Ilikuwa nife jioni hii ya leo!!!

Ilikuwa nife jioni hii ya leo!!!

Ungekufa 2 ndo akili ingekukaa
Kufa kupo tu hata ukajifungie kwenye nyumba ya ibada ujue zikitimia utakufa hivyo usiweke sana mbele kudhani kuna ambae hatakufa.
 
Hayo ni matokeo ya ujuaji na ubishi kwa vyombo vya dola, Makofi uliyopata mbele ya mtoto hatasahau, atakukumbusha daima Baba siku ile ... Pole kwa maumivu.
 
Ee bwana ee! mdigo gani muoga wa polisi hivi 😀?! Unakimbia kwa kutokua na leseni tu na una mtoto mdogo ndani? Sasa mlima ule wa amboni ungeshukaje kwa spidi kali hivyo na chini kuna daraja tena chini yake mto wenye maji na pengine mamba na njia nyembamba! kungekua na magari mengine upande wa pili? Duuh. Hatari sana ulifanya. Hata hivyo pole ndugu.
Japo sio mdigo bali nilinunua tu viwanja kule, lakini bado napokea pole yako na pia nakubali kuwa unayajua vema maeneo yale.
 
Wenzako kabla ya kuosha tunaangaliaga wamepack pembeni au la..kama wako watupu unaosha tu kama wapo na gari unaandaa mkono au msimbazi[emoji23]..pole sana
 
..udaresalamu mafi ungekuua b.w.e.g.e wewe!
..sasa mwezi mzima uwe unampa shikamoo huyo mwanao;na ale kuku!utajenga mwakani!
....kaidi tena na hili
Matusi kwangu ni kama chakula tu mkuu maana nimepitia gereji na kutukanana ndiyo kama kuitana, jiulize jambo hili hufanya wangapi na pia ujipe jibu kuwa hii ni funzo kwao.
 
Usirudie tena kuwakimbia askari kwani kufanya hivyo unaweza kusababisha mengine kabisa (kama yaliyokukuta). Ungeweza hata kugonga mtu/watu, mnyama au ajali ya kipuuzi ukapata hasara kubwa. Simama umalizane nao tu. Wengi wa askari wetu (kama walivyo Watanzania wengi) usipowaprovoke wako poa sana tu, hata ungekua na makosa mia wanaweza kukuachia. Labda uwaonyeshe dharau, kiburi, ubabe, nk.

Nimekua nikitumia gari bovu sana labda kuliko yote Moshi mjini miaka ya 2000 hadi nikafahamiana na askari ila sijawahi hata siku moja kuwakimbia askari. Wengi wako friendly kama utajishusha, kuwaheshimu na mara chache kuwatoa (posho ya kubrashia viatu)
Nashukuru kwa kunipa maneno ya busara na nitayafuata maana busara hujenga.
 
Uzi wako umetoa elim kwa watu wenye rabia za kuwakimbia askari.
Nilishawahi kuona huo mchezo bagamoyo kipindi cha nyuma kidogo enzi za TZR au black mamba(wale wa dar es salaam watanielewa)
Jamaa kapigwa mkono na traffic akawakimbia,kilichotokea ikaingia deffender barabarani ikaanza kuranda nae jamaa akaws anawazunfusha mtaani tu bagamoyo.
Wakat wanazungushana kumbe askar wanawasiliana na wenzao ,baada ya muda jamaa akajikuta amekuwa blocked.
Kilichotokea hapo ni historia
Waliodhani Tanzania nzima jambo hili ni mimi tu na kunidhihaki, wapate darasa hili na wengine wajifunze.
 
Kutokea tukio kama hili ni mara ya kwanza kabisa.....kumbuka mkuu ndege mjanja hunaswa na tundu bovu.
Mkuu wangu mi yote hayo 9; mi bado akili yangu ipo kwa mtoto tu matokeo yangu akili imegoma kusikia la mnadi sala msikitini wala la mpiga kengele kanisanii!! Yaani kama isingekuwa mtoto... hii kwangu ingekuwa ni one of the best road adventure! Ingawaje mimi mwenyewe sifahamu uchungu wa mtoto kv sinae lakini nikiona mtu anacheza na maisha ya mtoto; nakuaga mkali sana... dada zangu wenyewe wananijua! Si unajua wanawake wanavyopenda kupiga watoto?! Hawawezi kufanya ushenzi kama huo mbele yangu hata siku moja.
 
Kutokana na sikukuu iliyo mbele yetu ya Eid el haji, nilifunga safari kuelekea Tanga ambapo ndiyo chimbuko la ukoo wangu.

Nilifika salama salmini na kwa kuwa niliwahi kuanza ujenzi siku za nyuma huko maeneo ya Mabokweni (mji ulio mbele ya Amboni na ni halmashauri ya Jiji la Tanga) nikaona nichukue nafasi hii nikamalizie kabisa kwa kuweka madirisha na milango ili nimweke japo mtu akae kwa kuwa sina malengo ya kuishi huko kwa sasa.

Kazi imeanza jana na leo ilikuwa ni siku ya kumaliza shughuli hiyo hivyo niliondoka na mafundi wangu asubuhi na kuelekea kwenye ujenzi, ilipofika jioni kama saa kumi na mbili na nusu kazi ikawa imekwisha hivyo tukaanza safari ya kurudi.

Nilikuwa na gari aina ya Carina nikiendesha huku ndani nikiwa mimi , mtoto wa kiume wa dada yangu wa miaka kama 21, mwanangu wa kiume wa miaka minne pamoja na mafundi watatu.

Ilikuwa ni safari yenye maongezi na furaha huku kukiwa na mziki mzito kutoka katika gari na nikiendesha kwa mwendo wa taratibu tu, ila kufika maeneo ya Mikocheni (karibu na amboni) nikasimamishwa na askari mmoja aliyesimama katikati ya barabara huku pembeni kuna gari ya polisi aina ya Land rover.

Nilianza kusimama lakini nikakumbuka leseni yangu imekwisha muda mrefu hivyo baada ya kujadiliana na wenzangu wakanipa moyo kuwa TEMBEA.

Nikaondoka taratibu ila kufika mbele kidogo nikagundua lile Land Rover linakuja kwa kasi kunifuata, hapa nikajikuta akili haipo na wenzangu wamechanganyikiwa pia hivyo nikaongeza speed zaidi na kujikuta kila ninavyotembea lakini ile gari bado naiona hali iliyopelekea kuitembeza gari kwa speed ya kutisha na bado nikihisi haitembei.

Hali ilikuwa ya kutisha maana pamoja na kuwa barabarani miaka mingi lakini hapa nilinusa harufu ya kufa (wanaoijua njia hiyo wanatambua vema namna ilivyo), hata hivyo tukashauriana na kuona ni bora niingie njia ya mtaani na mpaka hapo jamaa niliwaacha mbali sana lakini cha ajabu nilipoingia njia hiyo tu kwa kuwa kulikuwa na taa taa nikawaona wakiwa nao wanakuja kwa kasi na nusura wagonge watu watatu! Kwa kuwa njia ile ilikuwa mbaya sana na mashimo makubwa niona nizunguke na kuingia tena kwenye lami na nikanyooka tena, ni hofu kubwa niliyonayo na haswa ukizingatia nilijua hayatakuwa hayo yote hivyo nikajikuta sina ujasiri haswa kwa hofu ya kuiangusha gari maana speed ilishanipa wasiwasi.

Ghafla nikawaona jamaa wakiwa karibu kabisa na hapo nikaamua mwenyewe nipaki pembeni na wao wakapaki kwa mbele yetu na kuruka kwa kasi na kuivamia gari yetu huku wakiwa kama nane na bunduki mkononi.

Tukapigwa sana na kubebwa juu juu na kupakizwa katika bodi la gari yao huku kipigo cha bakora, makofi na virungu vikiendelea, wakasema nimewasumbua sana na kufika pale walishakoki bunduki ili kutushambulia iwe ni matairi au hata sisi......wakasema kwamba moja kwa moja walihisi sisi ni magaidi toka mapangoni na kuniadhibu sana huku wakiniuliza kwa nini nikimbie wakati najua wazi hali ilivyo hapa Tanga hivyo tungekufa kwa uzembe! Pia wakanilaumu kwa wao kuwakosa kosa watu kuwagonga,

Wenzangu wakaendelea kupigwa huku wamelala kwenye bodi na mimi nikatolewa nje chini ya ulinzi na kuambiwa niiwashe gari yangu maana niliizima na kuiwasha inataka maujanja maana switch haifanyi kazi, nikaiwasha na wakaiendesha wao na mimi nikapakizwa mbele katika gari la polisi.

Hatua kadhaa mbele tukakutana na gari nyingine mbili za polisi zikitoka Tanga mjini na tukasimama, kumbe mawasiliano yalifanyika wakati nawatoka polisi hivyo hawa walikuja kuniwekea target.

Hapo gari ikafunguliwa buti na kuanza kuipekua wakakuta tu kigunia kidogo cha mkaa na vifaa vya mafundi, hawakuridhika mkaa wakaumwaga wote kujiridhisha, wakachukua speak tyre na kuitoa upepo ili kujiridhisha na pia wakaipekua gari yote kila mahali lakini hawajakuta chochote kibaya.

Wakasema wao wanakuwa doria kwa sababu ya hali ya usalama eneo lile na pia kuzuia mirungi toka Kenya.

Nilijikaza kiume kwa kuona 'nimeshayakanyaga' na kuomba tuyajenge ila ilikuwa mbinde maana walishakuwa si chini ya thelathini wanawake kwa wanaume maana wengine walikuja kwa gari ndogo aina ya Mark x.......muda wote huo mwanangu alikuwa akilia sana kuona babaake nikila makofi hali iliyopelekea askari wa kike kupatwa na huruma na kukaribisha mazungumzo.

Niliyamaliza ki utu uzima na tukapewa gari yetu na kuendelea na safari japo wenzangu kule kumbe walichezea virungu zaidi.

Najiuliza iwapo ningeitia gari darajani kwa mwendo ule pengine tungekuwa chumba cha maiti sasa......najiuliza iwapo wangemimina risasi kwa mimi kukaidi agizo lao la kusimama, saa hizi tungekuwa chumba cha maiti......najiuliza kwa nini nisinge simama pale pale tu!
Japo hapa nilipo masikio bado yana mwangwi kwa sababu ya makofi mazito ya mfululizo na magoti yanawaka moto kwa virungu lakini bado naona yangekuwa makubwa zaidi hivyo nimejifunza mengi na namshukuru Mungu kwa yote.

KWELI KUZALIWA SIKU MOJA NA KUFA SIKU MOJA.
Pole sana,nadhani umeshajifunza.Ujuaji hausaidii sana.Nenda uka-renew leseni yako,mbona sio hela nyingi.
 
Hayo ni matokeo ya ujuaji na ubishi kwa vyombo vya dola, Makofi uliyopata mbele ya mtoto hatasahau, atakukumbusha daima Baba siku ile ... Pole kwa maumivu.
Akhsante japo makofi kwangu ilikuwa ni kitu kidogo, nafikiria zaidi iwapo wangenishuti, kulala ndani, kufunguliwa kesi au hata kupata ajali.
 
Pambavu, umeona binduki unataka kujiua je? Utaenda kuandamana wewe?
Ukisoma vizuri utagundua nilipokuwa naondoka hakukuwa na bunduki wala askari wengi zaidi ya alie nisimamisha.
 
Wenzako kabla ya kuosha tunaangaliaga wamepack pembeni au la..kama wako watupu unaosha tu kama wapo na gari unaandaa mkono au msimbazi[emoji23]..pole sana
Nashukuru wazee wa rodi mmejitokeza na kuonyesha uma kuwa hivyo ni vitu ambavyo vipo ila tu imetokea misteki na mbuzi kafia kwa muuza supu.
 
Mkuu wangu mi yote hayo 9; mi bado akili yangu ipo kwa mtoto tu matokeo yangu akili imegoma kusikia la mnadi sala msikitini wala la mpiga kengele kanisanii!! Yaani kama isingekuwa mtoto... hii kwangu ingekuwa ni one of the best road adventure! Ingawaje mimi mwenyewe sifahamu uchungu wa mtoto kv sinae lakini nikiona mtu anacheza na maisha ya mtoto; nakuaga mkali sana... dada zangu wenyewe wananijua! Si unajua wanawake wanavyopenda kupiga watoto?! Hawawezi kufanya ushenzi kama huo mbele yangu hata siku moja.
Ilianza kama mzaha na baadae ukaja moyo wa matumaini....nikajikuta maji nimeyavulia nguo bila kupenda.
 
Back
Top Bottom