Imenisikitisha sana hii...

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931

Tunawafundisha nini watoto wetu Bandugu?. Ni mzazi wa Kitanzania, anatundika picha ya mwanae hewani hivi ili walimwengu waone jinsi aleavyo mwanae.

Huyu mtoto hajui afanyalo na akikua kwa maadili haya, mzazi atakuwa na haki ya kumkea mtoto kama huyu?.Hivi ile Sheria ya Watoto (The Children Act, 2009 http://www.africa.gnrc.net/mm/file/positionpapergnrc.pdf) ina maana yeyote kwa Watanzania kama ilivyo kwa wenzetu Ulaya na Marekani ? Tokea imetingwa mwaka Jana 2009, sijapata kusikia makali yake hata kidogo japo ilisemekana itazuia mambo kama haya ikiwemo kupiga vita tabia za wazazi kuwatuma watoto baa au kuingia nao Baa na kumbi za starehe .
 
This is abusing the future generation. The parent or whoever is so stupid for letting the kid consume alcohol
 
Ukisikia wazazi bomu ndiyo hawa...ila kuna sheria mpya kuhusu watoto imetungwa hivi karibuni na mzazi huyu anaweza kuchukuliwa hatua za kisheria kwa malezi mabovu yanayoweza kuleta athari za makuzi ya mtoto...sina shaka na hilo hapo ni moja wapo.
 
Ngoshwe,
Usisikitike sana. Watoto wangu walipokuwa wadogo walikuwa wakipenda kuonja Heineken yangu. Niliwaachia kwa sababu bia pia ina protein.
Lakini ukubwani wote hawajageuka kuwa walevi. Wananiangalia tu nikibighua bia zangu na mwingine ananiuliza " Dad why do you like beer so much?
 
Mkuu, yawezekana kabisa ..hata kule kijijini wengine tulikulia migongoni mwa akina mama zetu wakati wakihangaika na mapishi au kuuza pombe (komoni, Kindi, chimpu na Kangara). Hakika wazazi waliweza kutupa pombe wakati huo. Ila kwa dhana ya malezi, kumpa mtoto ulevi kwa maana yeyote ile ni kumwaribu huyo mtoto. Hii ni sawa na kumwacha mtoto kuanza mapenzi mapema kabla ya umri, japo tendo husika ni "tamu" na pengine halina madhara ya moja kwa moja, lakini kwa ubongo wa mtoto haitamchukua muda kabla hajaharibikiwa. Waweza kulinganisha hata na baadhi ya watu wazima wenyewe wanavyoharibikiwa kutokana na kutumia vileo.

Mafundisho ya kweli kwa watoto ni kumzuia hasiyaone au kuyafuata yale ambayo hata kwetu watu wazima yanaweza kutuharibu akili na maisha kwa ujumla ukiwemo ulevi. Tuwaache waje wayajue wenyewe wakikua vinginevyo, mzazi utabaki katika kumbukumbu ya uharibifu wa maisha yake yote hapa duniani.
 
mwacheni mtoto anenepe jamani mbona mmesema sanaaaa., katoto kanajipatia tusker bariidi kakimaliza kanalala kwa utulivu.
 
Cjui nimeanza kunywa pombe lini. Nimekua na akili nikiwa na uwezo wa kunywa mbege bohora za lita 1 zaidi ya 4 at a time. Ila sio kigezo cha kuwapa watoto pombe. Vichwa vinatofautiana, mazingira na uwezo pia. God forbid. Wazazi na wananchi wote tuwapende watoto na tuwaepushe na vishawishi, tamaa na hatari zozote zilizowazunguka.
 
Kule Songea mbona mtoto kubembelezwa na ulabu ili alale ni kawaida tu. Halafu hiyo chupa imeandikwa "hairuhusiwi kunywa kwa wenye umri chini ya 18" lakini huyo mtoto kashika tu hiyo chupa yaani hajanywa. Kwa maoni yangu mtu mzembe na mshenzi ni huyo aliyempa chupa kushika na kumpiga picha (shame on him).
 
si limbukeni ni maisha aliyojichagulia yeye na familia yake,si ur life is how u made choise?
 
Ngoshwe,
Usisikitike sana. Watoto wangu walipokuwa wadogo walikuwa wakipenda kuonja Heineken yangu. Niliwaachia kwa sababu bia pia ina protein.
Lakini ukubwani wote hawajageuka kuwa walevi. Wananiangalia tu nikibighua bia zangu na mwingine ananiuliza " Dad why do you like beer so much?

ni kweli kabisa unajua pombe ni uamuzi wa mtu,watoo wengine wanalelewa bar lakini wanapokua wakubwa wankuwa hawapendi pombe
 
kama mzazi anafahamika tumshitaki,
naomba kuelewa, uwezekano wa kumpata huyo mzazi ukoje, kwani usipochukua hatua mtoto huyo atakuja kuwa chachu ya kupotosha mwanao.
 
No one is Guilty until Proven So. hapo tatizo ni nini?, Mtoto kushika hiyo chupa ya Bia au amekunywa hio bia???. picha inaonekana mtoto kashika Chupa ni sio kunywa. picha ingeonyesha mtoto anakunywa bia ndo ingekuwa tatizo. Kushika sio issue, ni mtoto mdogo huyo anaweza kushika chochote kibaya, ungemkuta na Kondomu je, ingekuwaje?????!!!!!
 
Tunawafundisha nini watoto wetu Bandugu?. Ni mzazi wa Kitanzania, anatundika picha ya mwanae hewani hivi ili walimwengu waone jinsi aleavyo mwanae.

Huyu mtoto hajui afanyalo na akikua kwa maadili haya, mzazi atakuwa na haki ya kumkea mtoto kama huyu?.Hivi ile Sheria ya Watoto (The Children Act, 2009 http://www.africa.gnrc.net/mm/file/positionpapergnrc.pdf) ina maana yeyote kwa Watanzania kama ilivyo kwa wenzetu Ulaya na Marekani ? Tokea imetingwa mwaka Jana 2009, sijapata kusikia makali yake hata kidogo japo ilisemekana itazuia mambo kama haya ikiwemo kupiga vita tabia za wazazi kuwatuma watoto baa au kuingia nao Baa na kumbi za starehe .

angalia mashavu na pozi lake hapo amepiga kitu bariidi.si masihara .hiyo 1500 ingetosha kununulia lita3 za maziwa.lakini watoto wengine wakikuona unakamua watalilia mpaka utawaonea huruma,wanaamini kila wanachotumia wzazi ni kitukizuri.
 
Samaki mkunje bado mbiiichiiii, akishakaukaa hakunjiikiii, ooooh enye wazaazii, ooh enyi wazazi!!
waliimba vijana jazz zama hizo kwa anaokumbuka
 
ningekua karibu ya aliyempa hii chupa ningemlamba kofi....................!
mbaya sana hii......................!
 
yaani katoto kazuri hivyo jamani!Ila ngoshwe usishangae,mm nimeona watu wanajichkelesha kuwa mtoto wao anapenda pombe kama vile ni sifa!au unakuta mjamzito anakunywa kama pampula,au yuko ngwasuma tena pembeni ya spika kabisaa na anacheza kuliko wacheza shoo!tumo humuhumu,tumepata ujumbe.Tuwaache watoto wakue,wachague wenyewe style gani ya maisha wanataka.
 
Back
Top Bottom