Inakuwaje mtu anatoa posa then anapangiwa mahali halafu anapotelea mitini? (Haoi)

Wanaume tuweni serious tusicheze na hisia za wachumba zetu, nashangaa kuona mtu anatoa mpaka posa anapangiwa mahali halafu anamkimbia bint hamuoi anaenda kuoa mwanamke mwingine, sijui tatizo huwa ni nini.
Unapangiwa mahari ambayo ni ya kikatili, utadhani wewe ndio unae taka wakati ni matakwa ya wote yaani kijana na binti mwenyewe, ifike mahala mahari itakayo tajwa igawanywe kwa mbili!
 
Sababu inaweza kuwa mahari ni kubwa sana au baada ya barua mchumba kakengeuka mfano kamfumania, bwana amegundua ana tabia mbaya mfano kudanga, ulevi, uchoyo, uchawi, ugomvi. Pia labda bwana kapata mchumba bora zaidi au hata karogwa na dem mwingine, mambo ni mengi mda mchache.
Yawezekana kabisa
 
Ipo posa tulimpeleka mshkaji flani 2 yrs ago, ke alikuwa rubani, tulipokelewa vizuri kufikia mahari jamaa akapigwa bill ya 100M , ndio hujakosea ulichosoma millioni mia moja ,alipotoka pale alienda moja kwa moja mazima hajarudi hadi leo.

Tunavoongea ameoa bank teller wa CRDB mahari alitoa millioni tano tena alitaka yy,hawakumpangia bei ,

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
Duh aisee
 
Mtu hawezi ghaili bila sababu,unakuta vikwazo toka kwa mwanamke au familia ndio sababu...ilitokea jamaa wamekaa kwenye uchumba na binti 3yrs,binti anakaribia kumaliza masomo akamwambia jamaa katoe mahali,jamaa akaenda na mshanga na wazaz kutoa mahali,..familia ikasema mila yetu mahali tutachukua siku ya harusi,..jamaa kajipanga kwa harusi miezi 3 binti kagoma kuolewa mpk afanye kazi mwaka 1 ndio wafunge ndoa,jamaa akaamua kuachana nae...baada ya muda binti na wazazi wanamtafuta jamaa,..binti akachanganyikiwa kwamba jamaa kamuaibisha...nani anakosa hapo?
Huyo bint na wazazi wake ni vichaa
 
Back
Top Bottom