Poleni jamani. Huyo Lowassa na viongozi wengine wa ccm ndio waliolifikisha taifa letu hapa. Wao ndio mainjinia wa mikataba mibovu, siasa za majitaka, watu wenye kupenda majungu na kutumia madaraka vibaya. Leo hii wamebaki kulipa waandishi na vijana ili wawapigie debe kubaki/kurudi madarakani wakati tunawajua ndio tatizo halisi la nchi hii. Hao wameishiwa mbinu wamebaki kutegemea dola na uwezo wao wa kujenga hoja ni mdogo. Na kama ameshalitumikia taifa sasa ni wakati wake kukaa pembeni ili watanzania wengine waonyeshe uwezo wao na yeye apate kujifunza yapi yalikuwa ni mazuri yake na yapi yalikuwa madhaifu yake. Hebu tuambie kama yeye ni kiongozi bora ni mchago gani ameutoa kwenye katiba pendekezwa, zaidi ya kuwa ni mmoja wa wajumbe waliolazimisha maadili ya uongozi yaondolewe?
Kwa hiyo ndugu naomba nichukue nafasi hii kukuomba kama anakulipa hela uumpigie debe acha kumtia hasara hizo hela zake akazitumie kwenye uzee wake. Kumbuka huyo Lowassa amechafuka na mkataba unaotugharimu watz mpaka sasa ni huo wa umeme. Nadhani wewe ni shahidi wa gharama za umeme tunazolipa zilivyo juu. Na kwabahati mbaya hajawahi kusema ukweli kuhusu mkataba huo. Leo hii mtu ambaye uadilifu wake ni wakutiliwa shaka na watz wengi mnatuletea sifa za kijinga na historia zisizo na maana katika maisha yetu. Kumbukeni watz tunavidonda vya ugumu wa maisha vilivyosababishwa na hao akina Lowassa. Huu si wakati wa kuwapa nchi watu ambao uwajibikaji na uaminifu wao ni wa kutiliwa mashaka na hasa ukizingatia wamepitisha katiba pendekezwa ambayo itaendelea kuwafanya wafanye watakalo katika nchi hii kama viongozi.