Ilikuwa nife jioni hii ya leo!!!

Ilikuwa nife jioni hii ya leo!!!

Mbona unaweweseka kuna sehemu nimekwambia ujitetee kwangu? Usionyeshe umwamba kwa vitu ambavyo huviwezi na kama unavyojinasibu kuwa si muoga usingesimamisha gari ungeendelea na mwendo sasa wewe unafika mbele unasimama halafu unaleta umwamba upo na watoto hizo akili matope? Onyesha uhodari wako ukiwa pekee ako kwenye gari siyo unawaingiza matatizoni watu wengine ambao hata hawakustahili
Sasa huo utetezi wa kijinga nimejitetea kwa nani? Umejiona sasa ulivyo mtupu? Sikuondoka kwa uoga bali niliona itakuwa usumbufu na tatizo lilipokuwa kubwa nililiweka sawa sababu mawe yalikuwa yapo ya kutosha.

Nadhani kama ni wewe ungechukuliwa kama maiti na kuwekwa ndani mpaka sikukuu zikaisha ukapandishwa mahakamani......watoto wa mjini tumeshazoea purukushani za maisha hivyo jifunze ujasiri bwana mdogo.
 
Bahati nzuri mimi huwa siandiki nikiwa tumbo wazi kama wewe,halafu unajiita mtoto wa mjini hapo ndo umedhihiridha kuwa unakua mwili tu ila akili kisoda tena shukuru hao mafundi uliokuwa nao walikuwa wanabusara mana ningekuwa ni mimi ungelazwa hospitali.
Endelea kujiita mtoto wa mjini mana ndo UGOTO wa akili yako ulipokomea..ila jitahidi kuwa mkubwa wa mjini
 
Pole sana mkuu wangu....town hiyo ya kuwatoka jamaa ni kawaida tu ila nadhani ulifanya hivyo muda mbaya na sehemu mbaya kitendo kilichofanya jamaa wajue kuna jambo zaidi haswa kipindi kama hiki, pia nikusifu jinsi ulivyosimama kiume baada ya kuona tatizo limeshakuwa kubwa ukaonyesha ujasiri wa kuyajenga na kueleweka mara moja pamoja na kuwachezesha kwata.

Mwanaume linapotokea tatizo na ukaona limeshakuwa kubwa, lazima usimame imara na kuutua mzigo wa uoga ili yasifike mbali na hivi ndivyo ulivyofanya.....natambua hapo nafasi ya mjadala ilikuwa ndogo lakini ulilicheza hili na hukutafuta baba wala mama.

Wasikutishe humu na maneno ya nyuma ya keyboard ilihali hakuna asiye na makosa, wanaiba wapenzi wa watu, wanavunja ndoa za watu, wanaiba vya watu, wanadhulumu nk lakini wanaogopa kutoa ushuhuda ila wenzao wakieleza ili tujifunze wanaanza kulalamika.

Saluti mkuu
 
Narudia tena usiogope matatizo ukiwa mwanaume, utakuwa na tofauti gani na mwanamke ikiwa unalalamika hivi kama wao? Ingekuwa ni wewe hivi ungeweza kutaja hata jina lako (sembuse kujenga hoja) mbele ya sub machine gun pamoja Ak 47? Hivi kijana hata shilingi elfu hamsini umeshawahi kuipata kwa nguvu yako? Maana sije ikawa namaliza bando na wale wanaosubiri ajira huku mashamba yamejaa.
 
Akhsante mkuu na wewe hata ungekuja kumposa mwanangu ningekuozesha bure maana una akili ya kiume kuliko kulaumu laumu kama ilivyo desturi ya watoto wa mama.
Hapa najiandaa kwenda tena huko ili nikaangalie usalama wa ujenzi ingawa nitatumia chombo nyingine na ile nitaipeleka gereji mafundi wakajiridhishe kwanza.
 
Narudia tena usiogope matatizo ukiwa mwanaume, utakuwa na tofauti gani na mwanamke ikiwa unalalamika hivi kama wao? Ingekuwa ni wewe hivi ungeweza kutaja hata jina lako (sembuse kujenga hoja) mbele ya sub machine gun pamoja Ak 47? Hivi kijana hata shilingi elfu hamsini umeshawahi kuipata kwa nguvu yako? Maana sije ikawa namaliza bando na wale wanaosubiri ajira huku mashamba yamejaa.
Ni rahisi kuniita kijana kwa vile hunifahamu na yawezekana nikawa sawa na baba yako au kaka yako..ndomana nasema tena nakuona mjinga kuna vitu vya kuonyesha umwamba siyo hicho ulichokifanya na kujiona mjanja wa mjini huku ukiandika kwa mbwembwe..yawezekana lengo lako kuu la kuandika huu uzi ni usifiwe kwa kuendesha gari kwa spidi ukiwa unakimbizwa na polisi kwa kudhani labda JF ni wewe pekee mwenye gari ila wengine hawana.
Pili baba yeyote mwenye mtoto/watoto kama mimi siwezi kubali hatarisha maisha ya watoto wangu kwa ujinga na inakupasa utambue unawajengea picha gani kama mzazi lakini kwako unafamilia ya watoto wawili halafu unaona umefanya kitendo cha maana napata wasiwasi labda hao watoto unaowasema wako huna uchungu nao
 
Pole sana mkuu. Umetupa somo zuri sisi wengine.
Akhsante sana mkuu wangu nashukuru na sikutaka kuongeza neno wala kupunguza neno ili iwe funzo kwa wengine.
 
Pole sana mkuu wangu....town hiyo ya kuwatoka jamaa ni kawaida tu ila nadhani ulifanya hivyo muda mbaya na sehemu mbaya kitendo kilichofanya jamaa wajue kuna jambo zaidi haswa kipindi kama hiki, pia nikusifu jinsi ulivyosimama kiume baada ya kuona tatizo limeshakuwa kubwa ukaonyesha ujasiri wa kuyajenga na kueleweka mara moja pamoja na kuwachezesha kwata.

Mwanaume linapotokea tatizo na ukaona limeshakuwa kubwa, lazima usimame imara na kuutua mzigo wa uoga ili yasifike mbali na hivi ndivyo ulivyofanya.....natambua hapo nafasi ya mjadala ilikuwa ndogo lakini ulilicheza hili na hukutafuta baba wala mama.

Wasikutishe humu na maneno ya nyuma ya keyboard ilihali hakuna asiye na makosa, wanaiba wapenzi wa watu, wanavunja ndoa za watu, wanaiba vya watu, wanadhulumu nk lakini wanaogopa kutoa ushuhuda ila wenzao wakieleza ili tujifunze wanaanza kulalamika.

Saluti mkuu
Endelea kumdanganya mwenzio,kuna vitu vingine unaweza kujiona shujaa kumbe unajimaliza mwenyewe
 
Ni rahisi kuniita kijana kwa vile hunifahamu na yawezekana nikawa sawa na baba yako au kaka yako..ndomana nasema tena nakuona mjinga kuna vitu vya kuonyesha umwamba siyo hicho ulichokifanya na kujiona mjanja wa mjini huku ukiandika kwa mbwembwe..yawezekana lengo lako kuu la kuandika huu uzi ni usifiwe kwa kuendesha gari kwa spidi ukiwa unakimbizwa na polisi kwa kudhani labda JF ni wewe pekee mwenye gari ila wengine hawana.
Pili baba yeyote mwenye mtoto/watoto kama mimi siwezi kubali hatarisha maisha ya watoto wangu kwa ujinga na inakupasa utambue unawajengea picha gani kama mzazi lakini kwako unafamilia ya watoto wawili halafu unaona umefanya kitendo cha maana napata wasiwasi labda hao watoto unaowasema wako huna uchungu nao
Soma tena halafu uelewe kwanza maana ni wengi wametoa mtazamo wao kwa namna walivyotaka na sikupingana nao, hivyo jiulize una nini kichwani mwako? Ukishindwa hivyo soma tu hata kichwa cha habari unaweza pia kujua mada imeelemea wapi! Hakuna nilipojisifu wala kulaumu zaidi ya kuonyesha kujutia haswa mwishoni mwa uzi wangu....umeona sasa? Je bado nikuone una akili kwa kuzidi kuniandama? Kama wewe ni mzee basi niseme tu kama Taifa lina wazee wa aina yako basi ndiyo mliotufikisha hapa kwa woga wenu wa kuogopa Mamlaka kupita kiasi.
 
Endelea kumdanganya mwenzio,kuna vitu vingine unaweza kujiona shujaa kumbe unajimaliza mwenyewe
Hajakataa iwapo kafanya kosa na amesema wazi kama ameleta kama funzo, sasa unataka nimwandame kama tunasutana? Muhimu ni kuangalia aliyamalizaje na usimuandame mtu kama kakuchangisha mchango au ameomba ukamchukulie dhamana.
 
Una haki ya kucheka maana halijakukuta.....ila nashukuru nalala nyumbani badala ya korokoroni japo nimeshaanza kuhisi homa kwa mbali.

Am sorry bana... ndio maana nikasema usichukie.. i know umepata matatizo, ila nilicheka sana, sbb nikasema atleast umejifunza polisi ni nani.. siku nyingine huwezi rudia.. jikaze sasa kiuanaume, maisha yanaendelea, stop thinking of the past, coz past has nothing to do with today and the future
 
Maajabu dereva kushauriwa na fundi madirisha kuhusu sheria na maadili barabarani
 
Maajabu dereva kushauriwa na fundi madirisha kuhusu sheria na maadili barabarani
Ni jambo linapotaka kukukuta tu na ndiyo maana sikumlaumu yeyote zaidi ya kujutia makosa yangu ili wengine wajifunze maana ya utii wa sheria.
Pia nimewasifu wanausalama wetu kwa namna wanavyouza roho kutulinda raia wao, kwangu ilikuwa kama sehemu ya kujifunza.
 
Upuuzi na uongo. Yani leseni tu ndo ukimbie polisi? Watu wenyewe wameruhusiwa kuchukua buku 5 za kufuta vumbi? UONGO ULIOPITILIZA
 
Kutokana na sikukuu iliyo mbele yetu ya Eid el haji, nilifunga safari kuelekea Tanga ambapo ndiyo chimbuko la ukoo wangu.

Nilifika salama salmini na kwa kuwa niliwahi kuanza ujenzi siku za nyuma huko maeneo ya Mabokweni (mji ulio mbele ya Amboni na ni halmashauri ya Jiji la Tanga) nikaona nichukue nafasi hii nikamalizie kabisa kwa kuweka madirisha na milango ili nimweke japo mtu akae kwa kuwa sina malengo ya kuishi huko kwa sasa.

Kazi imeanza jana na leo ilikuwa ni siku ya kumaliza shughuli hiyo hivyo niliondoka na mafundi wangu asubuhi na kuelekea kwenye ujenzi, ilipofika jioni kama saa kumi na mbili na nusu kazi ikawa imekwisha hivyo tukaanza safari ya kurudi.

Nilikuwa na gari aina ya Carina nikiendesha huku ndani nikiwa mimi , mtoto wa kiume wa dada yangu wa miaka kama 21, mwanangu wa kiume wa miaka minne pamoja na mafundi watatu.

Ilikuwa ni safari yenye maongezi na furaha huku kukiwa na mziki mzito kutoka katika gari na nikiendesha kwa mwendo wa taratibu tu, ila kufika maeneo ya Mikocheni (karibu na amboni) nikasimamishwa na askari mmoja aliyesimama katikati ya barabara huku pembeni kuna gari ya polisi aina ya Land rover.

Nilianza kusimama lakini nikakumbuka leseni yangu imekwisha muda mrefu hivyo baada ya kujadiliana na wenzangu wakanipa moyo kuwa TEMBEA.

Nikaondoka taratibu ila kufika mbele kidogo nikagundua lile Land Rover linakuja kwa kasi kunifuata, hapa nikajikuta akili haipo na wenzangu wamechanganyikiwa pia hivyo nikaongeza speed zaidi na kujikuta kila ninavyotembea lakini ile gari bado naiona hali iliyopelekea kuitembeza gari kwa speed ya kutisha na bado nikihisi haitembei.

Hali ilikuwa ya kutisha maana pamoja na kuwa barabarani miaka mingi lakini hapa nilinusa harufu ya kufa (wanaoijua njia hiyo wanatambua vema namna ilivyo), hata hivyo tukashauriana na kuona ni bora niingie njia ya mtaani na mpaka hapo jamaa niliwaacha mbali sana lakini cha ajabu nilipoingia njia hiyo tu kwa kuwa kulikuwa na taa taa nikawaona wakiwa nao wanakuja kwa kasi na nusura wagonge watu watatu! Kwa kuwa njia ile ilikuwa mbaya sana na mashimo makubwa niona nizunguke na kuingia tena kwenye lami na nikanyooka tena, ni hofu kubwa niliyonayo na haswa ukizingatia nilijua hayatakuwa hayo yote hivyo nikajikuta sina ujasiri haswa kwa hofu ya kuiangusha gari maana speed ilishanipa wasiwasi.

Ghafla nikawaona jamaa wakiwa karibu kabisa na hapo nikaamua mwenyewe nipaki pembeni na wao wakapaki kwa mbele yetu na kuruka kwa kasi na kuivamia gari yetu huku wakiwa kama nane na bunduki mkononi.

Tukapigwa sana na kubebwa juu juu na kupakizwa katika bodi la gari yao huku kipigo cha bakora, makofi na virungu vikiendelea, wakasema nimewasumbua sana na kufika pale walishakoki bunduki ili kutushambulia iwe ni matairi au hata sisi......wakasema kwamba moja kwa moja walihisi sisi ni magaidi toka mapangoni na kuniadhibu sana huku wakiniuliza kwa nini nikimbie wakati najua wazi hali ilivyo hapa Tanga hivyo tungekufa kwa uzembe! Pia wakanilaumu kwa wao kuwakosa kosa watu kuwagonga,

Wenzangu wakaendelea kupigwa huku wamelala kwenye bodi na mimi nikatolewa nje chini ya ulinzi na kuambiwa niiwashe gari yangu maana niliizima na kuiwasha inataka maujanja maana switch haifanyi kazi, nikaiwasha na wakaiendesha wao na mimi nikapakizwa mbele katika gari la polisi.

Hatua kadhaa mbele tukakutana na gari nyingine mbili za polisi zikitoka Tanga mjini na tukasimama, kumbe mawasiliano yalifanyika wakati nawatoka polisi hivyo hawa walikuja kuniwekea target.

Hapo gari ikafunguliwa buti na kuanza kuipekua wakakuta tu kigunia kidogo cha mkaa na vifaa vya mafundi, hawakuridhika mkaa wakaumwaga wote kujiridhisha, wakachukua spare tyre na kuitoa upepo ili kujiridhisha na pia wakaipekua gari yote kila mahali lakini hawajakuta chochote kibaya.

Wakasema wao wanakuwa doria kwa sababu ya hali ya usalama eneo lile na pia kuzuia mirungi toka Kenya.

Nilijikaza kiume kwa kuona 'nimeshayakanyaga' na kuomba tuyajenge ila ilikuwa mbinde maana walishakuwa si chini ya thelathini wanawake kwa wanaume maana wengine walikuja kwa gari ndogo aina ya Mark x.......muda wote huo mwanangu alikuwa akilia sana kuona babaake nikila makofi hali iliyopelekea askari wa kike kupatwa na huruma na kukaribisha mazungumzo.

Niliyamaliza ki utu uzima na tukapewa gari yetu na kuendelea na safari japo wenzangu kule kumbe walichezea virungu zaidi.

Najiuliza iwapo ningeitia gari darajani kwa mwendo ule pengine tungekuwa chumba cha maiti sasa......najiuliza iwapo wangemimina risasi kwa mimi kukaidi agizo lao la kusimama, saa hizi tungekuwa chumba cha maiti......najiuliza kwa nini nisinge simama pale pale tu!
Japo hapa nilipo masikio bado yana mwangwi kwa sababu ya makofi mazito ya mfululizo na magoti yanawaka moto kwa virungu lakini bado naona yangekuwa makubwa zaidi hivyo nimejifunza mengi na namshukuru Mungu kwa yote.

KWELI KUZALIWA SIKU MOJA NA KUFA SIKU MOJA.
Ni ujinga mkubwa kuwakimbia polisi wa doria.
Ungeweza kupigwa risasi na wangesema tu mtuhumiwa wa ugsidi ameuwawa.
 
Back
Top Bottom