^^
Unaweza kumuuliza swali rahisi mpenzi mpya mf 'Kwa nini uliachana na mpenzi wako wa zamani?'
Anakujibu kwa kujiamini ' Yaani we acha tu, hakuniletea zawadi wakati wa birthday yangu, hajawahi kuni suprise! Yu no what bebi, is not that attractive'
Majibu kama haya kwa mwanaume makini unaetafuta mke,anastahili big NO.
Kwani ni wazi anahitaji muda wa kukua.
Mwingne unamuuliza swali lile lile, kwa nin uliachana na mpenzi wako wa zamani, jibu linakuwa ' Yule mwanaume hana staha kwa ndugu na rafiki zangu, alikuwa anataka anachopanga hataki kuingiliwa, hashauriwi'
Mwanamke wa aina hii, nampa BIG YES maana ni mpenda haki,anajitambua na yupo tayari kwa mazungumzo nyakati za kutoelewana.
Nimetoa mfano wa swali 1, ila kimsingi yapo Maswali 11 yanayoweza kukupa mwanga juu ya Past ya mwenza.
^^