SI KWELI IMF Withdraws Statement on $443.9 Million Disbursement to Tanzania

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
The International Monetary Fund (IMF) has retracted a previous statement claiming that Special Drawing Rights (SDRs) amounting to $443.9 million had been allocated to Tanzania. The communication, originally said to be dated July 10, was officially withdrawn by the IMF.

Officials confirmed there are currently no plans for an alternative announcement regarding this disbursement or any new allocation for Tanzania.

This development comes amid global scrutiny over financial disbursements to developing nations, as the IMF aims to maintain transparency and accountability in its fiscal operations.

Source: Devdiscourse

For Swahili viewers.

IMF yaondoa taarifa kuhusu mkopo wa dola milioni 443.9 kwa Tanzania.

Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limebatilisha taarifa ya awali iliyodai kwamba "Special Drawing Rights"(SDRs) zenye thamani ya dola milioni 443.9 zilikuwa zimetengwa kwa Tanzania.

Mawasiliano hayo, ambayo awali yalisemekana kuwa ya tarehe 10 Julai, yaliondolewa rasmi na IMF.

Maafisa walithibitisha kuwa kwa sasa hakuna mipango ya tangazo mbadala kuhusu utoaji huu au mgao wowote mpya kwa Tanzania.

Hali hii inakuja huku kukiwa na uchunguzi wa kimataifa kuhusu utoaji wa fedha kwa mataifa yanayoendelea, kwani IMF inalenga kudumisha uwazi na uwajibikaji katika shughuli zake za fedha.
 
Tunachokijua
Madai

Kumekuwapo na picha ya makala inayosambaa mtandaoni ikidai kuwa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limeondoa taarifa yake kuhusu kuidhinisha ufadhili wa Dola za Marekani milioni 443.9 kwa Tanzania na kwamba hakutakuwa na taarifa nyingine itakayotolewa.

Je, ni upi uhalisia?

Picha hiyo ina taarifa zinazopotosha. Hakuna ushahidi wa IMF kufuta au kubatilisha uamuzi wa kuidhinisha fedha hizo kwa Tanzania.

Tarehe 10 Julai 2026, Bodi ya Wakurugenzi ya IMF ilikamilisha mapitio ya programu za Tanzania chini ya mpango wa Extended Credit Facility (ECF) na Resilience and Sustainability Facility (RSF) na kuidhinisha kutolewa kwa fedha hizo.

Uamuzi huo uliwezesha Tanzania kupata takribani Dola za Marekani milioni 443.9, zikiwa ni takribani Dola milioni 154.1 chini ya ECF na Dola milioni 289.7 chini ya RSF. Taarifa rasmi ya IMF kuhusu uamuzi huo bado inapatikana kwenye vyanzo rasmi vya taasisi hiyo. Hakuna taarifa rasmi kutoka IMF inayoonesha kuwa uamuzi huo umefutwa au kubatilishwa.

Aidha picha inayodaiwa kuwa makala ya habari ina viashiria vya kutengenezwa:

Picha iliyotumika katika makala hiyo ina dalili za kutengenezwa kwa kutumia Akili unde (AI), ikiwemo makosa ya tahajia kwenye maandishi kama “INTERNATIOAL MONAARY FUW” na “REFARM”. Kichwa cha habari kinachodai IMF imeondoa taarifa hiyo hakina ushahidi wa moja kwa moja kutoka IMF wala hakijaambatanishwa na tamko rasmi la taasisi hiyo.

Hakuna kiungo au nukuu kutoka kwa maafisa wa IMF kuthibitisha madai kuwa taarifa hiyo imeondolewa kwa sababu uamuzi wa fedha hizo umebatilishwa.

Hivyo madai kwamba IMF imeondoa taarifa ya kuidhinisha ufadhili wa Dola za Marekani milioni 443.9 kwa Tanzania hayajathibitishwa. Taarifa rasmi ya IMF kuhusu idhini hiyo bado ipo, na hakuna ushahidi unaoonyesha kuwa fedha hizo zimefutwa au kusitishwa.​
The International Monetary Fund (IMF) has retracted a previous statement claiming that Special Drawing Rights (SDRs) amounting to $443.9 million had been allocated to Tanzania. The communication, originally said to be dated July 10, was officially withdrawn by the IMF.

Officials confirmed there are currently no plans for an alternative announcement regarding this disbursement or any new allocation for Tanzania.

This development comes amid global scrutiny over financial disbursements to developing nations, as the IMF aims to maintain transparency and accountability in its fiscal operations.
ok.🐒
 
Haya bwana...Nakumbuka zile mbwembwe za JPM alifunga nchi, na tunaupiga mwingi. Sio tu kwamba tunaupiga mwingi, sasa tunaupiga mwingi na kuutanua.

Ni kujidanganya tunapofikiri tunawexza kufanya jambo lolote, hata kama ni dhuluma, jinai na dhambi, bila kupata madhara yoyote, hapa duniani na baadae mbele ya kiti cha haki.

Kila chenye mwanzo hakikosi kuwa na mwisho.........
 
The International Monetary Fund (IMF) has retracted a previous statement claiming that Special Drawing Rights (SDRs) amounting to $443.9 million had been allocated to Tanzania. The communication, originally said to be dated July 10, was officially withdrawn by the IMF.

Officials confirmed there are currently no plans for an alternative announcement regarding this disbursement or any new allocation for Tanzania.

This development comes amid global scrutiny over financial disbursements to developing nations, as the IMF aims to maintain transparency and accountability in its fiscal operations.
Basi hizi ndizo habari mnazozipenda, mwazitafuta sana na kuzishabikia sana huko CHADEMA as if mnamkomesha Samia na misaada hiyo itakuja kwenu
 
Mimi nawaomba Wazungu na wafadhili wetu wote waacha kiherehere Cha kutukopesha na kutupatia misaada

Tuna nchi iliyopata uhuru miaka zaidi ya 60 sasa

Tatajitegemea lini?

Na tunaposhindwa kujitegemea ilihali tumezungukwa na rasilimali Kila pahala, Shida ni kuwa, viongozi wetu ni empty

Watupishe
 
Back
Top Bottom