Impala Hotel, Leopard Tours Offices kuvunjwa

DaveSave

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
440
637
impala.jpg
leopard.jpg

Habari za mida hii wandugu?

Katika kile kinachoonekana kuendana na kasi ya Rais wa awamu ya tano ndugu JPM, Manispaa ya jiji la Arusha imeanza operesheni ya kurudisha maeneo ya serikali yaliyohodhiwa na watu binafsi kinyume na sheria kwa kuandikia barua uongozi wa Hoteli maarufu jijini Arusha pamoja na Kampuni ya Leopards Tours Safaris kwa kuingia kwa kiasi fulani eneo lililokuwa la shule ya msingi ya serikali.

Najaribu kuambatanisha barua hiyo katika jukwaa hili.
 
Last edited by a moderator:
Kama serikali inatoa vibali watu wanajenga kuna haja gani kuwafata hao hao tena kuchukua vibali maana wanaendelea kutoa vibali watu wanajenga harafu hao tena wanakuja kuvunja...
 
pale ni karibu na shule kabisa asiyejua lazima abishe. mafisadi ni hatari.
 
Impala hotel hii ni ya lowasa,

Revenge at work,
Hamna lolote,
 
Nadhani kwa sababu ilikuwa ni enzi za Mkapa hivyo mamlaka tofauti ndio ilitoa kibali.Na unavyoelewa katika Nchi za ki-Afrika kujuana(nepotism) ni kwingi.This is Magufuli era,some will win while others will loose too.
 
Leopard kuna mjengo bado haujamalizika lile eneo lote mali ya shule ya msingi Kijenge.Kama mimi serekali mwakani wanafunzi wote wa darasa la kwanza wanaingia mjengoni bila chenga.
 
Rweye....siyo swala la mimi kuridhika...bali msumeno ukate mbele na nyuma.Je itawezekana au tufanye subira.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom