winston20
JF-Expert Member
- Jun 21, 2020
- 1,117
- 2,256
SURA YA KWANZA
28/3/1989
Ulikuwa ni msafara wa watu watano, wawili kati yao, pamoja na mimi mwenyewe,
tukiwa ni waandishi wa habari waajiriwa wa kampuni ya Film Tanzania ambayo
ilikuwa ni kampuni ya habari na matangazo iliyojihusisha pia uchapaji wa
magazeti ya Tabasamu na Sunday, wakati wale wengine wawili walikuwa ni
wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambao walikuwa wanafanya tafiti
kwa ajili ya shahada yao ya pili pale Mlimani.
Tulikuwa ni watu wenye furaha kubwa kutokana na namna ambavyo kazi yetu
ilivyo kwenda sawa bin sawia, ilituchukua zaidi ya wiki mbili tukiwa mkoani Geita
tulikokwenda kikazi, ambapo kampuni ilituteuwa kwenda huko kuangazia matukio
yaliyokuwa yakiendelea kutokea katika mkoa wa Geita ambayo kwa kiasi
kukubwa yalikuwa yakigusa hisia za watu wengi nchini na hata duniani kwa
ujumla…migogoro ya wakulima na wafugaji.
Siku hii ya Jumatano ya tarehe 28/3/1989 ni tarehe ambayo haiwezi kufutika katika
akili yangu kwa miaka mingi mno.
Safari ilikuwa ndefu mno kiasi fulani ilinichosha, lakini hata hivyo kila nilivyo
fikiria matunda ya kazi iliyotupeleka huko kwa kweli nilipata nguvu kubwa.
Mwendo mkali wa Land Cruiser iliyokuwa ikiendeshwa na bwana Magembe
Matiku tulitazamia kati ya saa mbili ama saa tatu tutakuwa tumekwishawasili jijini
Dar es Salaam.
Tulindoka mkoani Geita mapema alfajiri. Awali wakati tunaanza safari ndani ya ile
Land Cruiser kulirindima maongezi vicheko na utani mwingi miongoni mwetu,
lakini kadri muda ulivyozidi kuyoyoma ndivyo zile bashasha zilivyozidi kuyeyuka,
hii ni kutokana na umbali mrefu wa safari yetu uliosababisha kukinaiwa na safari
ile ndefu.
Saa tisa juu ya alama tuliingia mkoa wa Dodoma, hapo bwana Magembe Matiku
dereva wa ile Land Cruiser alitutaka tupate chakula cha mchana kabla ya
kuendelea na safari ile, tuliingia katika hoteli iliyokuwa ndani ya kituo cha mafuta
cha Gapico na kujipatia chochote.
3
Jua lilikuwa ni kali mkoani Dodoma tofauti na mikoa tuliyopita huko nyuma, jaketi
nilililokuwa nimevaa halikuwa na nafasi tena katika maungo yangu.
Nililivua.
Wakati naliondoa lile jaketi maungoni mwangu nililiweka katika mgongo wa kiti
nilicho kuwa nimekalia kisha nikaendelea kushambulia chakula kilichokuwa
mezani kwangu kwani njaa ilikuwa ikiniuma kisawasawa.
Katika meza niliyo kuwa nimeketi, sikuwa peke yangu tuliketi wawili mimi na
Loveness huyu alikuwa ni mfanyakazi mwenzangu tuliyekuwa pamoja katika ule
msafara wa Geita.
Hatua chache kidogo kulikuwa na meza iliyokaliwa na watu watatu yanii bwana
Magembe Matiku ambaye ni dereva wa kampuni yetu, pamoja na john, na
mwenzake Fidelix hawa ni wale wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam
waliokuwa katika utafiti wa masomo yao.
Sambamba na hilo, katika viti vingine vilivyokuwa mule katika hoteli ile kulikuwa
na watu wengine wengi tu ambao walikuwa wakijipatia chakula mchana ule,
Upande wa mbele wa meza niliyokuwa nimekaa kulikuwa na meza nyingine
iliyokaliwa na mkaka aliyekuwa akinitumbulia macho pindi tu nilivyosaula jaketi
katika maungo yangu.
Macho yetu yaligongana mara mbili, awali nihisi imetokea bahati mbaya na
nikaendelea kushughulika na kula, macho yakiwa katika sahani.
Angalau sasa tumbo langu lilishiba, nikanyanyua uso wangu kuangaza eneo la
kunawia mikono. Lakini wakati nafanya hilo, bahati mbaya tena nikagonganisha
macho na yule mwanaume kwa mara nyingine tena, hapo nikagundua kuwa yule
kaka alikuwa akinitizama muda wote. Pia alikuwa akiniangalia katika namna
ambayo ilinielewesha kitu gani kilikuwa kinapita katika akili ya yule mtu.
Ajabu ni kuwa, pindi nilivyopata kugonganisha macho na yule mtu kwa mara hii
ya tatu nilipatwa na kitu fulani cha ajabu katika mwili wangu hali iliyonifanya
nistajabu.
Nilipapatwa na ganzi chini ya mapaja yangu lakini wakati huohuo nikajikuta
naingia katika siku zangu japo nilikuwa na wiki moja tangu nitoke katika hedhi na
siku zangu za hedhi huwa hazina kawaida ya kubadilika kiasi kile.
4
Upesi akili yangu ikaanza kufikiri kuhusu mkoba wangu ulio kuwa ndani ya ile
Land Cruiser ambao ndani yake kulikuwa na pedi ambazo huwa natembea nazo
wakati wote.
Nazipiga hatua kwenda kunawa mikono, kabla ya kuendea mkoba kwa ajili ya
kujihifadhi na damu iliyokuwa inachafua nguo yangu ya ndani.
Wakati nikiwa nanawa mikono, niligeuza shingo kumwangalia yule mtu, nikaona
bado ananitizama katika namna ile ile. Nafikiri macho yake yalikuwa yakivutiwa
na uzuri wa sura niliyojaliwa na Muumba, na pengine labda macho yake
yalivutiwa na umbo langu lililokuwa kama namba nane, ningekuwa nimevaa blauzi
ya kubana ningesema labda yale macho yalikuwa hayajiwezi kwa sababu ya
maziwa yangu saizi ya embe dodo bichi, lakini kwa bahati mbaya au nzuri
nilikuwa nimevaa shati lilionikaa vizuri ikiwa kwa ndani ya kifua changu nikiwa
nimeyabana maziwa yangu kwa sidiria ndogo.
Sasa vipi huyu mtu anitumbulie mimacho kiasi kile..!
Anajua yeye mwenyewe.
“Zahara vipi tena mbona hivyo?” Loveness alinistua wakati nikitoka ndani ya
hoteli ile kuelekea mahala lilipokuwa gari.
“Aah!. we acha tu shosti niko kwenye siku zangu mwenzio nafuata mkoba garini
nichukue pedi nijistiri”
Nilimjibu haraka haraka kwa sauti ya chini, kisha nikazipiga hatua upesi kwenda
lilipokuwa gari. Lakini wakati huo huo bwana Magembe Matiku na Fedelix
pamoja na John nao walikuwa wanatoka mule hotelini.
“Jamani hatuna muda wa kupoteza wapenzi inabidi tufike Dar es Salaam kabla ya
saa tatu usiku” alisema bwana Magembe akichezeshachezesha lundo la funguo
mkononi mwake.
Niliongeza mwendo hadi katika ile Land Cruiser nikachukua mkoba wangu
uliokuwa na pedi kisha kikaelekea maliwato na kujihifadhi.
Wakati huo, yule mtu aliyepatwa na ugonjwa wa kuniangalia angalia hovyo
nilikuwa nimekwishamsahau katika akili yangu.
Dakika kumi zilizofuata tulikuwa ndani ya gari tukiuacha mji wa Dodoma na joto
lake, gari lililokuwa likiendeshwa na bwana Magembe likiwa katika mwendo
mkali hatari.
5
Kulikuwa na maongezi ya hapa na pale ndani ya gari. Lakini wasaa ule niliishia
kuelekeza macho yangu huko nje nikiangalia vijumba vifupi na vidogo vya makuti
vilivyokandikwa kwa udongo, yakiwa ni makazi ya wanakijiji wafugaji jamii ya
Wagogo.
Dakika arobaini baadae watu wote walikuwa wanasinzia isipokuwa mimi na
bwana Magembe. Kulirindima ukimya garini zaidi ikiwa ni mlio wa gari uliokuwa
ukilalama kutokana na vile bwana Magembe alivyokuwa akilivuta kisawasawa.
Ni hapo nilipo kumbuka radio yangu ya CD kifaa nilichokitumia kusikiliza muziki
mbalimbali niliyoihifadhi katika CD…..na wakati nakumbuka kifaa kile ndipo
hapo moyo wangu ulipopiga “paaaaaaa” kila kitu kilipita katika akili yangu kama
tamthilia.
Nikajikuta napiga ukulele wa fadhaa. “Jaketi languuuuuuu!!..” Nikamstua kila mtu
aliyekuwa amelala.
Na sasa nikakumbana na maswali lukuki kutoka kwa wenzangu. Vipi nibwate kwa
sauti kubwa kiasi kile kwa ajili ya jaketi. Thamani yake ni kubwa kwa kiwango
gani hata nibweke namna ile na kuondoa kabisa utulivu wa watu mule garini.
Nilibaki nimeganda nimekodoa macho, mdomo wangu ukiwa wazi,lakini mkono
wangu wa kushoto ukiwa umefunika domo lile, sura yangu ikiwa imejaa mshangao
mkubwa.
“Zahara kwani hilo jaketi la kazi gani tena ilihali Dar es Salaam lingeenda kukaa
katika begi, tena pengine lingeishia kuwa chakula cha mende na panya”.
Alisema John akimaanisha hapakuwa na sababu ya kujutia kulisahau jaketi ilihali
mahala ninakokwenda ni sehemu ya joto kali ambapo uhitaji wa masweta na
majaketi haupo.
“Naenda kufanya nini Dar es Salaam bila lile jaketi jamani? ndani ya hiyo nguo
kulikuwa na kila kitu ambacho kilitupeleka Geita. Kitabu chenye taarifa zote kipo
katika mfuko wa jaketi, kamera ndogo yenye picha za video pia ipo katika mfuko
wa jaketi, kinasa sauti kilichokuwa na sauti za mahojiano tulizofanya na wale
jamaa waliokuwa wanagombana kuhusu mipaka, kifaa kile kimo katika mfuko wa
jaketi, na hata zile karatasi za maswali na majibu ya mkuu wa mkoa zooote zimo
katika mfuko wa jaketi. Lakini pia, hata vitambulisho vyangu vyote vimo katika
lile jaketi”.
6
“Nooooo!!.” Nini tunafanya jamani!!. nini hiki aah” bwana Magembe alipiga
kelele baada ya kutoa maelezo yale. Na mwisho alikanyaga breki ghafla na gari
likasimama katikati ya barabara huku tairi za gari zikijiburuza katika lami na kutoa
mlio mkali wa mburuzo.
Kwa kweli maelezo yangu yalimchanganya kila mtu hasa wale wafanyakazi
wenzangu, vifaa vilivyokuwa katika jaketi vilikuwa ni vitu muhimu kwa
mustakabali mzuri wa ajira zetu.
Kamwe mkurugenzi isingeweza kutuelewa kama tungerudi bila taarifa yoyote ya
Geita ilihali ofisi iligharamia gharama zote za utafiti wa makala ile na hata kutulipa
pesa nzuri tu kwa kipindi chote ambacho tulikuwa mkoani Geita.
“Sasa tunafanya nini jamani” aliuliza Loveness.
“Unajua kama huu ni uzembe wa kipuuzi ulio ufanya wee Zahara” badala ya
kujibu bwana Magembe Matiku aliyekuwa amefura kwa hasira alinitupia lawama.
Nilijisikia vibaya mno kwa maneno yale ya bwana Magembe lakini sikuwa na la
kufanya kwani kweli kosa lilikuwa langu japo sikukusudia kulitenda. Sikujibu
chochote zaidi ya kuwa kimya nikingoja maamuzi ya wenzangu juu ya ni kitu gani
watafanya.
“Hatuna chaguo jingine zaidi ya kurudi Dodoma” Fidelix aliyekuwa kimya muda
mwingi alishauri, Ushauri ulioungwa mkono na John na hata Loveness, bwana
Magembe alikuwa amevimba kwa hasira alitizama saa yake ya mkononi na kuona
ilikuwa ni saa kumi na mbili na robo za jioni.
Aliachia breki na kuingiza gia kisha akaliondoa gari kwa kasi na kukata kona kwa
kasi na kulielekezea kule tulikotoka.
Safari ya kurudi Dodoma ikaanza.
Ilituchukua dakika arobaini na tano nyingine kufika Dodoma mjini na hapo
tukanyooka na barabara kama tunaelekea Singida na kilometa moja nyingine
tukawa tumefika katika kile kituo cha mafuta ambacho kilikuwa na huduma ya
mgahawa.
Hapo ilikuwa yapata saa mbili kasorobo usiku.
Nilikuwa wa kwanza kushuka katika gari na kukimbia ndani ya ule
mgahawa,nilipo ingia ndani macho yangu moja kwa moja katika kiti nilichokuwa
nimekalia ambapo ndipo nilipoweka lile jaketi.
7
Moyo wangu ulinidunda kwa nguvu kutokana na kile nilichokiona, kiti kile
kilikuwa kitupu. Lile jaketi halikuwepo mahala pale.
Sasa nilianza kuona dalili ya kupoteza kibarua chuangu kinachoniweka mjini mimi
na familia yangu.
Kwa muda wa nusu dakika niliweza kuona maisha ambayo nitakwenda kuishi
muda mfupi ujao baada ya kufukuzwa kazi katika kampuni.
Nilimwona mama mwenye nyumba wangu (mama Leila) namna atakavyokuwa
akinisumbua juu ya kodi yake ambayo ilikuwa ikielekea ukingoni, niliona namna
wazazi wangu watakavyokuwa wakinipigia simu mara kwa mara na kuhitaji
msaada wa kifedha kutoka kwangu hali ya kuwa wakati huo mifuko yangu itakuwa
imetoboka kwa kutokuwa na ajira yenye kuniingizia pesa.
Lakini pia, niliona namna mdogo wangu Nasri namna anavyositisha masomo yake
kwa kushindwa kuendelea kumsomesha kwa kukosa ajira yenye kuniingizia fedha.
“Vipi dada yangu kulikoni?” nilistushwa na sauti ya muhudumu wa mgahawa ule
aliyekuwa amesimama nyuma yangu na kunishangaa namna nilivyokuwa
nimeganda mithili ya sanamu.
Lakini kabla sijamjibu, muda huohuo akina Loveness nao wakaingia.
“Vipi umeliona” wote waliniuliza kwa pamoja kana kwamba waliambizana.
“Hapana, kiti ni kitupu, jaketi halipo”
“Shuuuuph” bwana Magembe alishusha pumzi huku mikono yake ikiwa kiunoni.
“Kwani kuna nini jamani” Muhudumu wa ule mgahawa aliuliza.
“Kuna jaketi nililisahau katika kiti hiki wakati tulipo kuja kula chakula hapa kama
lisaa limoja hivi limepita”
“Jaketi la rangi ya kaki..?”
“Ndiooo” niliitikia upesi upesi nikihisi kuna uwezekano wa kulipata ile nguo kwa
kuona muhudumu yule analifahamu.
“Hiyo nguo niliichukua na kuipeleka ofisini lakini alikuja mkaka mmoja jina lake
nimelisahau alisema lile jaketii ni la mwenzenu ambaye mpo nae katika safari
moja mkitokea Geita na ulikuwa umelisahau na mmemtuma yeye aje kulichukua
hapa”
8
“ Whaaat!.”
Wote tuliuliza kwa mshangao, kwa pamoja.
“Kwani ninyi huyo mtu hamjamtuma na hamjui?!” Muhudumu aliuliza tena kwa
mshangao.
“Hicho kitu unacho sema kigeni kabisa. Hatumjui huyo mtu” John alisema.
“Na kwani huyo mtu yukoje” niliongezea kwa kuuliza.
“Mkaka mweusi mrefu ana kitambi kidogo, wakati ninyi mnakula chakula yeye
alikuwa amekaa katika kiti hicho hapo” Hapo taswira ya yule mtu aliyekuwa
akinikodolea mimacho yake mibaya hadi nikaingia katika siku zangu, sura yake
ikanijia mbele yangu
“Blood fool mijitu mingine sijui ikoje kudada’deki ni lile likaka lililokuwa limekaa
hapo likiniangalia hovyo” nilisema kwa ukali huku nikihisi huzuni isiyo na kifani
“Basi huyo mvulana atakuwa ni mwizi” Loveness alisema pia kinyonge.
“Sasa tutafanya nini?” mtu mwingine aliuliza, mie nguvu zilikwisha, niliona
nilichokuwa nimebakiza ni kufukuzwa kazi na kuingia uraiani na kupambana na
ukali wa maisha kwa namna nyingine.
“Kuna kituo cha polisi hapo mbele kama hamtojali tuongozane tukafungue kesi”
alisema yule mfanya kazi wa ule mgahawa.
Tulikubaliana na ushauri wa yule muhudumu tulikwenda kituo cha polisi na
kufungua kesi kisha tukapewa RB.
Baada ya hapo safari ya Dar es Salaam ikaanza tena.