Swali zuri hili na mara nyingi tunakuwa hatuwezi kuuliza maswali kama haya kwa sababu tunajifanya tunajua kwa hio tukiuliza maswali kama haya tunajiona wajinga,kwa hio tunabakia hatuulizi ili tuwe miongoni mwa wanaojua.
Roho, nafsi na mwili ni vitu tafauti na kila kimoja kina kazi yake ili kumtimiza mwanadamu awe kamili,ukikosa kimoja kama ya hivyo vitatu, uwawadamu wako utakuwa mashakani.
Tuanze na mwili
Mwili asili yake ni hapa duniani au kwenye dimension hii au realm hii ya dunia au existence, hapa ndio pahala pekee mwili unapoweza ku-exist
Kazi ya mwili kubwa ni ku-host nafsi,yaani nafsi inauvaa mwili na kuishi kwenye mwili, yaani kama vile unapokumbwa na shetani, Anakuwa ameuvaa mwili na anajitambulisha kama yeye na sio wewe tena. Na nafsi inafanya hivyo in a permanent basis yaani kwa namna ya kudumu.
Na mwili ni kama mashine inayomfanya kazi kwa ajili ya nafsi kuweza kuishi kwenye dunia hii,realm au dimension hii.
Mwili kazi yake ni kukusanya information kupitia hisia zake kuu tano,kuona,kusikia,kuonja,kuhisi,kunusa
Sasa twende kwenye roho au kwa kiingereza soul
Soul ni kiunganishi baina ya nafsi na mwili, soul au roho ndio muezeshaji mkubwa wa nafsi, soul ndio mkalimani anaetafsiri kwa nafsi kila kitu kinachofanywa na mwili hapa duniani,
Ndani ya soul kuna emotions,intellect and will, sijui kwa Kiswahili nisemeje hapa,mi sijui tunaitaje emotions kwa Kiswahili
Mwili kupitia hisia zake kuu tano unakusanya information na kupeleka kwenye soul kwa njia ya intellect(akili)
Akili inaweza kufanya kazi upitia hisia za mwli tu bila ya hisia za mwili akili haina uwezo wa kufanya kazi,macho yakiona kitu akili ina-process na kutafsiri ni nini macho yameona kupitia kumbukumbu za akili.
Maskio yakisikia kitu akili ina-process kisha inatafsiri nini maskio yamesikia
Na hisia nyengine kazi ndio hio hio
Sasa tuingie kwenye nafsi au sprit
Sprit ndio uhai wenyewe,yaani sprit ndio mtu mwenyewe naejelewa au kujitambua,utambulisho wa mtu hautokani na mwili wala roho wala akili
Utambulisho wa mtu mimi ni nani unatokana na nafsi au sprit
Kwenye sprit au nafsi kuna mambo matatu makuu
Kuna intuition,consciousness na submission to the source au God
Intuition ni uwezo wa kujua kitu bila ya kujua umejuaje, inatokea unajua tu bila kuambiwa ua kufundishwa
Consciousness ndio uhai wenyewe na kujitambua
Na submission to the source ni kusalimu amri kwenye chanzo cha sprit au nafsi na hiki tunakiita mungu au God
Vitu hivi vyote vipo kwenye nafsi au sprit
Nafsi au sprit haiwezi kuishi hapa duniani bila ya mwili na soul(roho) ndio mana mtu akiwa mzee na mwili umechoka nafsi inaondoka na mwili unaparalaiz na haujiwezi tena na hicho ndio kifo.
Pia mwli ukipata majanga makubwa kama ajali na ukawa hauwezi tena kui-support nafsi dakika hio hio nafsi inaruka permanently na kuondoka na hicho ndio kifo
Kifo ni kufariki
Fariki maana yake ni kutenga,au tunasema kufarakana maana ni kutengana
Kwa hio maana yake ni nafsi inafarakana na mwili hio ndio kufariki au kufa
Mi nadhani niishie hapa kama kunakuwa na Shaka tutaulizana
Mada hii nlielezea kwa kina kidogo kwenye uzi huu hapa chini wa kiingereza
What is spiritual awakening? Spiritual Awakening means that you have realized that you are an Immortal and Eternal Spiritual Being, not a Mortal Human Body. Where do we come from? God, or Divine Intelligence, is not a Person but a Neutral Power with the Potential for Unlimited Creation. God...
www.jamiiforums.com