Ingekuwa wewe ungefanyaje?

Ingekuwa wewe ungefanyaje?

Captain22

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2011
Posts
630
Reaction score
285
Jamaa yangu wa karibu ameoa na wana watoto watatu.

Miezi miwili iliyopita wife kamuaga anaenda kwa dada yake kumsaidia kwani yu mgonjwa.

Jamaa akamruhusu bila hiyana. Baadae mchana katika pitapita zake jamaa uso kwa uso na huyo dada aliyetajwa na mkewe kuwa mgonjwa. Kwa ustaarabu jamaa hukumuliza shemeji yake kulikoni mgonjwa kuzurura mjini.

Nae dada mtu akauliza hali ya mdogo wake. Ilipotimu saa 3 usiku mke akarudi kwa maelezo kuwa amechelewa kwa sababu mgonjwa hali yake bado mbaya. Jamaa akampa mkewe pole na bado anatafuta ushauri wa nini cha kufanya.

Je wewe ungefanyaje?
 
sasa ushauriwe nini hapa?
Kupanga ni kuchagua
 
Kama atataka amuulize, kama hataki asimuulize. Na atakapo jibiwa kama atataka akasirike, kama hataki amsamehe.
 
Ni mimi sijaelewa vizuri au??! Ni miezi miwili iliyopita na bado jamaa hajaelewa cha kufanya!!! Kama ni hivyo mwambie aendelee kutoelewa cha kufanya... Ilitakiwa siku iliyofata yeye na wife wake waende wakamuone 'mgonjwa'. Sasa mtu amezubaa miezi miwili imepita bado anatafuta cha kufanya!!
 
Binadamu tunatofautiana sana sana.Miezi miwili bila ya kuchukua maamuzi!Mwambie amuulize then jibu atakalopewa atuletee hapa ili tumshauri kwa hatua itakayofuata ikibidi.
 
Sema nae, ukimya mwingi utakuharibia ndoa yako!
Ngoja Lizzy atakushauri vizuri.
 
swali ningekua mimi,jibu ningempeleka kwa dada mgonjwa aendelee kumuuguza kwani ni mgonjwa wa akili ndio maana anazululazulula mtaani.
 
Ni mimi sijaelewa vizuri au??! Ni miezi miwili iliyopita na bado jamaa hajaelewa cha kufanya!!! Kama ni hivyo mwambie aendelee kutoelewa cha kufanya... Ilitakiwa siku iliyofata yeye na wife wake waende wakamuone 'mgonjwa'. Sasa mtu amezubaa miezi miwili imepita bado anatafuta cha kufanya!!

Si kwamba kazubaa kwa jinsi ninavyo mwelewa nahisi yupo kwenye denial window haamini kama ni kweli.
 
miezi miwili? mwambie siyo kweli atakuwa aliota tu au kumsaidia zaid mwambie when u r in deep shit dont open ur mouth.
 
Si kwamba kazubaa kwa jinsi ninavyo mwelewa nahisi yupo kwenye denial window haamini kama ni kweli.

Tabia mbaya sana! Kitu cha kuongea siku moja tu lakini kinarundikwa rohoni ili iweje?? Mwanaume kisasi weye, umeweka makosa mangapi moyoni mwako??
 
Mimi nampongeza huyo jamaa kwa kuzuia mihemko isiyo na maana,mke wake kamdanganya hilo linaeleweka,ishu ni kuwa alikoenda alienda kufanya nini,anaweza kuwa alienda kwenye mambo mengine ya kawaida tu ambayo sio kuzini japokua na hilo lipo.Ajiulize kama mke wake hua ana tabia ya kutokatoka kabla ya hapo.Pia baada ya hapo anatokatoka au vipi!
 
From the very first time I blessed my eyes on you,girl
My heart said follow through
But I know now that I'm way down on your line
But the waiting feeling's fine
So don't treat me like a puppet on a string
'cause I know how to do my thing
Don't talk to me as if you think I'm dumb
I wanna know when you're gonna come, 'see
I don't wanna wait in vain for your Love
I don't wanna wait in vain for your Love


Courtesy of Bob.
 
Back
Top Bottom