I'm so low nifariji

I'm so low nifariji

Usitoe mimba ukizaa atakuja cha msingi muombe mungu na umwamin hakika atakutendea hata asiporudi huyo kidume mungu atafungua mlango mwingine
 
Ndugu ninapitia wakati mgumu sana kimwili na kiroho. nina mimba ya miezi 2 lakini mhusika amenitelekeza kwasababu nimekataa kuitoa eti hako tayari kulea mtoto kwa sasa. ameapa nikiamua kulea mimba hii basi nisimjue na kweli amekata mawasiliano hadi hapo nitakapokuwa tayari kutoa nimpigie. nimekubali kuilea japo sijajua nitaileaje. kazi ninafanya ya kibarua mahali ambapo wananiita wakati wakiwa na project. wazazi wako kijijini hawajiwezi.
Upo wapi?una qualifications gani??
 
shukrani zangu za dhati kwenu wote mnaojitolea muda wenu kunipa maneno ya kunitia nguvu. wanawake wanapitia mengi ni vile hawawezi kufunguka wote. raha mnapata wote na ahadi anakupa nyingi sana. linapokuja swala la matokeo ya raha anatoa udhuru. wanaume walio wengi mnabeba laana pasipo kujua. kwangu nimesamehe. nimeamua kutembea na huu mzigo kwa miezi yote saba iliyobaki. nimesoma kisa cha millen magese ambae ametafuta mtoto kwa miaka mingi kwa nini mimi niitoe hii mimba
 
Pole bint.
Sielewagi mwanaume anayekubali msitumie kinga na hahoji kama unatumia contraceptives kisha bint aki conceive aseme hayuko tayari kulea kulea,simuelewagi zaidi bint anayekubali ngono bila kinga wakati hajajadili kuhusu mimba na huyo mwenza wake. Tukubali kuwa kama hujabakwa mimba si ajali!!
Hongera kwa kuamua kulea mimba,hizo project ukilipwa huwa una save? Anzisha biashara hata ndogo tu ije iku assist baadae,ulezi si rahisi ila sio mgumu kiasi cha kukukatisha tamaa,watu wanatelekezwa na watoto wanne na wanalea mbona?
Sahau huyo loser,move on!!!
 
Ndugu ninapitia wakati mgumu sana kimwili na kiroho. nina mimba ya miezi 2 lakini mhusika amenitelekeza kwasababu nimekataa kuitoa eti hako tayari kulea mtoto kwa sasa. ameapa nikiamua kulea mimba hii basi nisimjue na kweli amekata mawasiliano hadi hapo nitakapokuwa tayari kutoa nimpigie. nimekubali kuilea japo sijajua nitaileaje. kazi ninafanya ya kibarua mahali ambapo wananiita wakati wakiwa na project. wazazi wako kijijini hawajiwezi.

Usitoe mimba, wala usiwe na wasiwasi, utapata msaada tu, na maisha yako yanaweza kuja kuwa better kuliko hivi sasa.
Wewe sio wa kwanza, nimeshuhudia mabinti wengi waliopitia hatua kama yako. Walilia sana mwanzoni baada ya kutelekezwa kwa staili hiyohiyo, baada ya kujifungua walipata faraja ambayo hawakuwahi kufikiri wangeipata.
Mlete mpwa huyo wala usihofu wajomba zake tupo.
 
shukrani zangu za dhati kwenu wote mnaojitolea muda wenu kunipa maneno ya kunitia nguvu. wanawake wanapitia mengi ni vile hawawezi kufunguka wote. raha mnapata wote na ahadi anakupa nyingi sana. linapokuja swala la matokeo ya raha anatoa udhuru. wanaume walio wengi mnabeba laana pasipo kujua. kwangu nimesamehe. nimeamua kutembea na huu mzigo kwa miezi yote saba iliyobaki. nimesoma kisa cha millen magese ambae ametafuta mtoto kwa miaka mingi kwa nini mimi niitoe hii mimba

Kibebi maisha hayana huruma hata kidogo, kuna mengi mabaya yanakuja, moja na la muhimu simama as single id n never ever trust anyone, Mungu tu na wazazi basi lakini the rest ni chenga tupu
 
thnx God umefunguka,dnt dare kuitoa,hata mimi nili experience the same thing,umesha fanya dhambi ya kuzini,usiongeze nyingine ya kuua kiumbe kisicho na hatia,na huna uhakika kama ukiitoa hiyo mimba utaweza kuja kuzaa tena baadae,na je ukipoteza maisha wakati wa kuitoa,achana nae huyo muhusika,amini hakuna kama mama,mshirikishe mama yako mzazi hata kama hana uwezo lazima atakusaidia na ataakikisha unajifungua salama,hilo limtu utaliona linakutafuta baadae sana akisikia umejifungua,utaamua mwenyewe sasa hapo atakapokurudia
 
To be down sometimes is human, to be always up is fictitious.

Cry, scream, yell, shout. Utapata ahueni isiyo na mfano.
 
In life kuna kupanda na kushuka.. Na hakuna jaribu lisilokuwa na mlango wa kutokea. Tambua ya kwamba wapo wenye jaribu kubwa zaidi yako so usikate tamaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom