Impala Hotel, Leopard Tours Offices kuvunjwa

Impala Hotel, Leopard Tours Offices kuvunjwa

Hiyo shule lazima haina hati sababu Majengo ya Serikali yalikuwa hayana hati miliki(Kulingana na hotuba ya Rais akiongea na wafanyabiashara) ndio wana-process sasa.

Hilo la hati si tatizo . kama palipimwa na kuna ramani ....na mawe yapo lazima aachie tu.
 
Unaweza kutufafanulia ni kwa nini hatua hazikuchukuliwa tangia hiyo 2013 Mh. Diwani?
Cc. Nanyaro Ephata

hatua zimechukuliwa kwa wamiliki kupewa notisi ya kuvunja (hapa ni kwa wale waliojenga,Mezaluna,kijenge supermarket,Bushbuck,exim bank,na Leopard).Hii ni buffer zone lazima ibaki kuwa wazi!.Pia walitakiwa kulipa kwa wale wanaotumia kwa matumizi ya maegesho tu,jambo ambalo linafanyika.
Impala hotel haipo kwenye huu mkumbo
 
Habari za mida hii wandugu?

Katika kile kinachoonekana kuendana na kasi ya Rais wa awamu ya tano ndugu JPM, Manispaa ya jiji la Arusha imeanza operesheni ya kurudisha maeneo ya serikali yaliyohodhiwa na watu binafsi kinyume na sheria kwa kuandikia barua uongozi wa Hoteli maarufu jijini Arusha pamoja na Kampuni ya Leopards Tours Safaris kwa kuingia kwa kiasi fulani eneo lililokuwa la shule ya msingi ya serikali.

Najaribu kuambatanisha barua hiyo katika jukwaa hili.

Leopard Tours si ya Lowasa? Au nimekosea?
 
Sio Mchina aliahamishia kwa Father..... Father na watu wake waliona lile eneo ni potential hivyo wakajenga mazingira ya kumsumbua mchina ili akimbie na wao wakachukua. Sasa ngoma imegeuka. Acha livunjwe. Dawa ya dhuluma mwisho wake ni huo.

Nakumbuka sana lakini mchina alipoanza kufuatwa fuatwa kaamua kuhamishia msala kwa Fadhal.
 
Watoa vibali ni wapiga shekels si zaidi ya hapo, hao wanataka vibali wanaenda pale wakiwa na fedha zao so lolote wanataka wafanyiwe.
Mwisho wa siku ndiyo hao hao ambao magufuli alisema wanafoji hizo hati zionekane za kale!. Isanga family
 
Last edited by a moderator:
Hao ambao wako more equal than others ni wanyama gani na ni kwa nini wawe more equal...????
The big guns in politics and government administration, the rich guys are more equal than the hoi-sleepers!
 
View attachment 312334 View attachment 312335
Habari za mida hii wandugu?

Katika kile kinachoonekana kuendana na kasi ya Rais wa awamu ya tano ndugu JPM, Manispaa ya jiji la Arusha imeanza operesheni ya kurudisha maeneo ya serikali yaliyohodhiwa na watu binafsi kinyume na sheria kwa kuandikia barua uongozi wa Hoteli maarufu jijini Arusha pamoja na Kampuni ya Leopards Tours Safaris kwa kuingia kwa kiasi fulani eneo lililokuwa la shule ya msingi ya serikali.

Najaribu kuambatanisha barua hiyo katika jukwaa hili.


Tunataka fidia pia kwa hicho kipande cha ardhi kilichotumika na hiyo hotel kwa miaka hiyo yote, kubomoa pekee hakutoshi,
 
Kubomoa haya majengo ni kutokufikria kwa kina.
Kama eneo ni la shule, serikali itaifishe hayo majengo ili yawe madarasa na ofisi za shule. Over
 
Kubomoa haya majengo ni kutokufikria kwa kina.
Kama eneo ni la shule, serikali itaifishe hayo majengo ili yawe madarasa na ofisi za shule. Over
Wazo zuri,tatizo utekelezaji.
 
Tatizo ni kwamba hizi Hotel zitavunjwa tuu...

No way out!
 
Kama tunataka maendeleo kwa nin tusipime maeneo mapya tuweke mipango mizuri ya ardhi mbona tanzania kubwa sana, sehemu zilizokosewa tuachane nazo tufocus kwenye miji mipya kuwabomolea watu ni kurudisha watu nyuma na kuutafuta umasikin kwa nguvu. Kikwete aliwahi kusema Dar kuna foleni lkni hawez kubomoa majengo ili bara bara ipite, unless kama sababu ni nyingine lkn kwa kwel kubomoa hayo majengo ni kukosa busara.
 
Back
Top Bottom