Interpol wanasa bilionea mwingine Arusha

Feedback

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
7,988
4,507
Wakili maarufu jijini Arusha, anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kukutwa na kiasi kikubwa cha fedha kwenye akiba yake binafsi, zinazodaiwa kuingia kwa njia isiyo halali. Wakili huyo aliyejijengea umaarufu nchini kutokana na uendeshaji kesi zake, anadaiwa kukamatwa Agosti 2, mwaka huu wakati akiendesha gari lake la kifahari aina ya Escalade, Polisi wa Kimataifa Interpol walimshikilia kabla ya kumfikisha Kituo Kikuu cha Polisi.

Inadaiwa chanzo cha Interpol kufuatilia nyendo zake, inatokana na akiba ya wakili huyo kukutwa na kiasi cha zaidi ya Sh30 bilioni zinazodaiwa kuingizwa njia zisizo halali.

Thomas Mashalla, Arusha WAKILI maarufu jijini Arusha, anadaiwa kushikiliwa na polisi kwa tuhuma za kukutwa na kiasi kikubwa cha fedha kwenye akiba yake binafsi, zinazodaiwa kuingia kwa njia isiyo halali.

Wakili huyo aliyejijengea umaarufu nchini kutokana na uendeshaji kesi zake, anadaiwa kukamatwa Agosti 2, mwaka huu wakati akiendesha gari lake la kifahari aina ya Escalade, Polisi wa Kimataifa Interpol walishikilia kabla ya kumfikisha Kituo Kikuu cha Polisi.

Taarifa zilipatikana zinadai ya kuwa, kushikiliwa kwa wakili huyo kunafuatia polisi nchini kufuatilia nyendo zake kwa kipindi kirefu kuhusiana na shughuli zake, huku wakihofia kiasi kikubwa cha fedha kilichokutwa kwenye akaunti yake binafsi kwenye benki moja nchini.Pia, taarifa hizo zinadai wakili huyo alikamatwa majira ya usiku na kwamba, kabla ya Interpol kumfikisha Kituo Kikuu cha Polisi walifanya upekuzi kwenye nyumba yake iliyopo mkoani Arusha.

Vyanzo vya habari vinadai kuwa, baada ya polisi hao kufanya upekuzi wa kina sehemu hizo mbili walimfikisha Kituo Kikuu cha Polisi ili kuruhusu hatua nyingine kufuata.Taarifa zinadai kuwa, wakati anakamatwa ndani ya gari alikutwa na zaidi ya Sh20 milioni na kwamba, baada ya kumhoji juu ya kiasi hicho cha fedha, inadaiwa aliwajibu hizo zilikuwa kwa ajili ya matumizi yake madogo.

"Walimkamata akiwa anaendesha gari lake hapa mjini, lakini ndani ya gari walikuta Sh20 milioni, walipomuuliza aliwajibu kuwa hizo ni kwa ajili ya matumizi yake madogo madogo," kilisema chanzo cha habari. Inadaiwa chanzo cha polisi kufuatilia nyendo zake, inatokana na akiba ya wakili huyo kukutwa na kiasi cha zaidi ya Sh30 bilioni zinazodaiwa kuingizwa njia zisizo halali.

Pia, inadaiwa polisi walikuwa na mashaka na gari analotumia kuingizwa nchini kinyemela.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye, alipoulizwa kuhusu taarifa hizo, hakukiri wala kukataa zaidi ya alisema suala hilo liko ngazi za juu, hawezi kuzungumzia.

"Kwa kweli hilo suala liko juu ya ngazi yangu, siwezi kulizungumzia chochote kwa sasa hadi nipate idhini kutoka kwa wakubwa wangu," alisema Andengenye.

Andengenye alisema anasubiri taarifa kutoka Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam na akipata kibali atalitolea ufafanuzi.Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) tawi la Arusha, Duncan Ooola, alikiri kukamatwa kwa wakili huyo na kwamba, walipofuatilia waliambiwa anachunguzwa na polisi.

"Ni kweli wamemkamata (jina tunalo) Jumanne, lakini sijui saa ngapi, tulikwenda polisi kujua chanzo walitwambia anachunguzwa, hiyo ndiyo taarifa ninayoweza kukupa," alisema Ooola.

Source: Mwananchi
 
ningekuwa na uwezo hawa wote napiga shaba. Tatizo ni serkali legelege ilitakiwa kwanza wazipige pin hizo hela halafu wamwambie amezipata wapi ?
 
I am not that credulous to accept anything coming my way. This thread is akin to Shimbo's story and will equally end up thrashed. We have a lot of sensitive and exigent issues requiring swift solutions, rather than engaging into discussing slanderous tales.
 
Afadhali kwa huyu hata ni mfanyabiashara toka alipotoka chuo. Kuna watumishi wa Umma toka wamalize chuo, Mishahara na paosho zao zinajulikana. Hawajawahi kufanya biashara ya aina yeyote, Hata ya ubuyu. Anaishi nyumba ya milioni 800, ana magari kibao ya milioni zaidi ya 80. Na bank ana zaidi ya milioni 200.

MBONA HAWAFUATILII TUJUE WAMETOA WAPI? Sipingi kwa wafanyabiashra kufuatiliwa, ILA TUNGEANZA KWA WATUMISHI WETU WA UMMA!
 
Kumbe haya mamlaka tumeyakabidhi Interpol, poor Tanzania !

Inaelekea hivyo Mkuu maana kule TAKUKURU kumejaa mafisadi tu na siyo siri kwamba kazi ya kupambana na mafisadi na watoa/wapokea rushwa imewashinda.
 
Selikali inamuogopa Alex Massawe kama vile selikali ya Colombia ilivyokuwa inamuogopa Pablo Escobal. Haya yote utasikia mwisho wa siku yanatoweka kama barafu mbele ya joto!
 
Selikali inamuogopa Alex Massawe kama vile selikali ya Colombia ilivyokuwa inamuogopa Pablo Escobal. Haya yote utasikia mwisho wa siku yanatoweka kama barafu mbele ya joto!

Kumbuka pia amekua mdhamini wa CCM for many years, ameanza kujenga jina ndani ya chama toka zamani. Infact wakuu wapolisi mpaka jeshi wanamfahamu vizuri including Zombe.
 
Naona ni mwendo wa tatu tatu tu!!!, trilioni 3, bilioni 30 na not too long kuna bilioni 300 inakuja!!!!
 
Wakili maarufu nchini akamatwa akituhumiwa kukutwa na fedha
Send to a friend
Friday, 05 August 2011 20:52

Thomas Mashalla, Arusha
WAKILI maarufu jijini Arusha, anadaiwa kushikiliwa na polisi kwa tuhuma za kukutwa na kiasi kikubwa cha fedha kwenye akiba yake binafsi, zinazodaiwa kuingia kwa njia isiyo halali.

Wakili huyo aliyejijengea umaarufu nchini kutokana na uendeshaji kesi zake, anadaiwa kukamatwa Agosti 2, mwaka huu wakati akiendesha gari lake la kifahari aina ya Escalade, Polisi wa Kimataifa Interpol walishikilia kabla ya kumfikisha Kituo Kikuu cha Polisi.

Taarifa zilipatikana zinadai ya kuwa, kushikiliwa kwa wakili huyo kunafuatia polisi nchini kufuatilia nyendo zake kwa kipindi kirefu kuhusiana na shughuli zake, huku wakihofia kiasi kikubwa cha fedha kilichokutwa kwenye akaunti yake binafsi kwenye benki moja nchini.Pia, taarifa hizo zinadai wakili huyo alikamatwa majira ya usiku na kwamba, kabla ya Interpol kumfikisha Kituo Kikuu cha Polisi walifanya upekuzi kwenye nyumba yake iliyopo mkoani Arusha.

Vyanzo vya habari vinadai kuwa, baada ya polisi hao kufanya upekuzi wa kina sehemu hizo mbili walimfikisha Kituo Kikuu cha Polisi ili kuruhusu hatua nyingine kufuata.Taarifa zinadai kuwa, wakati anakamatwa ndani ya gari alikutwa na zaidi ya Sh20 milioni na kwamba, baada ya kumhoji juu ya kiasi hicho cha fedha, inadaiwa aliwajibu hizo zilikuwa kwa ajili ya matumizi yake madogo.

“Walimkamata akiwa anaendesha gari lake hapa mjini, lakini ndani ya gari walikuta Sh20 milioni, walipomuuliza aliwajibu kuwa hizo ni kwa ajili ya matumizi yake madogo madogo,” kilisema chanzo cha habari. Inadaiwa chanzo cha polisi kufuatilia nyendo zake, inatokana na akiba ya wakili huyo kukutwa na kiasi cha zaidi ya Sh30 bilioni zinazodaiwa kuingizwa njia zisizo halali.

Pia, inadaiwa polisi walikuwa na mashaka na gari analotumia kuingizwa nchini kinyemela.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye, alipoulizwa kuhusu taarifa hizo, hakukiri wala kukataa zaidi ya alisema suala hilo liko ngazi za juu, hawezi kuzungumzia.

“Kwa kweli hilo suala liko juu ya ngazi yangu, siwezi kulizungumzia chochote kwa sasa hadi nipate idhini kutoka kwa wakubwa wangu,” alisema Andengenye.

Andengenye alisema anasubiri taarifa kutoka Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam na akipata kibali atalitolea ufafanuzi.Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) tawi la Arusha, Duncan Ooola, alikiri kukamatwa kwa wakili huyo na kwamba, walipofuatilia waliambiwa anachunguzwa na polisi.

“Ni kweli wamemkamata (jina tunalo) Jumanne, lakini sijui saa ngapi, tulikwenda polisi kujua chanzo walitwambia anachunguzwa, hiyo ndiyo taarifa ninayoweza kukupa,” alisema Ooola.
 
pamoja na gazeti hili kumwogopa hata kumtaja jina yasadikiwa kuwa Ni Mwale....................................ndizo habari zilizozagaa jijini Arusha..........................
 
Kumbe haya mamlaka tumeyakabidhi Interpol, poor Tanzania !

Mimi ntashukuru kama ni kweli, tuwape tu vyombo vyote mpaka TISS. Our security institutions dont care about our security, if privatisation is possible, it will be better. Wanaangaika na CHADEMA, wakati nchi imejaa majambazi kila kona.
 
Back
Top Bottom