Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,397
- 3,884
Nimefuatilia trend ya huduma za internet kwa mitandao kadhaa na kusema kweli hali ni mbaya na ya kusikitisha sana.
Kwa miaka kadhaa sasa, Serikali imejaribu mbinu mbalimbali za kubana uhuru wa watu kuongea. Siku za nyuma watu walikuwa wananyakuliwa kutokana na post zao. Lakini mbinu hiyo imeonekana kutofanya kazi sana.
Ambacho naona kinafanyika sasa ni kufanya gharama za vifurushi kuwa aghali mno. Nia ni kupunguza muda ambao watu watakaa kwenye mitandao, na mategemeo yao ni kuwa itasaidia watu wasifuatilie au kuchangia mijadala ya kisiasa inayoendelea.
Bei za vifurushi zimekuwa kubwa mno. Na si kubwa kwa sababu ya bei tu ya vifurushi lakini kiasi cha data ambazo unapewa kwa kila kifurushi kimepungua mno kiasi kwamba kwa vifurushi vingi, ndani ya siku moja mtu unalazimika kununua zaidi ya mara moja hata kama una matumizi ya kawaida tu.
Huu ni ushetani na sidhani kama utaleta faida wanazozifikiria. Sana sana inapunguza fursa za watu kupata elimu na kujifunza mambo ya msingi mitandaoni, kufanya biashara mtandao na hata kubadilishana mawazo na watu mbalimbali duniani ambayo mwisho wa siku yatasaidia kujenga nchi.
Wakiona wameshindwa huko kote watasema mtu haruhusiwi kununua zaidi ya kiwango fulani cha data kwa siku bila kibali maalumu! Tunapokwenda, ukiwa mnunuaji mkubwa wa bundle za internet unaweza kuwa suspect wa ugaidi!