Ilinibidi kupitiliza kituo baada ya kuhisiwa mwizi

Nikiwa hatua chache kufika sehemu nayotakiwa kushuka kabla sijamwambia dereva anishushe mara namuona mdada anahangaika akisakua mkoba wake na kujisachi, kwa wenge akasema "Simu yangu siioni!!.... Nimepoteza simu yangu!" Daah!.... Zoezi langu la kutaka kumwambia dereva anishushe liliishia hapa kwa muda. Kwani ungekuwa wewe ungeshuka ndugu ili mdada akujazie watu
😂😂😅😅😅😅😅😅
 
Siku moja nimepanda bajaji kwenda eneo fulani nilikuwa nimekaa na mdada mmoja maneno mengi sana ambaye inaonekana anajuana na dereve bajaji au wamezoeana muda mchache.

Nikiwa hatua chache kufika sehemu nayotakiwa kushuka kabla sijamwambia dereva anishushe mara namuona mdada anahangaika akisakua mkoba wake na kujisachi, kwa wenge akasema "Simu yangu siioni!!.... Nimepoteza simu yangu!" Daah!.... Zoezi langu la kutaka kumwambia dereva anishushe liliishia hapa kwa muda. Kwani ungekuwa wewe ungeshuka ndugu ili mdada akujazie watu?

Basi mwanaume nikakomaa bajaji ikichanja mbuga, mdada akamgeukia dereva akamwambia "Hebu niazime simu yako nibeep simu yangu nilikuwa nayo hapahapa!" Aibu kweli unafikiri kwanini hakuniomba mimi simu ajibipu!? Nadhani alihisi mimi ndio mwizi.

Wakati ananyanyuka kuchukua simu ya dereva bajaji Mungu si Athumani simu yake ikaanguka toka kwenye nguo zake, na alikuwa amejipigilia nguo haswaa kama kurasa za kitabu kama mjuavyo wanawake wa kiswahili mapigo yao (baadhi yao lakini)

Muda huohuo nikamuomba dere anishushe, nikashuka na kwenda bar ya jirani kupoza koo

View attachment 2156840
Nchi Ngumu Sana Hii Masta.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom