Kenya, EU kukamilisha makubaliano ya Biashara ya kuondoa Ushuru kwenye bidhaa za Kenya

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,280
Kenya na Umoja wa Ulaya zimesaini rasmi mkataba wa kibiashara utakaoruhusu taifa hilo la Afrika Mashariki kusafirisha bidhaa bila ushuru katika soko la Umoja wa Ulaya.

"Makubaliano yanaanzisha ukurasa mpya ambapo bidhaa za Kenya zitaruhusiwa kuingia soko la Ulaya mara moja kutozwa ushuru na bila kiwango cha ukomo," Waziri wa Biashara wa Kenya Rebecca Miano alisema kabla ya kutia saini mkataba wa kibiashara katika hafla iliyofanyika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, Jumatatu.

"Baada ya muda, bidhaa za Ulaya pia zitapata fursa ya upendeleo katika soko la Kenya," aliongeza.

Baraza la Umoja wa Ulaya liliidhinisha makubaliano hayo ya kibiashara wiki iliyopita, lakini bado yanahitaji kuidhinishwa na bunge la Kenya na Bunge la Ulaya kabla ya kuanza kutumika.

"Kiini cha mpango huu ni kuweka pesa halisi katika mifuko ya watu wa kawaida," Rais wa Kenya William Ruto alisema katika hafla ya kutia saini.

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen, ambaye pia alihudhuria tukio hilo, aliuita ushirikiano huo "hali ya ushindi wa pande mbili."

Mkataba huo unakuja wakati Brussels ikitafuta uhusiano thabiti wa kiuchumi na Afrika ili kukabiliana na ushawishi wa China, huku ikihimiza ahadi za maendeleo kati ya EU na Kenya katika maeneo ikiwa ni pamoja na ulinzi wa mazingira na haki za wafanyikazi.

Mauzo ya nje bila ushuru na bila ukomo.

Makubaliano ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya EU-Kenya (EPA), ambayo yalikamilishwa Juni 2023, yanahakikisha uingizwaji bila ushuru na bila ukomo wa bidhaa zinazotoka nchini Kenya katika jumuiya hiyo yenye nchi wanachama 27, ukiacha silaha.

Umoja wa Ulaya ndiyo soko muhimu zaidi la mauzo ya nje na mshirika wa pili kwa ukubwa wa kibishara.

Mwaka 2022, Kenya ilisafirisha bidhaa za thamani ya euro bilioni 1.2, hasa za kilimo katika Umoja wa Ulaya, ikiwemo chai, kahawa, maua, njegere na maharage. Zaidi ya theluthi mbili, au asilimia 70 ya uzalishaji wa maua ya Kenya yanauzwa katika soko la Umoja wa Ulaya.

Kwa upande wa Kenya, yenye uchumi mkubwa zaidi wa Afrika Mashariki, itafungua hatua kwa hatua soko lake kwa bidhaa za Ulaya, huku makubaliano yakishuhudia ushuru ukipunguzwa katika kipindi cha miaka 25. Kwa sasa, Kenya inaagiza hasa mashine na bidhaa za madini na kemikali kutoka EU.
 
Ulaya wamesaini mkataba kama umoja wa ulaya..sisi imesaini Kenya na sio umoja wa africa(AU)..hapa ndio tatizo la africa linapoanzia..kut
 
Back
Top Bottom