Bodaboda waishitaki Serikali kwa madai ya kuwatelekeza katika mipango yao, wadai fidia ya Ksh. Bilioni 426 (Tsh. Trilioni 6.7)

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,625
ruto.jpg

Baadhi ya waendesha pikipiki (bodaboda) kutoka jijini Malindi wameamua kuchukua hatua ya kisheria dhidi ya serikali ya Kenya Kwanza, wakidai kuwa wamesahaulika katika mipango ya serikali na kusababisha hasara kubwa kifedha pamoja na matatizo ya kisaikolojia.

Kulingana na nyaraka za mahakama zilizoonyeshwa na Citizen Digital, waendesha bodaboda hao wanadai kuwa ahadi za wanachama wa chama cha kisiasa cha Kenya Kwanza zimeleta athari kubwa kwa biashara zao, na hivyo kuwasababishia hasara kubwa ya kifedha na kuharibu sifa na mwelekeo wa biashara zao.

Waendesha bodaboda hao wanasema wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2022, serikali ya Kenya Kwanza iliahidi kuwawezesha na kuinua maisha ya watu wanaojihusisha na biashara ya bodaboda pamoja na Mama Mboga, lakini hawajapata msaada huo kama ilivyokuwa imeahidiwa.

Malalamiko yaliyowasilishwa na waendesha bodaboda wa Malindi, Linda Jamii, na wengine, pia yanadai kwamba kaulimbiu ya Kenya Kwanza imeondolea watu wanaojihusisha na biashara ya bodaboda na Mama Mboga mapato yao kutokana na uadui unaotokana na kutofurahishwa kwa wananchi wa Kenya dhidi ya serikali ambayo wamedai imeshindwa kupunguza gharama kubwa za maisha.

Kupitia kaulimbiu ya Kenya Kwanza, waendesha bodaboda na wafanyabiashara wa Mama Mboga wanadai kuwa mapato yao yameshuka kwa asilimia 32 ambayo ni sawa na takribani Ksh. Bilioni 426 bilioni (sawa na trilioni 6.8 za kitanzania) na kuitaka Serikali isitoe kauli yoyote kuhusu biashara zao wakidai kuwa yanaweza kuwa na athari kubwa kwa haki zao na uhuru wa kufanya biashara.



=============

Boda Boda Riders Sue Gov't Over Campaign Slogan, Say It Has Caused Them Psychological Trauma

A section of boda boda operators have sued the Kenya Kwanza government for allegedly leaving them out of government plans.

In court papers seen by Citizen Digital, the boda boda riders argue that during the period leading the 2022 General Election Kenya Kwanza ran a campaign that was majorly centered around the empowerment and uplifting of the lives of the persons engaged in boda boda and Mama Mboga business.

The riders state that the Kenya Kwanza government has since “peddled a narrative that strictures of the current political government is comprised of the bodaboda and Mama Mboga wo/men, while in fact the same is utterly false and untrue.”

"THAT as a result of the impugned utterances by the Members of the 1st Respondent political science party, the people engaged in boda boss business to earn a living suffer massive financial losses, in the future irreparable harm to their goodwill and business signatures,” reads the court papers.

The petition filed by Malindi boda boda operators,Linda Jamii and others also states that the Kenya Kwanza slogan has deprived the boda boda and Mama Mboga business people of their income owing to the hostility from Kenyans’ dissatisfaction with the current government.

“Additionally, the utterances of the Members of the 1st Respondent political party that the current executive arm of the government of Kenyaiscomprised of the boda boda and Mama mboga wo/men subject thepersons engaged in boda boda and Mama Mbogabusiness topsychological trauma owing to the reduction in their sourceof incomeand hostility of the people of Kenya who are clearly dissatisfied with the government’s inability to bring down the cost of living,” the petition further reads.

They now want the government stopped from making utterances on Mama Mbona and Bodaboda claiming that it has an effect of threatening to violate the Petitioners’ rights and fundamental freedoms as illustrated

The petitioners say there is a depreciation of the earnings of the persons in the boda boda sector of about 32% due to the use of the term by Kenya Kwanza which translates to about Ksh.426 billion.

Source: Citizen TV
 
Hawa wanajielewa.


Kwa Tanzania sio rahisi hivyo

Katiba katiba katiba yetu ibadilishwe haraka!
 
Back
Top Bottom