Ingekuwaje wangekuwa Wachagga?

Status
Not open for further replies.
Dr Hosea ana Usukuma gani? Hamuifahamu vizuri wilaya ya Kahama. Hata hivyo, kwa IDADI yao Wasukuma nafasi wanazoshika bado ni chache mno.
 
Hakuna jipya,mnaturudisha kule kule mwaka 1947. Kama mtu unawaza kikabila mpaka leo hii,kuna shida hapo.
 
Na hao unawaowashikia bango pia wao si wasukuma ni watanzania!

Nimeipenda hii comment. Unajua wasukuma wanapatikana Tabora, Shinyanga, Mwanza na labda sehemu nyingine zinazozunguka kanda ya ziwa. Hivi hawa wangekuwa wakabila na uwingi wao huu si ingelikuwa balaa? Nafasi zao wengi wamepata sio kwa sababu ya ukabila..ni utanzania!! Labda ungesema wasukuma wakiwa wengi ngoma za kucheza na nyoka na matambiko yatazidi naweza kukuelewa
 
Mwanzisha thread had a point kwamba Wachagga walijadiliwa sana bali ilipokuja kwa Wasukuma, kukawa hakuna mjadala.
The point is short and clear, Wasukuma ni wengi lakini hawana ukabila. Wachagga ni wachache lakini wana ukabila.

Kutokana na hisia za ukabila, watu huwa wana kama ka chuki fulani na Wachagga ndio maana ni ngumu kwa Mchagga au Nshomile kuwa rais wa nchi hii.

Hayo ni yale makubwa, acha madogo madogo ya Wachagga na Wasukuma.. Mimi nimetokea inter marriage family ya Baba Msukuma na Mama Mchagga. Mama alishika usukani, baba akajenga Moshi, kila Krismasi ni Moshi. Ndugu wa baba walimsema Baba na kudai huyu mama wa Kichagaa si bure. Baba alishika msimamo 'nimependa'. Ndugu muhimu nyumbani ni wale wa mama, wa baba kero.

Ikaja zamu yangu, kupitia mfluence ya mama nikaoa uchagani ila nikadhamiria niwe na msimamo indepedent sio kama baba. No kujenga Moshi, no safari za Moshi wakati wa Krismasi. Ilifikia wakati kulizuka mgogoro mkubwa na wakwe kisa nimedharau kupeleka familia mzima Moshi kwenye ubarikio wa ukweni.

Nimekuja ku learn the hard way, japo mke wa kichagga amenipenda, pesa is a big deal kwake na familia yake. Nilishaendeshwa puta mpaka tukahamia London kubeba box hatimaye US kusaka more money. Kwa wife Mchagga, money was everything kwa mimi Msukuma, money is nothing. Nililazimisha kurudi Bongo, na ilikuwa shughuli....

Misimamo kama hiyo inasababisha ama ukubali kupelekwa pelekwa ama usaffer the consequences. Haya ni mambo ya ndani madogo madogo ya contrast za Wasukuma na Wachagga.

Pamoja na Usukuma wangu wote, sikumbuki kuwahi kusaidiwa na Msukuma yoyote kwa sababu ya kabila langu, my wife was very junior kazini kwake, baada ya boss Mchagga kujua kumbe ni Mchagga, alipanda cheo to seniority within no time, mshahara mnono na gari ya ofisi, mbona ningepandwa kichwani maana alinipita mshahara. Msimamo mkali wa masikini jeuri ulinisaidia.

Nenda sherehe za Wachagga na kina Nshomile, ni wao watupu, sometimes hata jirani kama ni vikabila havieleweki, hakuna kualikwa. Ukikutwa kuna wengine kwenye mikusanyiko yao, ujue ni 'friendship of convenience' Huu sasa sio ukabila tena bali ni ubaguzi wa kichini chini kujiona makabila yao ndio bora na makabila mengine yote silolote si chochote.

Tupende tusipende hili la Wasukuma kutokuwa na ukabila kumeisaidia sana nchi hii itawalike kwa amani. Kama na sisi tungeanza kucheza karata za ukabili, kwa wingi wa Wasukuma, hakuna mtu anaweza kuwa rais wa nchi hii bila kura za Kanda ya Ziwa.

Wasukuma wote kwenye nafasi za madaraka, wameyapata kwa merits na sio kwa kubebwa na ukabila. Na naamini kuchelewa kwa Mzee wa Vijisenti kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria, ni wanasubiri ku synchronise the connected dots na sio kwa sababu ya Usukuma wake.

Hata hivyo pole Mangi wewe, Mangi Mramba na Mjomba Yona na Mgonja, issue yao ni politics za kupandisha credibility ya Mkulu ready for 2010 tuu, hazina legal merits kubwa sana, kesi zitaisha na watakuwa aquinted so do Mangi Kweka na Semeji Liyumba maana wale wadada ni wetu sote.

No wonder story imetoka gazeti la Mangi.
 
Jiulize kama wateule hawa wangelikuwa ni Wachagga kelele za ukabila zingeweza kuwa zimeenea kiasi gani?

Kwani hapa waliwahi kujadiliwa sana watu wa kabila la Wachagga eti wapo wengi Ikulu, Ujenzi,Mambo ya Nje, TRA,BOT na ofisi nyeti za serikali, ila huko kote ni TRA tuu ndio Mkurugenzi mkuu ndio Mchagga .

Wasukuma ndio waliopo kwenye vyombo nyeti vya taifa hili.
1.Mkurugenzi Mkuu TAKUKURU- MSUKUMA.
2.Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka- DPP -MSUKUMA.
3.Mkurugenzi mkuu wa Upelelezi na Jinai -Msukuma.

Hivi wangelikuwa ni wakutoka Kilimanjaro ingekuwaje?

Na juzi kwenye utafiti wa lugha uliofanyika nchini ulionyesha kuwa Kisukuma ndio lugha inayozungumzwa kwa wingi zaidi Tanzania .

Mchaga anapenda sana pesa na biashara!... hapo juu bold & red hakuna pesa wala biashara, zaidi ya kuumiza kichwa na kuhatarisha maisha!.. kwa sasa panaoneka hotcake coz of EPA,... et al, otherwise no attraction kwa chaga pale.....

kama ulivyoainisha hapo juu, Cheki Mchaga alipo "TRA", hapa kuna pesa ya kufa mtu, kula kiulaini... tofauti na kushughulikia mafisadi na waharifu...
 
Jiulize kama wateule hawa wangelikuwa ni Wachagga kelele za ukabila zingeweza kuwa zimeenea kiasi gani?

Kwani hapa waliwahi kujadiliwa sana watu wa kabila la Wachagga eti wapo wengi Ikulu, Ujenzi,Mambo ya Nje, TRA,BOT na ofisi nyeti za serikali, ila huko kote ni TRA tuu ndio Mkurugenzi mkuu ndio Mchagga .

Wasukuma ndio waliopo kwenye vyombo nyeti vya taifa hili.
1.Mkurugenzi Mkuu TAKUKURU- MSUKUMA.
2.Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka- DPP -MSUKUMA.
3.Mkurugenzi mkuu wa Upelelezi na Jinai -Msukuma.

Hivi wangelikuwa ni wakutoka Kilimanjaro ingekuwaje?

Na juzi kwenye utafiti wa lugha uliofanyika nchini ulionyesha kuwa Kisukuma ndio lugha inayozungumzwa kwa wingi zaidi Tanzania .

Hizi nafasi zote ulizozitaja sio priority kwa wachaga kama unataka tuongee kuhusu wachaga. Weka post zenye mambo ya Fwezaaaa hapa uoneee. (Sorry JF members but this dude push me to comment. Aint a tribalist)
 
kwa Watanzania kuzungumzia ukabila leo ni ufinyu wa kufikiri, hapa wote tu watanzania. Wengine tulishasahau yanayoongelewa hapa, katika familia moja wapo waliooa wachanga, wahaya, wangoni na dada zetu kuolewa na wabena, wasambaa alimradi ni mchanganyiko maalumu.

Upendeleo ni hulka ya mtu binafsi na wala sio utamaduni wa kabila. Mchaga katuzidi wengine kwenye utafutaji fedha na huo ndio ukweli, iwe kwa njia haramu au halali, wengi wanaoa wanawake wa kichaga kutokana na tabia ya wanawake hao kuwa wachapa kazi na ushahidi wa hilo ni wengi wamewpiga hatua kimaendeleo. Mwanamke wa kichagaa hasugui ****** nyumbani kusubiri aletewe na mumewe naye anajishughulisha, akiona ajira hailipi anajiajiri, tuukubali ukweli ndipo tutabalike, lakini sio kulalamika kila siku.

Kutawaliwa na mwanamke hakuhusiani na kabila ni suala la mtu binafsi, mbona sisi wapo waliooa wachaga lakini Krismas zote wanaenda Kyela badala ya Moshi, na kama kujenga wamejenga Kyela kwanza kisha DSM. Kukubali kwako kujenga Moshi ni ama udhaifu au utashi wako mwenyewe lakini hauhusiani na ukabila. Vipi ambao wameoa wanawake wa makabila mengine lakini wanaendeshwa kama wafanyakazi wa nyumbani, nao tuwahusishe na kabila! Hapana, tubadilike tuachane na mawazo haya finyu.

Mungu Ibariki Tanzania
 
Mwanzisha thread had a point kwamba Wachagga walijadiliwa sana bali ilipokuja kwa Wasukuma, kukawa hakuna mjadala.
The point is short and clear, Wasukuma ni wengi lakini hawana ukabila. Wachagga ni wachache lakini wana ukabila.

Kutokana na hisia za ukabila, watu huwa wana kama ka chuki fulani na Wachagga ndio maana ni ngumu kwa Mchagga au Nshomile kuwa rais wa nchi hii.

Hayo ni yale makubwa, acha madogo madogo ya Wachagga na Wasukuma.. Mimi nimetokea inter marriage family ya Baba Msukuma na Mama Mchagga. Mama alishika usukani, baba akajenga Moshi, kila Krismasi ni Moshi. Ndugu wa baba walimsema Baba na kudai huyu mama wa Kichagaa si bure. Baba alishika msimamo 'nimependa'. Ndugu muhimu nyumbani ni wale wa mama, wa baba kero.

Ikaja zamu yangu, kupitia mfluence ya mama nikaoa uchagani ila nikadhamiria niwe na msimamo indepedent sio kama baba. No kujenga Moshi, no safari za Moshi wakati wa Krismasi. Ilifikia wakati kulizuka mgogoro mkubwa na wakwe kisa nimedharau kupeleka familia mzima Moshi kwenye ubarikio wa ukweni.

Nimekuja ku learn the hard way, japo mke wa kichagga amenipenda, pesa is a big deal kwake na familia yake. Nilishaendeshwa puta mpaka tukahamia London kubeba box hatimaye US kusaka more money. Kwa wife Mchagga, money was everything kwa mimi Msukuma, money is nothing. Nililazimisha kurudi Bongo, na ilikuwa shughuli....

Misimamo kama hiyo inasababisha ama ukubali kupelekwa pelekwa ama usaffer the consequences. Haya ni mambo ya ndani madogo madogo ya contrast za Wasukuma na Wachagga.

Pamoja na Usukuma wangu wote, sikumbuki kuwahi kusaidiwa na Msukuma yoyote kwa sababu ya kabila langu, my wife was very junior kazini kwake, baada ya boss Mchagga kujua kumbe ni Mchagga, alipanda cheo to seniority within no time, mshahara mnono na gari ya ofisi, mbona ningepandwa kichwani maana alinipita mshahara. Msimamo mkali wa masikini jeuri ulinisaidia.

Nenda sherehe za Wachagga na kina Nshomile, ni wao watupu, sometimes hata jirani kama ni vikabila havieleweki, hakuna kualikwa. Ukikutwa kuna wengine kwenye mikusanyiko yao, ujue ni 'friendship of convenience' Huu sasa sio ukabila tena bali ni ubaguzi wa kichini chini kujiona makabila yao ndio bora na makabila mengine yote silolote si chochote.

Tupende tusipende hili la Wasukuma kutokuwa na ukabila kumeisaidia sana nchi hii itawalike kwa amani. Kama na sisi tungeanza kucheza karata za ukabili, kwa wingi wa Wasukuma, hakuna mtu anaweza kuwa rais wa nchi hii bila kura za Kanda ya Ziwa.

Wasukuma wote kwenye nafasi za madaraka, wameyapata kwa merits na sio kwa kubebwa na ukabila. Na naamini kuchelewa kwa Mzee wa Vijisenti kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria, ni wanasubiri ku synchronise the connected dots na sio kwa sababu ya Usukuma wake.

Hata hivyo pole Mangi wewe, Mangi Mramba na Mjomba Yona na Mgonja, issue yao ni politics za kupandisha credibility ya Mkulu ready for 2010 tuu, hazina legal merits kubwa sana, kesi zitaisha na watakuwa aquinted so do Mangi Kweka na Semeji Liyumba maana wale wadada ni wetu sote.

No wonder story imetoka gazeti la Mangi.

Hivi kabila la wachaga ni lipi hasa? maana nijuavyo mimi,Mmachame hawaelewani kiluga na mkibosho au mmrangu au mrombo ambao na wao wamegawanyika sana Mkuu, mashati ,Usseri.

Naomba kuelimishwa hapo!
 
Unapokuwa na nji (nchi) ndogo kama Kilimanjaro lazima kuwepo na elimu ya kutosha na hilo ndilo Watanganyika walichofanya,,, kuungana na Kilimanjaro ili kupata uhuru na kiwezesha Tanganyika huru kuwa na Wataalamu.
Kwa msaada tu ni kuwa wakati wa kudai Uhuru mwalimu alikutana na Mangi Marealle kule UN akidai UHURU wa northern Province. Ilibidi wakae chini Marealle na Mwalimu na wakakubaliana kuunganisha nguvu zao ili kudai UHURU wa Tanganyika. Marealle alimwalika Mwalimu Kilimanjaro na katika ziara yake hiyo alimtembelea mlowezi mmoja to Jamaica na hapo ndipo alipokutana na secretary wake wa kwanza Lucy Lameck. Alikuwa msomi huyu pia na mwalimu aliazimwa ali amsaidie kazi za kupiga chapa za mambo mbali mbali ya nchi hii. Hili nalo tulilalamikie?
 
Mie sioni cha msingi kuhusu Takukuru au DPP sijui nani kuwa Mpogoro au Mndengereko au Mbudha, kama hana sifa hapo lingekuwa jambo! Haya yalikuwa mambo ya kale wakati wa ujima ambapo walipigana kwa sababu ya mali, hawakuona wala hawakuishi pamoja, leo sote tupo Dar, Mwanza, Arusha, Singida; tunaona na kuoleana na kusihi nyumba moja.

Huu sio wakati wa kuangali tena makabila yetu, tufanyeni kazi na tuwapeleke wanetu shule ili waweze kushindana katika soko, vinginevyo tutabaki tukijadili tulikotoka badala ya tuendako.

Ukweli unabaki, Wasukuma ndio kabila kubwa Tanzania lakini hawakupata fursa za shule mapema kulinganisha na wachaga, wahaya! Lakini isingekuwa ajabu hata idadi yao ingekuwa kubwa kuliko ilivyo sasa.

Nadhani hata tunapochagua viongozi katika maeneo mbalimbali sio kwa sababu ya Ukabila, ila atatuletea maendeleo gani katika eneo letu!
 
Ila kweli kwa Wachaga kutafuta shilingi!

Yaani ukimrusha pesa yake tu..atakutoa roho!

Nadhani land pressure imewapa akili hawa jamaa!
 
Huu sio wakati wa kuangali tena makabila yetu, tufanyeni kazi na tuwapeleke wanetu shule ili waweze kushindana katika soko, vinginevyo tutabaki tukijadili tulikotoka badala ya tuendako.

Nono
Aisee una mawazo kama unatoka kwetu vile? I mean it, kwa sababu huko kwetu huwa hatujali mtu alitoka wapi, bali anaenda wapi. Philosophy yako inafanana kabisa na kwetu Mtagata.

On the other note, watu wasio na makabila, wepesi kutukana makabila ya watu kwa sababu hawajui utamu wa kabila. Matokeo yake unamkuta mwanamme anamvalia mama mkwe taulo!
]
 
Mimi swali langu ni juu kuna undugu kati ya Feleshi na Chenge (siyo hilo la ukabila au undugu wa Watanzania wote)
 
This thread is a non-starter. Maana wasukuma wasingekuwa wastaarabu nchi isingekalika.
So mwanzisha thread, njoo kwa gia nyingine mwanawane.
Halafu unajua dada wa kichagga kwa wasukuma wanaoza sana? lol. Heshimu shemeji zako.
 
...bachoji bah mhilya duhu angoh?! .....amboh bamanile tulenah-'masekeni (segeni), maalmasi, madhahabu, mang'ombe, mhulu (mhuru genge), sungwi, masondwa, mabele, ngubo, mahama, ng'ong'osela, maliboto, manumbu, bubele, lunyenya, madoke, nembe, mashe, sato, nguryati, linyanza, maliwa, maguha, makubi (nzubo, lunani, matembele, mashiri, manyang'wanga, ndulu, lugaka), noni (jiiji, hungwe, dodorima, jolowe, topunda, n'helegani...), etc, etc..... maaayne - just luv it!!! :) :) :D
 
Last edited:

Ango nyanda ng'wenuyo alena tuja gete!
Yeeeee, nkooooiiiii, mmmmhhhh, wanitwala kukaya loluh. Bopulu, kwaree, mabele ga masungaa, ne komoni (konyagi orijino gete)!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom