GAZETI
JF-Expert Member
- Feb 24, 2011
- 5,277
- 6,673
"Sasa Imekuwaje shoga?" Anayeulizwa hajibu badala yake anatoa kilio kidogo
cha kwikwi na kufuta Machozi kwa kanga yake. Baada ya muda kidogo anatulia
na kuanza kujibu. Natega sikio, niko kando yao hapa hospitali ya Malawi. Ni
simulizi ya kusikitisha kidogo.
Jamani! vikao vya harusi vilishafanyika na michango ikatolewa lakini jamaa kenda
kuoa mwanamke tofauti na ambaye alikusudiwa kwenye michango hiyo, Mbaya
kamwacha huyu mlengwa akiwa mjazito mbaya zaidi alishamwachisha biashara
yake ambayo ilikuwa inampatia riziki (Mama Lishe). Analia........ Anafikiria kurudi
kwao Kondoa.........
Haya ni mengi na kila siku yanatokea na kama hayajakukuta ni ya kawaida sana
lakini mimi nina wazo binafsi ambalo nahitaji mchango wenu kama ni sahihi au la!
Napendekeza kuwe na mkataba maalum sasa katika mapenzi ambao utatambuliwa
kama inavyotambuliwa mikataba ya wapangaji, mashamba n.k Ndani ya huu
mkataba kuwe na mambo maalum ambayo wapenzi watakubaliana ili kama kutatokea
tatizo muhusika achukuliwe hatua za kisheria.
Haiwezekani watu wanawapa ujauzito wenzao halafu bila huruma wanawatelekeza
na hakuna hatua yoyote wanayochukuliwa.
Hivi wenzetu katika nchi zilizoendelea inakuwaje? au ni kama huku kwetu?