Uncle bright
JF-Expert Member
- Feb 9, 2023
- 1,040
- 4,081
Habari zenu ndugu zangu, naombeni ufafanuzi
Mungu alishakataza pombe agano la kale na hata Yesu katika ile sala ya baba yetu ulie mbinguni kuna sehemu ya kuomba tuepushwe na majaribu ili tuepuke uovu.
Sasa inakuwaje tena kwamba hii pombe inabidi tuwe wanywaji na sio walevi?
Pombe ni dawa ya kulevya iliyohalalishwa kisheria kama ilivyo sigara. dawa zingine za kulevya ni bangi, mirungi, cocaine, n.k. zote hizi zinatumika kumlewesha mtu kwa namna tofauti. Pombe ni depressant drug, Bangi ni stimulant drug, cocaine ni hallucination drug, n.k. tena pombe ni hatari zaidi kuzidi hata bangi, huko makazini wapo wavuta bangi wanastua kabla ya kazi ila wanapiga kazi na ni ngumu hata kugudua, lakini kwa wale wanaokunywa pombe wanagundulika kirahisi kwa matendo na hata harufu kinywani, mlevi wa pombe kufukuzwa kazini ishazoeleka.
Hivi jamani kunywa pombe tu sio majaribu hayo? Maana ukinywa unapata karaha kenye majaribu ya kutaka kuendelea, pia akili inakuwa imeshuka uwezo wa kufanya maamuzi tofauti na ukiwa hujanywa, pombe nyingine hata ukinywa bila hata kulewa zinaanza kukupa ashki ya kufanya ngono.
Walevi nao huwa wanaanza kwa unywaji wa glasi moja tu tena unakuta ni mara 1 kwa mwezi, ila ikianza kumkolea hata hicho kiglasi hakina kazi tena inabidi aanze kupiga chupa mbili hivi na mazoea huanza kujengeka ya kunywa karibu kila baada ya siku kadhaa, hapo ni mnywaji tu, akianza ulevi pombe inakuwa kama dozi ni kila siku ama mara tatu kwa kutwa kama dawa.
Hata wale walevi wa bangi, unga, sigara, kamali, uzinzi, huwa mwanzoni wanaonja kidogo tu lakini ile raha ikianza kuwakolea ni majaribu tosha, wanajikuta tayari kwenye dimbwi zito kuchomoka inakuwa taabu. Hawezi kuvuka hata siku 2 ama 3 bila kustua.
Sasa inakuwaje kwamba tunaomba tuepushwe na majaribu huku tunajiweka kwa majaribu?
Hadi sasa ni wasabato pekee ndio nimekutana nao wao sheria zao zinapiga marufuku hata kuonja tone.