Inakuaje radio frequency zitofautiane?

Inakuaje radio frequency zitofautiane?

Mi nadhani kuna undani wa hizi frequencies kitaaluma kuliko tunavyofikiri hadi ajitokeze mjuzi zaidi atuelimishe.
Dunia nzima angani kuna mawimbi mengi mno tungekuwa na uwezo wa kuyaona tungehisi hatuwezi kupita.
Kuna frequency za radio, television,majeshi,mambo ya usafiri wa ndege,usafiri wa majini,radio call,mbuga za wanyama,usafiri wa anga za juu.
Wote hawa hawaingiliani labda kwa bahati mbaya mno nahisi kuna makubaliano ya kimataifa na kitaifa na ndio kuna chombo TCRA huku kwetu.Wajuzi watuelimishe.
 
Kwahiyo kila mkoa radio station inawabidi wafunge mnara au wanashare mnara mmoja!?.
Kama wanashare mnara inakuaje nyingine hazisikiki kwingine?.
Kama hawashei inakuaje kusave gharama ya kufunga minara 26 (mikoa ya Tz) radio station isitafute kifaa chenye uwezo wa kuamplify mawimbi mikoa 26.
Mkuu wana share minara ila sasa mpaka radio husika iwe imejitanua na iweze kulipa cost za sharing and broadcasting halfu mkuu ikifungwa transmitter ya kurusha mawimbi tz nzima haiwezekani na pia sio salama kwa afya na kwanza kwa structure ya dunia ilivo curved kuna sehemu hizo waves zitakuwa blocked ivo lazima kuwe na minara mingi mingi kwa ajili ya connection leo upo dar ukipiga simu usifikiri simu yako iko routed direct to Arusha hapana inapita kwenye minara mingi mingi na kwenye repeaters kuongeza ufanisi
 
ok, so bado kuna redio wanatumia AM mpaka miaka hii?
Naamini bado zipo.. Station kama Radio one, Radio free Africa, KBC wanaendelea kupatikana masafa ya kati..
Ila kama alivyosema kiongozi hapo juu, kuwa haya Masafa yaanaathiriwa sana na kelele za magari, viwanda, na mawimbi mengine kama simu, upepo that So.
Hvyo kwa nyakati kama hizi za science na technology vitu kama hvyo vinakuwa haviepukiki, hvyo hupelekea masafa hayo kuonekana si rafiki.
 
Mr Easy CHAZA na Idimi je kwanini Hakuna frequency moja kwa radio station moja Tanzania nzima?..
Miaka ya 90 RTD ilikua inapatikana Short Wave(SW) nchi nzima. Hata hivyo,kama ilivyo kwa Medium Wave(MW) au Amplitude Modulation(AM) kwani AM na MW zinafanana, ShortWave ilihitaji mitambo yenye nguvu,hivyo usikivu ulikua na changamoto,RTB ikaamua kufunga mitambo ya AM/MW kwenye kanda ili kuongeza usikivu. Kwa wale wanaokumbuka wakati wa Redio Philips zile za mbao,watakumbuka RTD ilikua ikipatikana Short Wave nchi nzima kwa Meter Band zaidi ya moja,unachagua ipi ina nafuu kutegemea na mkoa uliopo.

Mdau unatakiwa kesho au siku yoyote weka idhaa ya Kiswahili ya Radio Deustche Welle(DW) hata kwa kupitia radio zake washirika kama Redio Tumaini,RFA,Aboud hasa saa saba mchana. Wakati wanapofunga matangazo yao DW saa8 mchana wanakutajia Meter Band mbalimbali,nyingi ya hizo ni za Shortwave,so mtu unachagua uitakayo au utakayoipata. Hicho utakachokisia,ndicho ambacho zamani RTD ilitumia hizo Meter Band, ilikua free kwa popote ulipo. Was very powerful than FM,but with limitation ya mchemko mkubwa tofauti na FM ambayo haina makelele.
 
ok, so bado kuna redio wanatumia AM mpaka miaka hii?
Nyingi tu,mifano ni ZBC,TBC,Radio One,RFA,KBC. Ila kwa mijini,kelele zinakua nyingi sana. Lakini ukienda Vijijini tune tu AM,utazipata KBC,ZBC,RTD,RFA na Radio One Stereo.
 
Frequency kutokana na availability ya hio station ktk mkoa husika ww leo ukitaka kuanziasha radio basi utatafuta Frequency ambayo iko Empty haina mtu n
Frequency ya chini kabisa inaanzia ngapi na na ya juu kabisa ina ishia ngapi
 
Kwa walio mbeya kuna redio inaitwa ushind fm 98.6 nazan sasa hii frequency inaingiliana na ledio moja ipo malawi inaitwa two fm ni 98.7 ile inanguvu sana kwa wanaoish masukulu hawapat matangazo ya ushind fm labda ile ya malawi isiwe hewan ikilud tu hewan ya uku tz ndo bas tena
 
Back
Top Bottom