I'm so low nifariji

kibebi

Senior Member
Feb 22, 2013
108
252
Guys, habari ya hapo mulipo? jioni hii niko down sana. Najisikia kukata tamaa kwani nilivyopanga haijawa kama nilivyotarajia. Pia ninapitia wakati mgumu sana kibinadamu.

Naomba unifariji jisikie huru kuweka ujumbe wako hapa au kuja PM kuweka ujumbe wenye faraja na huenda nafsi yangu itapata ahueni.

Naogopa kushirikisha watu kile kinachonisibu wengi siwaamini.

Afadhali hapa JF walio wengi hatufahamiani.

Asanteni.
 
Unalipa kodi nn,make mwenyewe bb mwenye nyumba anadai kodi june hii najisikia mbofu mbofu sana!!!!
 
Just tambua kwamba siku hazifanani, wewe unapanga na Creator naye alishapanga. N a kushindwa leo ndio mwanzo wa mafanikio ya kesho. Hauko pekeyako kuna walioshindwa makubwa kuliko wewe. Wapaswa kumshukuru Mungu kwa kukuwezesha kufanya na kufanikisha hayo machache uliyoweza.
 
^^
Usiumie zaidi, kwani safari ya maisha haikuwahi kuwa rahisi kwa yeyote aliyepangiwa mafanikio! Legeza mwili.. Kama leo umekwama kesho itafunguka! Utafurahi.. Ndiyo huhitaji kuamini kila mtu ila unahitaji kuamini katika wewe! Rudi katika nafasi yako! Jipende! Jijali! Furahia.
Dont worry too much about tomorrow for God has been there for you!
Remember to smile inside yourself
^^
 
Pole kila jambo hutokea kwa sababu,pamoja hatujui kinachokusibu jipe moyo utavuka salama,chukulia mfano mdogo wa mkondo wa maji na tabia zake,maji yanapotiririka yakikuta kizuizi huwa na choice 3,moja kama kizuizi ni kidogo hukiondoa yaendelee na safari,kizuizi kikiwa kikubwa hufanya maamuzi either yapishe kizuizi pembeni yaendelee na safari au yatulie yakusanyike yawe mengi na hatimaye yakivuke kile kizuizi,daima hayarudi nyuma ,nawe usikate tamaa vua viatu kung'uta vumbi songa na life.
 
Pole sana ungefunguka basi nini tatizo kibebi

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums

Ndugu ninapitia wakati mgumu sana kimwili na kiroho. nina mimba ya miezi 2 lakini mhusika amenitelekeza kwasababu nimekataa kuitoa eti hako tayari kulea mtoto kwa sasa. ameapa nikiamua kulea mimba hii basi nisimjue na kweli amekata mawasiliano hadi hapo nitakapokuwa tayari kutoa nimpigie. nimekubali kuilea japo sijajua nitaileaje. kazi ninafanya ya kibarua mahali ambapo wananiita wakati wakiwa na project. wazazi wako kijijini hawajiwezi.
 
Ndugu ninapitia wakati mgumu sana kimwili na kiroho. nina mimba ya miezi 2 lakini mhusika amenitelekeza kwasababu nimekataa kuitoa eti hako tayari kulea mtoto kwa sasa. ameapa nikiamua kulea mimba hii basi nisimjue na kweli amekata mawasiliano hadi hapo nitakapokuwa tayari kutoa nimpigie. nimekubali kuilea japo sijajua nitaileaje. kazi ninafanya ya kibarua mahali ambapo wananiita wakati wakiwa na project. wazazi wako kijijini hawajiwezi.

Pole sana, Mimba ni rahisi sana kulea kwani tumbo kila mahali unakuwa nalo,ishu kubwa ni kwenye mtoto kama huna support walah unahisi dunia imeturn agaist you, All in All lea hiyo mimba mengine yatajulikana mbeleni..Huyo mwanaume achana nae,hukupangiwa na mwenyezi mungu awe wako...
 
Maisha ni mapito rafiki na yamejengwa na changmoto nyingi!bila changamoto maisha haya yangekuwa yanaboa sana.Changamoto hizo zinapima uvumilivu wetu na uwezo wetu wa kuchanganua vitu kwa maarifa.Chukulia haya unayoyapitia sasa ni mapito katika maisha wakati wa kuvuna utafika na utasahau machungu na maumivu yote!
 

Attachments

  • 1401414551110.jpg
    1401414551110.jpg
    9 KB · Views: 975

Similar Discussions

Back
Top Bottom