Habari zenu wakuu.. Poleni na majukumu na harakati za hapa na pale, gharama za maisha zinapanda ila tunapanda nazo hakuna kukata tamaa.
Kuna visa kama viwili viliwahi kunitokea back in the days vya kufumaniwa ambavyo sikuwahi kumueleza yeyote.
Cha kwanza kilikuwa hivi.
Kuna mwaka nilipata kazi mkoa fulani kwenye shirika moja lisilo la kiserikali. Ilikuwa ni nje ya mkoa niliokuwa nikiishi awali. Sasa kwenye mtaa niliokuwa nimepanga, kulikuwa na mwanamke mmoja ni kama alitokea kunizimia sana. Hatukuwahi kuwa na mazoea sababu alikuwa ni mke wa mtu, ila ishara za uzinzi zilinijulisha hivyo.
Kuna siku ikatokea pale mtaani kuna sherehe nyumba moja ya mshua fulani, na ndio mwenyekiti wa mtaa huo na ananikubali sana yule mzee, alizoea kuniita mwanaye, nilikuwa sehemu ya wahudhuriaji, yule bidada vilevile. Kutokana na huo mchanganyiko ndio ikawa mwanzo wa kuanzisha mazoea nae na mawasiliano tukabadilishana rasmi.
TUlikuwa tunapigiana simu mara mojamoja ndani ya ile wiki ya kwanza tena majira ya mchana na ilikuwa ni salamu tu na si love affairs ingawa kulikuwa kuna kujikanyaga kimaongezi ambapo haikuhitaji C tatu kujua kunapo jambo hapo.
Siku moja alinipigia simu usiku, nikashtuka kwanza sababu najua kaolewa inakuwaje anipigie muda ambao kwa namna yoyote mumewe anaweza kuwa nyumbani? Nikapokea, tukasalimiana ikabidi nimuulize kwanini apige muda huo akasema mumewe kasafiri. Basi tukaongea sana usiku ule hadi kuhitimisha kuwa tuwe wapenzi ila kwa siri sana. Roho za tamaa na uzuri wa bidada wala sikujali kama jamaa yake anaweza kunifanyia vibaya kama tupo Sodoma siku akija kugundua.
Usiku huohuo bidada akaanza kulazimisha aje kwangu alale, nikamzuia. Akaomba tutoke ikiwezekana ila nikakataa pia sababu ni mwanzo tu isije kuwa anataka kuniharibia tu. Basi tukawa wa kuwasiliana tu, siku kama ya tatu ikawa ndio siku ya kuonana nae rasmi, kwakuwa walikuwa hawajazaa haikuwa shida. Tulionana na niliichakaza vibaya mno. Bibie ana kimwili ka wastani tu, ni slim halafu mimi nimeenda hewani kumzidi kwa hiyo nilikuwa nafanya nnavotaka, iwe nimembebelea au nimembananisha bado iliwezekana, maamuzi yalikuwa kama ya Lowassa tu kuhama chama. Na yeye alidai anapenda kudeka kwenye mwili ulioenda air (hewani) kama wangu.
Basi bwana kadri muda ulivyozidi kusogea nikanogewa, akanogewa pia. Ikawa ndio mchezo wetu kukutana na kumwaga moto. Siku moja yule mzee mwenyekiti aliniita akaniuliza kuhusu mie na yule bidada mke wa mtu, nikashtuka sana kwa sababu sikutegemea kama anaweza kuwa anafahamu, na kajuaje ilhali mimi naamini najua kutunza siri? Mzee alinionya akaniambia acha kabisa mara moja. Nikaitikia kwa kichwa huku nikiwa na hofu pia sababu mambo yashakuwa exposed.
Nikataka kukata mazoea na bidada ila ilikuwa ngumu sababu alichokionja alidai hakuwahi kukipata. Basi nikapumbazwa na maneno ya kudeka nikaona potelea pote, nikaendelea kuburuza, kumbuka muda huo bado mumewe hajaja.
Siku hazikuganda, mumewe akarejea. Tulijitahidi sana kujizuia lakini tabia ikishajijenga ni ngumu sana kuishape... Ikawa ni ngumu hata kukutana tena. Nakumbuka tangu mumewe arudi nilikutana na bibie mara moja nikafanikiwa japo alikuwa rahisi sababu ya ugumu wa kupata nafasi. Ile mara ya pili ndio balaa lilipokujia.
Siku hiyo Bidada alitoka jioni kama saa 11 kwake anaenda nyumbani kwao mara moja. Sasa wakati anarudi ilikuwa mida kama saa tatu kasoro usiku akaomba anione angalau kwa dakika 10 tu sababu ya ufinyu wa nafasi sababu ya uwepo wa mumewe. Nikakubali, tukakutana kachochoro kamoja mbali kidogo na mtaani, huwa hakana jam sana kwa usiku kama ule. Nafsi ni kama ilikuwa inakataa ila kibri cha ubinadamu kiliniongoza. Kumbe ni kama kuna watu walikuwa wanaspy, sijajua waliorganize vipi hadi kujua tutakuwa eneo hilo, na walijuaje na nani aliorganize, I don't know.
Tulipokutana haikuishia story tu, ikabidi kapigwe kamechi ka kuibaiba. Baada ya kumaliza nikaona tochi zimewashwa toka pande moja ya chochoro kutuelekea, watu kama wanne halafu zikasikika sauti za kugadhabika zikisema tulieni hapohapo.. yule bidada nikasikia anasema Mungu wangu, mme wangu huku anajiliza kipumbavu.. aisee nguvu zikaisha nikawaza hata nikikimbia hawa ntawaacha wote kweli? Na hata nikithubutu, wakiniitia mwizi maana yake maisha yanatamatikia hapo. Akili ikawaza haraka sana kwamba leo, ndio ile siku naenda kutatuliwa kama pazia la hekalu.. nikaona noo, ikabidi nichanganye miguu kujinusuru, liwalo na liwe. Bora kufa umepambana kuliko kufa kizembe
Sasa kutokana na uhafifu wa mwanga nikakimbia bila hata kujua naelekea wapi wala ninapokanyaga, kama kona tatu naona njemba zinakuja tu, bahati baya nikaenda kukanyaga shimo la maji taka ya bafu nikateleza na kuanguka mguu ukawa kama umeshtuka.. aisee, nilijaza mtaa. Nilipigwa makofi na zile njemba utadhani zenyewe ndio zenye mke, ila mhusika akawa analia tu kwanini unatembea na mke wangu.. nilibebwa juu juu hadi kwa mwenyekiti. Wahuni hawakujali nimeenda hewani wala nini. Ndio nikaamini kumbe ukifumaniwa hakunaga cha mbavu nene, lazima unywee hata ukiwa kijeba kama Undertaker
Ilikuwa aibu siwafichi.. Kule kwa mwenyekiti baada ya muda tukabaki kama watu nane nahojiwa hapo.. Suala ikawa waende polisi ila mwenyekiti akawa kama ananikingia kifua kwa namna fulani akidai tuyamalize hukuhuku.
Acheni tu aisee.. nililala palepale sababu niliogopa nikienda kulala home naweza kuchomewa ndani au waniijie wanipelekee moto. Asubuhi walikuja wakuu wa pale kazini, ikawa ni vikao tu. Muda huo mguu ulioshtuka umevimba vibaya mno hata kutembea siwezi.. Ilinitoka Milioni 2 na laki tatu jamaa ndio akawa mpole aisee. Akiba karibu yote ikaenda kwenye msala. Na hapo nikawa naona kama bado jamaa ataniendea kwa Sangoma, sababu ni cama alikuwa calm kiaina flani, wasiwasi ukabaki kwangu. Kazini hawakunifukuza, wakanihamishia tu mkoa mwingine.
Baada ya kupata unafuu wa mguu nikamtafuta jamaa nikiwa siamini kama yameisha upande wake, nikamuachia na vitu vyote vya ndani nikaondoka na huo mkoa aisee. Sijajua walimalizaje na mkewe , ila ulipita muda sana nikiwa mkoa mwingine huo bidada akanicheki tena.. nikavunja kabisa ile line ya simu. Tunaonana kwenye social networks tu..
Kwakuwa tumeumbiwa kusahau, nikajichanganya tena kwenye mkasa wa pili..