Imefahamika, majina ya wamiliki DOWANS ni wafu.

Not_Yet_Uhuru

JF-Expert Member
Oct 11, 2010
1,304
431
Majina ya wamiliki wa DOWANS yaliyotolewa na Msanii na kuwadi wa RA, Waziri Ngeleja ni majina ya wafu, na yameundwa baada ya ziara ya fisadi RA kurudi safari zake za Asia na Uarabuni, ambapo bila wasiwasi tunagundua kuwa ndiko majina ya wanaotajwa na msanii Ngeleja kama ndio wamiliki. Inauma sana kuona udanganyifu huu kwa umma.

Naomba kuuliza, je haya yafuatayo hayawezekani kufanyika?
* kuandamana ili Ngeleja ajiuzulu kwa kuudanganya umma na kushindwa kuongoza wizara hii muhimu kwa umma?
* tuandamane kuomba interpol imkamate RA kwa kuvuruga utulivu wa nchi, kuongoza ufisadi na kuongoza utapeli na ufisadi wa kimataifa?
* kuandamana kuomba serikali itangaze wahusika wa 'biashara ya unga' ambapo RA tuna uhakika anahusika na ndio mkondo wake.?

Naomba kuwasilisha tujadili.
 
Weka basi ushahidi wa kuonyesha hao wamiliki ni wafu, ili tuanzie hapo kujadili
 
Kufa kishujaa ni bora kuliko kuishi kwa aibu........

Sasa watanzania tuendelee kuishi kwa taabuuu? bei ya mafuta taa, diesel,petrol zimepanda na hivyo nauli za daladala zitapanda,bei za vyakula zitapanda,sukari,mafuta ya kupikia n.k utaje...

Je kama bidhaa zitapanda, kipato chako kimepanda, mshahara wako umeongezeka??

Wanaokula mlo mmoja watapungua,na wanao kula milo 2 watakula mlo mmoja kwa siku.

Maisha ni magumu sana.

Wakati huo huo tunaibiwa kupitia mikataba feki, Dowans, EPA, MEREMETA na mengine utaje

Ukombozi hauji bila mapambano, maandamano ndo chaguo la sasa. twende mbele..
 
hOJA NZURI ILA SASA HAINA USHAHIDI. NI KAMA HISIA, SASA KUJADEILI MSTAKABARI WA HISIA TU SI SAWA HAPA
 
Majina ya wamiliki wa DOWANS yaliyotolewa na Msanii na kuwadi wa RA, Waziri Ngeleja ni majina ya wafu, na yameundwa baada ya ziara ya fisadi RA kurudi safari zake za Asia na Uarabuni, ambapo bila wasiwasi tunagundua kuwa ndiko majina ya wanaotajwa na msanii Ngeleja kama ndio wamiliki. Inauma sana kuona udanganyifu huu kwa umma.

Naomba kuuliza, je haya yafuatayo hayawezekani kufanyika?
* kuandamana ili Ngeleja ajiuzulu kwa kuudanganya umma na kushindwa kuongoza wizara hii muhimu kwa umma?
* tuandamane kuomba interpol imkamate RA kwa kuvuruga utulivu wa nchi, kuongoza ufisadi na kuongoza utapeli na ufisadi wa kimataifa?
* kuandamana kuomba serikali itangaze wahusika wa 'biashara ya unga' ambapo RA tuna uhakika anahusika na ndio mkondo wake.?

Naomba kuwasilisha tujadili.

Weka data ndg yangu maana utaonekana mzushi.
Kusema uongo kudanganya Watanzania
nina hakika ni sababu tosha ya kutokuwa na imani na waziri husika;Bora akajiudhuru mapema kuepuka aibu kabla ya bunge kukaa(Imperchment).
 
mi sielewi kitu kimoja, let say hiyo chadema imeshindwa uchaguzi coz haitawezekana ndani ya hii miaka 5 kuongoza nchi, mtazamo wangu ni huu.
instead ya kuendelea kulumbana kwa maslahi yao binafsi ya kushika nafasi za uongozi kwanini wao wasi organise hivi vitu? nikimaanisha wao kama ndio viongozi wetu ambao ni visible.
first- waandae hayo maandano ya huyo ngelaja kujiuzulu.
second- kuomba rostam aziz akamatwe.
third-kushinikiza serikali isilipe hiyo kampuni ya matapeli.
maana hapa tutaishia kutoa mada na kubwabwaja tu hamna chochote kinachofanyika kwasababu hatujuani na wala hiyo serikali haiwezi kufanya tunavyotaka.
im sure wakiomba watu waandamane kwa hivyo vitu,hamna atakayebakia ndani,hata mtu wa ccm atatoka ndani kwenda kuandamana
 
leteni majina yao,tupeleleze ktk list ya vizazi na vifo,kwani in the developed world kujua umekufa ni rahisi sana
 
Back
Top Bottom