India yaonesha nia ya kupata Duma kutoka Kenya, siku chache baada ya kuipa mkopo wa Ksh. Bilioni 38

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Serikali ya India imeonyesha nia ya kupata duma kutoka Kenya wakati wa ziara ya Kiserikali ya Rais William Ruto katika taifa hilo la Asia.

Kama ilivyoripotiwa na The Indian Express, Wizara ya Mazingira ya India tayari imewasilisha pendekezo hilo lakini maelezo kuhusu idadi ya duma walioombwa, idadi ambayo Kenya iko tayari kutoa na muda wa kuwanunua ulikuwa haujafichuliwa kufikia wakati wa kuchapisha makala haya.

Chapisho hilo lilimnukuu afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya India ambaye alithibitisha kuwa Wizara ya Mazingira ya nchi hiyo iliwasilisha rasmi maombi ya kuwanunua duma hao kutoka kwa serikali ya Kenya.

India imekuza hamu kubwa ya kupata duma kwa kuhofia kwamba mnyama huyo anatoweka. Kwa hali ilivyo, Hifadhi ya Kitaifa ya Kuno, ambayo iko katika Jiji la Kaskazini la Pradesh ni nyumbani kwa duma 15 walionusurika.

Wakati wa mkutano wake na Rais William Ruto, Waziri Mkuu Narendra Modi alipongeza uamuzi wa Kenya wa kukubali kujiunga na Big Cat Alliance, kikundi ambacho lengo lake kuu ni kuhifadhi paka saba wakuu duniani, ambao ni pamoja na Chuimilia, simba, chui wa theluji, chui, jaguar, puma, na duma

Haya yanajiri baada ya India mnamo Jumanne kukubali kukopesha Kenya Ksh 38.3 bilioni, fedha zilizotengwa kwa ajili ya kuboresha sekta ya kilimo nchini.

Rais William Ruto na Waziri Mkuu Modi walishuhudia kutiwa saini kwa Hati 5 za Makubaliano (MOUs) kati ya mataifa hayo mawili.

Mikataba hiyo inahusisha sekta mbalimbali za kiuchumi, zikiwemo Biashara, Kilimo, Usalama na Mahusiano ya Nje.

India na Kenya pia zimejitolea kuimarisha ushirikiano wa pande zote katika uwanja wa kukabiliana na ugaidi.
 
Back
Top Bottom