🧠 Intuition vs Reasoning: Ipi Inapaswa Kuongoza?

Nyakati hizo za mamilioni ya miaka iliyopita, nyakati ambazo mwanadamu yupo katika hatua za mwanzo za evolution, nyakati ambazo ubongo ulikuwa haujakua kwa kiwango cha sasa ukiwa tu kama brain stem mwanzoni mwa uti wa mgongo; emotional centre pekee ndio ilikuwa ipo, sawa na primates wengine.

Emotional centre ndio mahali ambapo hisia na instincts mbali mbali zilitengenezwa na kuhifadhiwa, hakukua na cognitive centre, cortex na neocortex. Hisia hizo ndio zilifanya mwanadamu aweze kupona katika mazingira magumu na hatarishi sana ya wakati huo.

Miaka maelfu ikasonga, ubongo ukakua na parts zinazohusika na reasoning zilitengenezwa. Reasoning ndio ikapelekea dunia ya kisasa yenye vumbuzi nyingi ambazo zilipelekea mwanadamu kuyatawala mazingira vizuri na kupunguza kabisa hatari za hapo kale.

Baada ya hayo, sehemu za kale za ubongo bado tunazo na ingawa kuna wakati hisia zikiwa kali zinazishinda sehemu za reasoning lakini uhalisia ni kwamba sehemu hizo mbili zinashirikiana katika kuleta majibu yenye logic.

Mwanadamu ili afanikiwe na kufiti vizuri katika jamii anahitaji skills zote mbili emotional intelligence na cognitive intelligence
 
Shida ya kusikiliza sauti ya ndani ni huwa inaniacha na wasiwasi sana.Kuna siku huwa nakuwa na mipango ya safari,sasa intuition zangu zikinambia 'usiende leo' basi hiyo safari nashindwa niende lini halafu mbaya zaidi inakuwa ya lazima kwenye wiki husika.
 
Imewahi kutokea ukakaidi intuition yako likakukuta jambo?
 
Ndiyo vinaweza kufanya kazi kwa pamoja. Mimi sijui inanitokeaje ila huwa sometime najiona mchawi, Nafikiri Mwili unahitaji balance kwenye kila kitu chake. Mfano akili na mwili jinsi vinavyoreact wakati tofauti
Unaposema kama mchawi una maana gani mkuu?
 
Kwa hayo matukio umehitimisha intuition na reasoning havika chungu kimoja?

Huoni kama wewe ndio ulishindwa kufanyia kazi intuition yako kwa usahihi?
 
Kwa hayo matukio umehitimisha intuition na reasoning havika chungu kimoja?

Huoni kama wewe ndio ulishindwa kufanyia kazi intuition yako kwa usahihi?
Hisia nyingi zinazosababushwa na intuition, kwa akili ya kawaida huwa hayaelezeki.

Sauti inakuambia usiende huko, haikuambii sababu ya kutokwenda, hapo unafanya reasoning kivipi?

Ukitii hiyo sauti, unaweza ukaja kujua kule unakokwenda, majambazi yalivamia hilo eneo, wakaua, au ajali ya gari nk.
 
Sasa unataka tena sauti ikupe sababu
Sababu unazitafuta mwenyewe kwa kutumia reasoning ambayo mara nyingi ni uzoefu

Mimi pia nimesema huko juu ni mara kadhaa nimekumbwa na majanga kwa kupuuza intuition yangu pengine ni kwa sababu nilishindwa kutumia reasoning kufikia muafaka

Na ndio nikaendelea kuuliza
Je intuition na Reasoning haviwezi kufanya kazi pamoja?
Ili kuepsha majuto
 
Intuition Inakuja kama umeme vile hauna muda wa kufikiri na wala Huna sababu za kufanya unajikuta Tu hata sekunde tano hazijafika tayari umeamua tena inahitaji Utulivu mkubwa Sana haihitaji hofu wala stress, ukiona unaanza kufikiri Tu ndo reasoning inaanza sasa na Ukiendelea zaidi bila stop Unakuwa overthinker na mwishoni lazima uharibikiwe... Intuition ni sasa, inaangalia sasa hivi tena Kwa haraka bila muda wa kufikiria, ujinga wake kukupeleka Chaka ni dakika sifuri tu ndio maana inahitaji uwe na Utulivu kwenye maisha kitu ambacho ni ngumu sasa so Chaka lazima uingie.
 
Noma sana mkuu
 
Denial of gut feelings ndo chanzo cha majuto mengi.

Mimi mwenyewe Nime delay kwenye vitu vingi kwa sababu ya kifikiri sana
 
Asante kwa maoni
Naunga mkono hoja yako

Sometimes intuition inaweza kukuingiza chaka
Lakini je reasoning na intuition haviwezi kufanya kazi kama couple ili kuleta matokea positive?

Intuition ikuingize chaka!! Labda utakuwa unaichanganya na vitu vingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…