Ndugu Zangu,
Hii ni nchi yetu. Tunayaandika haya kwa mapenzi ya nchi yetu. Yanayotokea Loliondo yanaanza kubeba sura ya kashfa. Taratibu, Loliondo inaonekana kuwa ni aibu ya kitaifa kwenye masuala ya kimsingi ya afya ya watu wake.
Si kawaida, na yawezekana ni mara ya kwanza kutokea, kwa blogu ya jamii kutoa msimamo juu ya jambo la kitaifa. Tunauona umuhimu huo, tunafanya hivyo. Ndio, Hali ni mbaya Loliondo. Kuna Watanzania wenzetu wanakufa kila siku. Wanakufa wakiwa kwenye foleni ya kupata kikombe cha Babu au baada ya kunywa kikombe hicho na kuacha kutumia dawa zao walizokuwa wakitumia kabla.
Asubuhi hii nimepokea simu kutoka Dodoma. Kuna mganga aliyenielezea hali mbaya zinazowapata wagonjwa wake wa kisukari mara baada ya kupata tiba ya Babu na kuacha kutumia dawa zao. Anasema ni mbaya zaidi kwa wagonjwa wa kisukari, maana, kisukari kinapanda haraka. Anasema kuna wagonjwa waliokufa baada ya kuacha kutumia dawa zao.
Baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa mstari wa mbele katika kupigia debe tiba ya Babu bila kufanya uchunguzi yakinifu. Ndio, duniani kuna fikra dhanifu na fikra yakinifu. Ya Babu wa Loliondo ni dhania iliyopaswa kuhojiwa kabla ya kupigiwa debe.
Hivi, wanahabari wetu wanashindwaje mpaka hii leo, kuwahoji madaktari bingwa kwenye maradhi kama UKIMWI, kisukari, na mengineyo. Madaktari hawa wako Agha Khan, wako Bugando, Mount Meru na kwengineko. Hivi, Watanzania wenzetu hawa, katika kazi zao, mpaka hii leo hawana cha kusema, cha kitaalam juu ya Tiba ya Babu? Au media imechagua kuficha ukweli?
Tunajua, kuwa habari za Babu wa Loliondo zinauza magazeti kwa sasa. Lakini, ni dhambi na kutoitendea haki nchi yetu kama tutaamua kufanya biashara na afya za watu wetu. Ni laana kubwa.
Ona sasa, Watanzania kwa maelfu wanakwenda gizani bila kuhoji, au kusaidiwa kuhoji. Katika dunia ya sasa ya Sayansi na Teknolojia hatuwezi kwenda mbele kwa kuendekeza Abrakadabra kama hizi za Loliondo.
Huu ni wakati, kwa Wizara na waziri mwenye dhamana, kutoa tamko rasmi juu ya ukweli kuhusu tiba hiyo ya Babu. Na kama Babu ataruhusiwa aendelee na tiba yake kwa wenye imani, basi, Babu huyu asaidiwe kuhamishia shughuli zake Arusha mjini. Lifanyike hilo ili tunusuru maisha ya Watanzania wenzetu walio katika hatari ya kupata maradhi mapya katika mazingira ya sasa ya Loliondo.
Tunayasema haya kwa mapenzi ya nchi yetu, basi.
Maggid,
Iringa,
Ijumaa, Machi, 25,2011
MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo
Chini hapa ni bahadhi ya maoni ya wadau;
Mdau wa kwanza:
Hapa Arusha KILA HOSPITALI IMEPOKEA WATU WA MAGONJWA YA PRESHA, KISUKARI, PUMU, N.K. AMBAO WALIKWENDA LOLIONDO "KUTIBIWA" MARADHI HAYO NA BAADA YA KUPATA "NAFUU" (PSYCHOLOGICAL) KWA KAMA WIKI MBILI TU WAMEANZA KUUMWA SERIOUSLY NA KURUDIA DAWA ZAO ZA HOSPITALI TENA.
Pili, mimi nikiwa mfanyakazi wa maabara ya hospitali ya MT Meru, sijaona hata mgonjwa mmoja wa ukimwi aliyepata "seroconversion" yaani kurudi "seronegative from serpositive status". Kinachosikitisha ni kuwa kuna watu hawataki kabisa kusikia yanayosemwa na madaktari na wafanyakazi wa hospitali mbalimbali hapa Arusha ambao kila siku tuna-deal na watu wanaozidiwa baada ya kwenda Loliondo.
Mbaya zaidi kuna magazeti, tv na redio hayataki kabisa kusikia ukweli wa majanga yaliyowafika watu waliokwenda huko. Ajabu pia ni kuwa kuna watu ambao ukitaka kuwaeleza ukweli wanakuona wewe ni mpagani usiyemwamini Mungu. Naomba waandishi wa habari wawe proactive katika kutafuta ukweli na si kutegemea mass hysteria iliyowakumba maelfu ya watu wanaotafuta miujiza kwa nguvu."
Mdau wa pili:
Kuna madaktari wengi wa hospitali mbalimbali hapa Arusha (k.m. St. Thomas, Mount Meru, n.k.) ambao wametoa onyo kuwatahadharisha wananchi waliokwenda Loliondo wasiwache dawa zao za kisukari na BP. Inaelekea kuwa, kwa sababu zisizojulikana, vyombo vya habari vya Tanzania vimesusia kuchapisha au kurusha tahadhari za madaktari hao. Juzi kituo cha TV NTV ya Kenya imewaonyesha madaktari mbalimbali wa Arusha wakitoa tahadhari hiyo.
Ikiwa madaktari na wafanyakazi wa maabara [medical laboratory technicians] wanaona watu wanakufa kila siku kwa maradhi yaliyowapeleka Loliondo ni wajibu wao waseme ukweli huo. Ni mtu mjinga ndiye anayeweza kusema kutoa tahadhari hizo ni udini. Si udini. Udini ni kutaka watu waamini miujiza ambayo inakwenda kinyume na ushahidi wa kisayansi na hali halisi. Nimeamini kuwa matatizo ya dunia ya tatu ni mengi mno, lakini matatizo kuu ni kutokujua na kutotaka watu waseme ukweli.
Mdau wa tatu:
Mjengwa mimi pia niko Arusha na ni kweli kuwa kila daktari ninayeongea naye anasema kuwa wagonjwa wengi waliokwenda Loliondo imebidi warudie dawa zao na wengine wamefariki dunia. Nina hakika kuwa Wizara ya Afya ina taarifa hizo lakini nadhani Wizara hiyo haiwezi kusema lolote kwa kuwa wanaogopa kuambiwa kuwa wao ni wadini.
Tumefikia hali ambapo madaktari wengi (hasa Wakatoliki, Wasabato, Waislamu, Waanglikana, nk) wanaogopa kujitokeza hadharani na kusema kuwa watu wanakufa BAADA ya kwenda Loliondo simply kwa kuwa wanaogopa kuambiwa kuwa wao ni wadini.
Juzi, daktari mmoja wa hospitali ya AICC hapa Arusha aliniambia kitu kilichonistusha sana. Alisema "Maafa ya tiba ya babu yataanza kuonekana kikamilifu baada ya mwezi moja". Sasa ikiwa watu wameanza kufa tangu Januari (kumbuka watu wa Arusha walianza kwenda Loliondo September 2010) hapa Arusha na Moshi na wengine wanaendelea kufa kila siku porini Loliondo mnataka watu wasiseme na wakisema mnawaita wadini, why? Hiyo ni moral blackmail.