Aomba kupelekwa polisi baada ya kugonga gari la gharama

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
439
Reaction score
1,070
Mzozo wa barabarani umejitokeza baada ya dereva wa pikipiki ya miguu mitatu (Toyo) kugonga gari la kifahari, kisha kuomba apelekwe kituo cha polisi kuliko kutakiwa kulipa gharama za matengenezo ambazo hana uwezo nazo.

Tukio hilo limetokea baada ya mfumo wa breki wa Toyo hiyo kukatika ikiwa safarini, hatua iliyosababisha chombo hicho kupoteza mwelekeo na kugonga gari hilo.

Baada ya ajali hiyo, mmiliki wa gari alimwomba dereva huyo amsaidie kiasi kidogo cha fedha ili kuwezesha matengenezo ya gari lake. Hata hivyo, dereva wa Toyo alieleza wazi kuwa kutokana na hali yake ya kiuchumi na kipato chake kidogo, hana uwezo kabisa wa kulipia uharibifu huo.

Dereva huyo aliongeza kuwa yupo tayari kupelekwa kituo cha polisi na kutumikia kifungo kuliko kuingia kwenye deni kubwa, hata kama hatua hiyo itaifanya familia yake kupitia changamoto za kimaisha bila yeye kuwepo.
 
View attachment 3668325
Kama ana leseni na toyo ina bima aende pooisi atalupa fine tu na huyo mwenye gari atalipwa na bima.Hakuna kufungwa Wala nini.Fine uenyewe 20k tu
 
Back
Top Bottom