kama ya watu wa kawaida. Japo hawa viumbe hasa walioelimika,ni wabaguzi sana. Kama huna tatizo kama lao,kukuamini ni ngumu. Jiulize inapofikia hatua ya kuoana wao kwa wao
 
Hahahahahaha mkuu,
Ukiwaona wakipita utahisi wapo wapo tu. Ila ukikaa nao,kwa karibu,utagundua kuna watu wenye macho,lakini hata akili zao hazifikii za hawa unaoulizia.
Binafsi nilichogundua,sehemu ya macho,walipewa sensi nyingine na inafanya kazi. Kwani unadhani mfano ukiingia ndani bila kubisha hodi haelewi kwamba kuna mtu kaingia?
Wapo vizuri sana. Wanasoma,yupo mmoja ana PHD. Sasa kwenye ndoto,huongea na watu,husimuliwa na wanavutaga picha ya simulizi. Kwa hiyo,kasoro tu macho,maisha mengine ni kama ya watu wa kawaida. Japo hawa viumbe hasa walioelimika,ni wabaguzi sana. Kama huna tatizo kama lao,kukuamini ni ngumu. Jiulize inapofikia hatua ya kuoana wao kwa wao
Hapo kwenye kuvuta picha kutokana na wanachogusa au kusikia ndipo penye utata ningependa kupata majibu,

Taswira Yao inatengenezwaje?
 
Swali lako lisipuuzwe. Lijibiwe kitaalamu na ki ushahidi na sio kihisia na kwa dhana
Unajua nini darcity , kwa mtu asiewaelewa ni haki kuwaza wanaishije.
Tofauti na watu wenye macho, ni kwamba kila kitu huwachukua mda kukamilisha. Wanafua nguo, wanadeki,wanapika balaa. Humenya viazi mwenyewe,atawasha jiko au gesi,atapika na atakupakulia.
-Humimina maji kwenye glass na hamwagi
-Huweza kutambua rangi ya nguo anayoenda kuvaa(anakuwa ameshakalili,ila ukimpa nguo yake atakwambia ina rangi gani)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom