Ilikuwaje Portugal kwa kiswahili ikaitwa Ureno?

ITEGAMATWI

JF-Expert Member
Jan 26, 2012
5,310
4,040
Wadau huwa najiuliza kila siku bila kupata jawabu!Hv ilikuwaje Portugal ikaitwa Ureno kwa kiswahili jina ambalo haliendani hata kidogo na jinsi wao wenyewe wanavyoiita nchi yao? Nimekuwa nikiangalia mfano wa nchi nyingine zinavoitwa kwa Kiingereza au wao wenyewe nimeona kwa kiasi fulani majina yanashabihiana na sisi tunavyoyaita;Mfano:- England - Uingereza. America - Marekani. Spain - Uhispania. Egypt -(Masr) wenyewe wanavyoiita!Misri kwa kiswahili! etc Hebu naomba mnisaidie wadau hii ilikuwaje? Nawasilisha!!!
 
Una hakika England inashabihiana na Uingereza au America na Marekani...umesema kama wenyewe wanavyojiita unauhakika Wareno wanaita nchi yao Portugal? Portugal ni Kiingereza na wala sio Kireno!
 
Una hakika England inashabihiana na Uingereza au America na Marekani...umesema kama wenyewe wanavyojiita unauhakika Wareno wanaita nchi yao Portugal? Portugal ni Kiingereza na wala sio Kireno!

Mkuu nina uhakika kuwa uingereza inashabihiana na neno england na Marekani na America pia hata wewe unaliona hilo labda kama hutaki tu kukubali!Pia nina uhakika kuwa Portugal hata kwa kireno inaandikwa hivyo kinachotofautiana ni matamshi tu na waingereza!!
 
Jina la "Kingdom of Portugal" katika Kireno ni "Reino de Portugal".

Sasa naona katika translation hapo watu wakachukua "Reino" wakaiswahili ndiyo ikaja kuwa "Ureno".

Ahaaa kumbe!!Akhsante sana mkuu Kiranga kwa ufafanuzi!Kumbe sisi tulichukua neno kingdom badala ya jina la nchi husika ndiyo tukalifanya liwe jina la nchi yenyewe!!
 
hivi jina lako hilo lina uhusiano na wewe?!!!!!

Kama sijakusoma vizuri vile mkuu!!Lakini kama una maana hiyo naweza kujibu kuwa ndiyo maana sisi tuliozaliwa miaka hiyo majina yetu tulikuwa tunapewa kulingana na tukio lililopo wakati huo!!
 
Kama sijakusoma vizuri vile mkuu!!Lakini kama una maana hiyo naweza kujibu kuwa ndiyo maana sisi tuliozaliwa miaka hiyo majina yetu tulikuwa tunapewa kulingana na tukio lililopo wakati huo!!

Lingine najiuliza eti kwa nin mshare wa saa ukiwa kwenye 1 tunasema saa 7.Na 12 tunaita saa 6.Nan kauleta huu ustaarabu kwa nin isiwe 1 iwe saa 1.PUMBAFU MAMBO MENGINE BWANA.
 
Msumbiji (literally Nchumbiji) na Mozambique je? :lol::embarassed2::eyebrows:

Mkuu kwani wamakonde wa msumbiji wanaiitaje nchi yao?sina uhakika lakini nadhani hawawezi sema mozambique kwa kimakonde!Hebu tuwaulize wadau na hilo!!
 
Lingine najiuliza eti kwa nin mshare wa saa ukiwa kwenye 1 tunasema saa 7.Na 12 tunaita saa 6.Nan kauleta huu ustaarabu kwa nin isiwe 1 iwe saa 1.PUMBAFU MAMBO MENGINE BWANA.

Halafu kweli hivi hii ilikuwaje?mbona wanalazimishe kufanya maisha magumu wakati njia fupi ipo?
 
Safi sana mkuu hata mie nilikuwa naperuzi asili ya neno hili. Sasa najua. Thanx
Jina la "Kingdom of Portugal" katika Kireno ni "Reino de Portugal".

Sasa naona katika translation hapo watu wakachukua "Reino" wakaiswahili ndiyo ikaja kuwa "Ureno".
 
Halafu kweli hivi hii ilikuwaje?mbona wanalazimishe kufanya maisha magumu wakati njia fupi ipo?

Lingine najiuliza eti kwa nin mshare wa saa ukiwa kwenye 1 tunasema saa 7.Na 12 tunaita saa 6.Nan kauleta huu ustaarabu kwa nin isiwe 1 iwe saa 1.PUMBAFU MAMBO MENGINE BWANA.

Hii inatikana na wakati gani siku huanza kwa wenzetu. Kwa wao siku mpya huanza saa sita na dakika moja usiku (00:01) kwa hiyo saa moja asubuhi ni masaa saba (7.00 Anti Meridian) tangu siku ianze.

Kwasisi waswahili siku huanza jua linapochomoza, kwahiyo saa moja asubuhi ni lisaa limoja tangu jua lichomoze (saa 12 asubuhi). Tulifanya hivyo kwasababu katika ukanda wa ikweta tuna masaa 12 ya mwanga na 12 ya giza, mwaka mzima. Wenzetu wasinge weza kutumia kigezo cha jua kwakuwa muda wa jua kuchomoza na kuzama hubadilika kutokana na majira
 
Msumbiji (literally Nchumbiji) na Mozambique je? :lol::embarassed2::eyebrows:
Msumbiji limotolewa katika hiyo Mozambique (Moza mbiki = Msu -Mbiji, unatujua tena Waswahili kwa kutohoa. Unajua neno gari linatukana na car?).
Neno lenyewe Mozambique lilipatikana kutokana na mfanyabiashara wa kiarabu Mossa al Bique (Musa Al Big or Mossa Al Bique or Mussa Ben Mbiki). Chungulia kwenye ya jina hilo kwenye Wikipedia sehemu ya Etymology
 
msumbiji limotolewa katika hiyo mozambique (moza mbiki = msu -mbiji, unatujua tena waswahili kwa kutohoa. Unajua neno gari linatukana na car?).
Neno lenyewe mozambique lilipatikana kutokana na mfanyabiashara wa kiarabu mossa al bique (musa al big or mossa al bique or mussa ben mbiki). Chungulia kwenye ya jina hilo kwenye wikipedia sehemu ya etymology

Sahihisho........gari ni neno linalojitegemea na tumekopa kwa wahindi...just like baba
 
Msumbiji limotolewa katika hiyo Mozambique (Moza mbiki = Msu -Mbiji, unatujua tena Waswahili kwa kutohoa. Unajua neno gari linatukana na car?).
Neno lenyewe Mozambique lilipatikana kutokana na mfanyabiashara wa kiarabu Mossa al Bique (Musa Al Big or Mossa Al Bique or Mussa Ben Mbiki). Chungulia kwenye ya jina hilo kwenye Wikipedia sehemu ya Etymology

Akhsante kwa ufafanuzi mkuu!!
 
Back
Top Bottom