WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 956
Kuna mada zimefanya nianzishe thread hii.... kuna mtu anaomba ushauri ati yeye na mdogo wake wanapendwa na mwanaume mmoja na wamekuwa wakimlia buku kumi kumi za vocha..... inaonekana hawawezi kuachia hizo buku kumi ndio maana wamemganda kama luba ..wakiomba ushauri wa kinafiki.
Ili basi kukwepa hali kama hizi .....
Itapendeza kama mtu humpendi ukaacha kupenda kila kitu chake ikiwemo pesa....
Itapendeza zaidi kama wewe mdada ukawa na akili ya kujitegemea zaidi kuliko kutegemea vya kupewa...
Itapendeza wewe mkaka kama utaacha kutoa fedha na vitu vingine kama chambo cha kuvuta unaemtaka... hadi utakapohakikisha kuwa the feeling is mutual...
Itapendeza sana kama wadada wataacha kujibwetesha na kuhangaika kutafuta badala ya kuwanyonya akina kaka kuanzia vocha, lunch, kinywaji, vivazi.....
endelezeni wana JF...