Ni vyema ila nilikua nashauri kungekua na midahalo ya aina hii kila wakati ili kuweza kujua masuala muhimu ya nchi yetu,lakini sidhani kama kunatakiwa kuwe na watu maalum wa kujibu maswali hayo ila kuwe na upande wa serikali na upande wa pili.Swali linaweza kuulizwa na member yoyote wa JF na upande husika ukatakiwa kujibu au kutafuta jibu kwa muda watakaoweza bila kikomo.Atakaejibu swali sio lazima atoke serikalini,anaweza kuwa yoyote anaeisuport serikali kwenye suala husika,kama jibu halitawaridhizisha waulizaji wataweza kuendelea kudebate.Ukura huo nashauri usiwe na mwisho ili yoyote akitaka ufafanuzi au akauliza swali ambalo lilishaulizwa na likajibiwa aelekezwe ili apate jibu kwenye ukurasa huo.Ni hayo tu!