Ilikuwaje watu wakaamini kwamba Tanzania inaweza kuendelea bila kushirikiana na dunia?

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
20,897
63,784
Huwa nawaza sana tulifikaje hapa tulipo leo,

Hivi ilikuwaje taifa lenye wasomi wazuri kabisa likaamua kufanya maamuzi ya kipumbavu ambayo hata Waroma wa kale walioishi miaka 2000 iliyopita wasingeyafanya. Hivi katika maksudi kabisa, taasisi nyeti za Tanzania ziliamini kabisa kwamba wao wangeweza kuifanya Tanzania nchi tajiri bila kushirikiana na dunia : Hivi ilikuwaje kabisa wataalamu wetu ambao wameenda shule, wanafahamu mifumo ya dunia ya kiuchumi, kiulinzi na kisiasa na wako kule USALAMA, BENKI KUU na MAMBO YA NJE wakakubaliana na huu upumbavu na kuanza kuutekeleza kabisa?

Mpangilio wa dunia yetu ya sasa uliwekewa msingi mwaka 1814 kule Vienna baada ya miaka 25 ya vita za mfalme Napoleon Bonaparte. Mwanamfalme Von Matternich alifahamu kabisa ili dunia isirudie kuingia kwenye songombingo la vita au kadhia yoyote ile, basi ni lazima watengeneze mfumo ambao uko kama utandu wa bui-bui: Kwamba maamuzi ya nchi moja yakifanyika lazima yaathiri nchi zote, hivyo nchi lazima zikubaliane kwenye baadhi ya mambo muhimu yanayowagusa wote. Ndiyo nadharia ya MZANI WA NGUVU (Balance of Power) ikazaliwa.

Mfumo wa dunia ya yetu hii tunayoishi leo hii umejengwa na matukio yaliyotokea miaka ya 1913, 1914, 1918, 1920, 1927, 1928, 1933, 1935, 1939, 1941, 1944, 1945, 1947, 1948, 1971 na 2001 . Kiufupi mlolongo wa matukio haya yafuatayo ndiyo yanatoa mwelekeo mzima wa mwenendo wa dunia yetu ya leo : Nashauri tufanya utafiti wa ndani kuhusu hili.

Formation of the Federal Reserve, World War I, Versailles Peace Treaty, Formation of League of Nations, Signing of Kellog-Briand Pact, The Great Depression, The Monte-Video Convention, America's Abolition of Gold Standard, World War II, The Bretton Wood Agreement, Formation of UNO, Signing of the GATT, Publication of the Universal Declaration of Human Rights, Nixon's Abandonment of the Gold Standard and China's Admission to the WTO n.k.

Mtaalamu yoyote yule wa Uchumi, Diplomasia, Ulinzi na Sheria ni lazima afahamu fika kuhusu haya ninayoyasema hapa. Kwamba dunia nzima tuko ndani ya utandu moja wa bui-bui. Huwezi kufanya jambo lolote lile ukiwa nje ya hapo. Ndani ya huu utandu wa bui-bui kuna kila aina ya watu: Wema na wabaya, Huru na watumwa, Masikini na tajiri, Wenye matumaini na wasio na matumaini, Wababe na dhaifu na Waamini Mungu na Maadui wa Mungu.

Huu ndiyo mfumo wa dunia (The World Order), huwezi kufanya maajabu yoyote yale ukiwa nje: Hata mataifa makubwa yenye nguvu duniani yanaheshimu huu mfumo kwasababu yanafahamu siku mfumo huu unaharibika basi ndiyo utakuwa mwisho wao. Hivyo kuna baadhi ya sheria hata yenyewe yatazifuata tu kwasababu zina manufaa kwao. Mwandishi George Orwell kwenye The ANIMAL FARM aliwahi kusema "All animals are equal, but some are more equal than others" hivyo hata kama tunataka usawa kuna wale waliotutangulia watakuwa mbele yetu kwenye baadhi ya mambo tu.

Sasa kinachoumiza wasomi wa Tanzania wenye PhD za sheria, uchumi na diplomasia. Huku wengine wakiwa na shahada kwenye masomo ya ulinzi, usalama na sayansi za vita wakiwa na akili timamu kabisa, wakaamua kuwa wapumbavu. Wakatundika elimu zao nyuma ya milango na kuanza kutekeleza jambo ambalo hata watu wa kale walioishi miaka 2000 hawakuwahi kuliwaza. Tanzania ina matatizo mengi, lakini ilikuwa inarekebishika vizuri tu kwasababu waliofikisha nchi yetu hapa wanafahamika na tunakula na kunywa nao kila siku.

Kuanza kulaumu mabeberu peke yake haisaidii kwasababu kuna wenzetu ambao wamefanikiwa kutumia mifumo hii-hii ya mabeberu kuwashinda mabeberu kiuchumi, kiulinzi na kisiasa. Ukweli ni kwamba huu mfumo umejengwa na mabeberu lakini hata walioujenga hawaundeshi wanavyotaka wao. Mataifa ya Magharibi ndiyo waanzilishi wa World Trade Organization (WTO) lakini leo hii, WTO imemnufaisha Uchina kuliko tangu alivyojiunga nao mwaka 2001 na mpaka sasa wanajutia kumkaribisha.

Nchi kama Singapore, India, Korea-Kusini na Brazil wamewezaje kucheza vizuri kwenye huu mfumo wa mabeberu hadi kufikia kuwango cha kuwashinda mabeberu kwenye baadhi ya mambo ??? Inahitaji akili ya ziada kutoka kwa Mungu ili kuweza kucheza kwenye huu mfumo. Raisi Donald Trump alijaribu kuitoa Marekani kwenye huu mfumo wa Vienna, lakini pamoja na maguvu yote ya Marekani alifanikiwa ???

Lakini leo hii kuna watu wako ndani ya IDARA ZA USALAMA ZA TANZANIA waliamini kabisa kwamba Tanzania inaweza kujitenga na dunia bila kupata madhara. Yaani waliamini kabisa na wengine bado wanaamini kabisa. Kuna wengine bado wanaamini kwamba mfumo wa Kileninisti na Kimaksisti (Marxist-Leninism) unaweza kutumika kuikomboa Tanzania. Sawa, lakini hata walioutuletea huu mfumo Warusi na Wachina, wamebadilisha sana baadhi ya hizi falsafa.

Dunia ya nchi moja kutawala wengine (Uni-Polar World) au nchi mbili kuamulia dunia nini kifanyike (Bi-Polar World) unakufa taratibu, ndiyo maana Marekani na Urusi wanapata shida kukubaliana na huu ukweli. Wao kama mataifa hawaanguki na bado wana nguvu, ila tu ni kwamba mataifa yale madogo na masikini kama Vietnam, Poland, Mexico yamekuwa makubwa yenye uchumi unaokua kwa kasi sana.

Tanzania tuliachiwa mtaji mkubwa sana kidiplomasia, ambao ulitujengea SOFT-POWER na INFLUENCE ambayo ilifanikisha ulinzi na usalama wa Tanzania kikanda na kidunia kwa kiwango kikubwa sana. Tuliingia sehemu ambazo hata nchi kubwa hazikuweza kuingia, tulipata taarifa nyeti kabla hata baadhi ya mataifa makubwa hayajazipata, tulipewa heshima ya kipekee (Special Treatment) ambayo mataifa mengine yenye uchumi mkubwa kuliko sisi barani Afrika hayakupewa.

Tuliogelea bwawa moja na mababeru, wakomunisti, wajahidina na wazayuni lakini tulitoka salama, kesho tena tukarudi kuogelea. We were a Shrimp among Whales, lakini bado tuliheshimika mno. Lakini leo hii hebu angalia, ile nguvu yote ambayo Mzee Nyerere na Raisi Mkapa walitutengenezea, imemomonyoka kisa kikundi cha watu wachache wasiokuwa na uelewa mpana wa mahitaji ya nchi yetu na nafasi yetu hapa ulimwenguni.

Binafsi naamini ili tuweze kutoka hapa tulipo ni lazima NYUMBA ISAFISHWE aidha mbele ya majirani au kisiri. Mambo ya UHAINI, KUHODHI MADARAKA, KUPANGA KUUA MARAISI WASTAAFU,KUSHIRIKIANA NA MAADUI WA TAIFA na KUWINDANA KWA KUTUMIA MAKUNDI NDANI YA TASISI ZA KIUSALAMA (Cloack and Dagger Diplomacy) tulikuwa tunayasikia nchi jirani tu: Kwetu sisi yalikuwa ni MWIKO KABISA. Vitendo vya kihaini tulishaachana navyo awamu ya kwanza. Lakini leo kuna kakundi kalifikiri kabisa kangeweza kutupangia sisi Watanzania nani awe Mkuu wa nchi kweli?

Halafu bado haka kakundi kanalelewa tu: Kuhakikisha kwamba nchi haiwezi kurudi tena kule ilipotoka there's one place these people belong : The Cemetery, A Noose or A Bullet in the head!!! A prison term is not enough for these ruthless and deranged fanatics (This is legal, legitimate, justified and righteous).

Mara nyingine huwa naumia sana kuhusu Tanzania, natamani hata nisingekuwa nayafahamu haya yanayondelea.....
 
😆😆😆

20211117_154133.jpg
 
Hakuna ambae hakutaka kushirikiana na nchi nyingine ila kushirikiana kwa kutunyonya hilo ndo tulikataa awamu ya tano na inatakiwa iwe hivo kwa nchi zote za Africa gasa kusini mwa jangwa la sahara! Ile mikata ya kusaini mi nakuletea kandamili ww nipe Tanzanite hatuitaki

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani huu unyonyaji dhidi ya Tanzania uanze tu awamu ya tano ???
Mjamaa Nyerere mbona alishirikiana sana na dunia ???
Alikuwa haogopi kunyonywa ???
 
Shida ya viongozi wengi ni Ubinafsi, ujinga na kutokuwa na muono wa miaka mingi ijayo.

UCCM na UCHADEMA pia umeathiri Kwa kiasi kikubwa taifa letu.

Kila kitu kinachukuliwa Kwa Mlengo wa kichama.

Vijana ambao wanatarajiwa hapo baadaye waweze kulinda na kuliendesha taifa hili, kulishauri na kulidhibiti ndio hawa ambao kutwa kuchwa wanaleta UCCM na UCHADEMA.

Ukisema ukweli na kulishauri taifa unaonekana Msaliti, ukiipinga na kuikosoa serikali unaonekana CHADEMA, na adui wa Nchi.

Ukiisifia na kuipongeza SERIKALI Kwa mazuri unaonekana kuwa wewe ni CCM.

Sijui hizi akili-mavi zilizojaa vichwani mwa wengi asili yake ni ipi.


Nchi hii ni nzuri Kama ubinafsi utaondolewa, uchama utaondolewa.
 
Ushirikiano wa kutuletea Symbion na Aggreko na kutukamua na capacity charge halafu wao wanakuletea vyandarua vya msaada gharama zake ni sawa na pesa ya siku moja wanayotukamua kwenye capacity charge.
Sasa hii ndiyo akili niliyokuwa naizungumzia hapa "A Parochial Mindset", yaani unaamini kabisa mahusiano ya Tanzania ni kwenye uwekezaji tu. Hili ndilo lilisababisha TAA YENU izimike ghafla,.....
 
Huwa nawaza sana tulifikaje hapa tulipo leo,

Hivi ilikuwaje taifa lenye wasomi wazuri kabisa likaamua kufanya maamuzi ya kipumbavu ambayo hata Waroma wa kale walioishi miaka 2000 iliyopita wasingeyafanya. Hivi katika maksudi kabisa...
Akili kubwa sana hii umeongea kwa uchungu sana ndio hivyo tena nchi hii imejaa vilaza sana rejea professor wa majalalani
 
Yaani huu unyonyaji dhidi ya Tanzania uanze tu awamu ya tano?
Mjamaa Nyerere mbona alishirikiana sana na dunia?
Alikuwa haogopi kunyonywa?
Hakuna wakumuogopa ila ukweli lazima tuwe makini. Kwani nani ambae hajui kuwa wale watu hawataki nyie mpate? Ukitaka kuwa rafiki mzuri wa nchi za Kimaghalibi linda maslahi yao basi hapo umemaliza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwa nawaza sana tulifikaje hapa tulipo leo,

Hivi ilikuwaje taifa lenye wasomi wazuri kabisa likaamua kufanya maamuzi ya kipumbavu ambayo hata Waroma wa kale walioishi miaka 2000 iliyopita wasingeyafanya. Hivi katika maksudi kabisa...
We jamaa umeandika thread ndeefu na mambo kibao ,ila tu HOJA YAKO KUU IMEJENGWA KATIKA MSINGI WA UWONGO,so this is just rubbish man!!(msisitizo kwa lugha ya kibeberu)
 
Hakuna wakumuogopa ila ukweli lazima tuwe makini. Kwani nani ambae hajui kuwa wale watu hawataki nyie mpate? Ukitaka kuwa rafiki mzuri wa nchi za Kimaghalibi linda maslahi yao basi hapo umemaliza.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nakubaliana kabisa na wewe, lazima tulinde rasilimali zetu kwa WIVU MKUBWA, lakini siyo kutumia ile njia ambayo kipenzi chenu alikuwa anaitumia. Amevuruga mambo na itifikati katika kiwango kikubwa sana,.....
 
Back
Top Bottom