NetMaster
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 1,454
- 4,853
Wasabato mkae pembeni hili haliwahusu
Sijawahi kuelewa hata kidog haya mambo ya unywaji na ulevi, huwa naonaga ni kama tiketi tu ya kuhalalisha ulevi.
Kama ni mlevi ama uliwahi kuwa mlevi wa sigara, bangi, pombe, ngono zembe, kamali, n.k. basi unajua fika kwamba siku ya kwanza huwa ni kujaribu kidogo tu lakini ukianza kadri siku zinavyoenda kukumbuka ile raha yake unajikuta tayari umeingia kwenye shimo la ulevi.
Sasa nachojiuliza ni kwamba, katika sala ile ya Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje, kuna kipengere tunamuomba Mungu pia atuepushe na majaribu... ni vipi aliweza kuruhusu unywaji wakati ni wanzo wa kuwa mlevi ?