Inaumiza sana Mtoto wa Masikini anapokosa Mkopo wa Elimu ya Juu

JF Member

JF-Expert Member
Dec 14, 2014
7,418
9,703
Nimefuatilia kwa ukaribu sana hili suara la board ya Mikopo. Ni kama serikali imeendelea kulifumbia macho, yaani haioni kitu kabisa.

Bungeni nako wameamua wanafunzi wapokelewe vyuoni bila kuwa na mikopo. Hapa ni danganya toto, vyuo vitajiendeshaje ? Wanafunzi wataishije huko vyuoni?

Serikali inaendesha matamasha kila siku na mengine inaweza ikafanya kwa njia ya media tu na ujumbe ukafika.

Mfano - Unatumia Billion 7 kutanganza matokeo ya sensa.. hapa ni zaidi ya wanafunzi 3,000 wangepata mkopo.

Unatumia pesa nyingi kujadili kwa nini watu wanatumia mikaa badala ya gesi na unalipa mamilion ya pesa ambayo yangeenda kwa wanafunzi.

Unasafiri nje ya nchi kila kukicha, safari zingine hazina hata ulazima, hizi pesa pelekeni kwa wanafunzi.

Hii nchi inajiendesha tu wala haina watu wenye maini sahihi.

Serikali punguzeni matumizi, mambo mengine fanyeni kwa mitandao sio kila siku watu wasafiri na kula na kulala..Unakuta kikao cha masaaa mawili mtu anasafiri toka Dar hadi Mwanza.
 
Kwani uchunguzi kuhusu kashfa ya mikopo huko loan board umebaini nini? nilishasema serikali irudie utaratibu wake wa awali wa kutoa ufadhili kwa wanafunzi waliodahiliwa kwenye vyuo vya umma pekee kupitia wizara ya elimu ili kujipunguzia mzigo.

Hii ni kwa sababu vyuo vya umma ndo vinaendeshwa kwa kodi za wananchi, na hii itafanya vijana wote wakiwemo wa wanyonge wapambanie nafasi za vyuo vya umma ili waweze kufadhiliwa na serikali. Hiyo loan board kama wanaitaka waiache ihudumie wanafunzi wa vyuo binafsi.​
 
Kwani uchunguzi kuhusu kashfa ya mikopo huko loan board umebaini nini? nilishasema serikali irudie utaratibu wake wa awali wa kutoa...​
Umeandika bila kufikiria hivyo vyuo vya serikali vitatosha kudahili wanafunzi wote nchi nzima ili wapate mkopo
 
Umeandika bila kufikiria hivyo vyuo vya serikali vitatosha kudahili wanafunzi wote nchi nzima ili wapate mkopo
Ndo maana nikasema wale ambao watadahiliwa na vyuo binafsi wanaweza kuendelea na utaratibu wa loan board na serikali inaweza kutoa fungu huko. Ila hawa walioko kwenye vyuo vya umma vinavyoendeshwa na kodi za wananchi wasiathirike kwa namna yoyote ile. Na vilevile serikali bado ina uwezo wa kuvipanua vyuo vyake na kuongeza nafasi zaidi za udahili.​
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom