Inauma sana!

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,278
6,671
"Sasa Imekuwaje shoga?" Anayeulizwa hajibu badala yake anatoa kilio kidogo
cha kwikwi na kufuta Machozi kwa kanga yake. Baada ya muda kidogo anatulia
na kuanza kujibu. Natega sikio, niko kando yao hapa hospitali ya Malawi. Ni
simulizi ya kusikitisha kidogo.

Jamani! vikao vya harusi vilishafanyika na michango ikatolewa lakini jamaa kenda
kuoa mwanamke tofauti na ambaye alikusudiwa kwenye michango hiyo, Mbaya
kamwacha huyu mlengwa akiwa mjazito mbaya zaidi alishamwachisha biashara
yake ambayo ilikuwa inampatia riziki (Mama Lishe). Analia........ Anafikiria kurudi
kwao Kondoa.........

Haya ni mengi na kila siku yanatokea na kama hayajakukuta ni ya kawaida sana
lakini mimi nina wazo binafsi ambalo nahitaji mchango wenu kama ni sahihi au la!

Napendekeza kuwe na mkataba maalum sasa katika mapenzi ambao utatambuliwa
kama inavyotambuliwa mikataba ya wapangaji, mashamba n.k Ndani ya huu
mkataba kuwe na mambo maalum ambayo wapenzi watakubaliana ili kama kutatokea
tatizo muhusika achukuliwe hatua za kisheria.
Haiwezekani watu wanawapa ujauzito wenzao halafu bila huruma wanawatelekeza
na hakuna hatua yoyote wanayochukuliwa.
Hivi wenzetu katika nchi zilizoendelea inakuwaje? au ni kama huku kwetu?
 
Ushawahi kusikia bwana harusi mtarajiwa kala hela za mchango wa harusi halafu akasepa? Hii imemtokea mwafulani pale juzi kati.
 
Ushawahi kusikia bwana harusi mtarajiwa kala hela za mchango wa harusi halafu akasepa? Hii imemtokea mwafulani pale juzi kati.
Nimesikia watu wanachangiwa halafu hawaoi, tena kuna ambao washafahamika
kuwa ndio mtindo wao, Lakini hii ya kuchangiwa kwa ajili ya mwingine na kwenda
kuoa mwingine ndio kwanza.....
 
Napendekeza kuwe na mkataba maalum sasa katika mapenzi ambao utatambuliwa
kama inavyotambuliwa mikataba ya wapangaji, mashamba n.k Ndani ya huu
mkataba kuwe na mambo maalum ambayo wapenzi watakubaliana ili kama kutatokea
tatizo muhusika achukuliwe hatua za kisheria.
Haiwezekani watu wanawapa ujauzito wenzao halafu bila huruma wanawatelekeza
na hakuna hatua yoyote wanayochukuliwa.
Hivi wenzetu katika nchi zilizoendelea inakuwaje? au ni kama huku kwetu?

haya hayatekelezeki..............................ukweli unabakia kuwa ni ukweli...........................sex outside marriage is at own risk.............................kama huna subira basi ujue hujaivuta kheri......................mikataba kila siku huvunjwa na hakuna sheria ya kumlazimisha mtu kuishi na mtu asiyempenda..................mtoto hawezi kuwa ni sababu ya kubanwa mbavu na mtu ambaye humhitaji...........................
 
Dah, umeme umekatika... Nitarudi baadae maana UPS inanialert!
 
mikataba kila siku huvunjwa na hakuna sheria ya kumlazimisha mtu kuishi na mtu asiyempenda..................mtoto hawezi kuwa ni sababu ya kubanwa mbavu na mtu ambaye humhitaji...........................
Basi kuwe na sheria ya kuwabana wanaowapotezea wenzao muda, maana mtu
anakuwa na matumaini mwishowe unamwacha solemba.... Bado Inauma sana!
 
ndo maana hata dada zangu nawaambia mambo ya kuoana anakuachisha kazi/biashara wasithubutu. Na ninachoshukuru hakuna aloacha. Duniani hapa jiamini mwenyewe tu, binadamu kigeugeu
 
ndo maana hata dada zangu nawaambia mambo ya kuoana anakuachisha kazi/biashara wasithubutu. Na ninachoshukuru hakuna aloacha. Duniani hapa jiamini mwenyewe tu, binadamu kigeugeu
Tatizo kuna mijitu inapretend kuwa ina wivu sana hata
Mtu awe TRA wanataka aache tu!
 
haya hayatekelezeki..............................ukweli unabakia kuwa ni ukweli...........................sex outside marriage is at own risk.............................kama huna subira basi ujue hujaivuta kheri......................mikataba kila siku huvunjwa na hakuna sheria ya kumlazimisha mtu kuishi na mtu asiyempenda..................mtoto hawezi kuwa ni sababu ya kubanwa mbavu na mtu ambaye humhitaji...........................

Mkuu kama umeongea ukweli vile! Tena ktk hili hali inaweza kuwa mbaya zaidi ya Richard Monduli na dawahasi (dowans)
 
Back
Top Bottom