Inakuja siku ambayo Uhalali wa Mtu kukubaliwa kisiasa itakuwa kama aliwahi kusimama kuitetea Chadema au Viongozi wake

Inakuja siku ambayo Uhalali wa Mtu kukubaliwa kisiasa itakuwa kama aliwahi kusimama kuitetea Chadema au Viongozi wake

Lord Denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
23,494
Reaction score
57,869
Hakuna kidumucho milele

Huu ni ukweli mchungu na mzito ambao inawezekana kuna binadamu wengi hawapendi kuusikia.

Huko nyuma ziliwahi tokea tawala za Kirumi, Ottoman, Persia, Nazi na nyinginezo nyingi.

Yamewahi kuiongoza dunia hasa kijeshi au kibiashara mataifa ya Uingereza, Italia, Hispania na hata Uholanzi.

Vimewahi kutawala Dunia vyama vya kisiasa na hata Madikteta waliojiona kuwa wao ni miungu watu. Hata hivyo walikuja kuanguka na tawala zao kufikia mwisho.

Tanzania ni sehemu ya Dunia. Haipo mbali na historia ya dunia na kamwe haiwezi kuwa exceptional na historia ya dunia.

Kuna watu wanaona raha leo kuwatesa Chadema, kuwanyanyasa Chadema, kuwaua na kuwafunga Magerezani makada na wafuasi wa Chadema.

Kuna wengine leo wanaona Chadema inavyoteswa ni vizuri wao wakikaa kimya. Hawaoni umuhimu wa hata kuwatetea kwa kuongea chochote.

Pamoja na yote haya leo napenda kusema hili. Ipo siku na itakuja siku ambayo uhalali wa mtu yeyote kisiasa au kuchukuliwa anastahili kuishi kwa amani nchini Tanzania utapimwa kwa namna kama aliwahi hata kusema kitu kuwatetea Chadema katika madhira waliyopitishwa na CCM na watu wao.

Bookmark this thread.

Lord denning.

FB_IMG_1750064496561.jpg
 
Back
Top Bottom