Ilikuwa nife jioni hii ya leo!!!

Ilikuwa nife jioni hii ya leo!!!

Na haswa hilo ndiyo lengo langu watu wajihadhari.....nimekuwa tofauti na wale wanaopost mambo mazuri tu yanayo wakuta na mabaya kuyaficha.

Hakika kama jamii ingesimama katika ukweli tungejenga taifa imara, changudoa angejitokeza na kueleza majuto yake, mwizi angejitokeza na kueleza majuto yake, aliathirika angejitokeza na kueleza hali ilivyokuwa na watu wangejifunza hakika......ila kwa bahati mbaya wanaogopa kukashifiwa na kuvunjwa moyo na uzao huu wa sasa na mwisho wake jamii haijifunzi na makosa waliyotenda wao au mapito yanarudiwa kila leo na kupoteza nguvu kazi ya Taifa.
Mkuu ulichokifanya ni jambo jema sana,kumjali hata yule usiyemjua ni zaidi ya upendo,dunia haitaisha watu wema.
 
Upo sahihi mkuu hao walikuwa na subira kwa vile waliona na mtoto yupo ndani.
Nina uhakika wakat wanamsimamisha walimuona na mtoto ndani na ndio maana hawakuwachakaza kwa risasi.
Kimsingi mleta mada popote utakapokuwa tambua mtoto kaokoa maisha yako na yenu wote,kama anavyosema mleta mada kuna askari wengine walokuja na private cars na walikuwa zaid ya 30 tafsir yake ni kuwa walijua ni magaidi au majambazi ila mtoto ndio aliwafanya wasichukue maamuzi mengine.
Dah!! Halafu unajua wewe ndo unanifungua akili hivi sasa?! Nakubaliana na wewe... walimuona mtoto na ndo ilikuwa salama yao vinginevyo hii thread isingekuwepo na ingekuwepo nyingine kabisa toka kwa mwandishi mwingine kabisa ikisema "POLISI TANGA WAUA RAIA WASIO NA HATIA...!" Kumbe ni raia wenyewe ndo wamesababisha!
 
Nami pia nimeliona hilo mkuu.....na imekuwa ni kama history katika maisha yangu.
Ila pole mkuu, ukisimamishwa na polisi , hata kama una kosa la kibinadamu ukieleza watakuelewa tu, maana hata wao ni binadamu.
Ila ukisepa, wooooi, inabidi watumie nguvu ya ziada kukuweka chini ya ulinzi, na katika process atatokea kijana ambaye atakupiga risasi kwa bahati mbaya.
Kwao inabidi wateteane kuwa ulikuwa unakimbia amri halali ya kujisalimisha, na utapewa kila aina ya ubaya kuhalalisha kuuwawa kwako.
 
Kutokana na sikukuu iliyo mbele yetu ya Eid el haji, nilifunga safari kuelekea Tanga ambapo ndiyo chimbuko la ukoo wangu.

Nilifika salama salmini na kwa kuwa niliwahi kuanza ujenzi siku za nyuma huko maeneo ya Mabokweni (mji ulio mbele ya Amboni na ni halmashauri ya Jiji la Tanga) nikaona nichukue nafasi hii nikamalizie kabisa kwa kuweka madirisha na milango ili nimweke japo mtu akae kwa kuwa sina malengo ya kuishi huko kwa sasa.

Kazi imeanza jana na leo ilikuwa ni siku ya kumaliza shughuli hiyo hivyo niliondoka na mafundi wangu asubuhi na kuelekea kwenye ujenzi, ilipofika jioni kama saa kumi na mbili na nusu kazi ikawa imekwisha hivyo tukaanza safari ya kurudi.

Nilikuwa na gari aina ya Carina nikiendesha huku ndani nikiwa mimi , mtoto wa kiume wa dada yangu wa miaka kama 21, mwanangu wa kiume wa miaka minne pamoja na mafundi watatu.

Ilikuwa ni safari yenye maongezi na furaha huku kukiwa na mziki mzito kutoka katika gari na nikiendesha kwa mwendo wa taratibu tu, ila kufika maeneo ya Mikocheni (karibu na amboni) nikasimamishwa na askari mmoja aliyesimama katikati ya barabara huku pembeni kuna gari ya polisi aina ya Land rover.

Nilianza kusimama lakini nikakumbuka leseni yangu imekwisha muda mrefu hivyo baada ya kujadiliana na wenzangu wakanipa moyo kuwa TEMBEA.

Nikaondoka taratibu ila kufika mbele kidogo nikagundua lile Land Rover linakuja kwa kasi kunifuata, hapa nikajikuta akili haipo na wenzangu wamechanganyikiwa pia hivyo nikaongeza speed zaidi na kujikuta kila ninavyotembea lakini ile gari bado naiona hali iliyopelekea kuitembeza gari kwa speed ya kutisha na bado nikihisi haitembei.

Hali ilikuwa ya kutisha maana pamoja na kuwa barabarani miaka mingi lakini hapa nilinusa harufu ya kufa (wanaoijua njia hiyo wanatambua vema namna ilivyo), hata hivyo tukashauriana na kuona ni bora niingie njia ya mtaani na mpaka hapo jamaa niliwaacha mbali sana lakini cha ajabu nilipoingia njia hiyo tu kwa kuwa kulikuwa na taa taa nikawaona wakiwa nao wanakuja kwa kasi na nusura wagonge watu watatu! Kwa kuwa njia ile ilikuwa mbaya sana na mashimo makubwa niona nizunguke na kuingia tena kwenye lami na nikanyooka tena, ni hofu kubwa niliyonayo na haswa ukizingatia nilijua hayatakuwa hayo yote hivyo nikajikuta sina ujasiri haswa kwa hofu ya kuiangusha gari maana speed ilishanipa wasiwasi.

Ghafla nikawaona jamaa wakiwa karibu kabisa na hapo nikaamua mwenyewe nipaki pembeni na wao wakapaki kwa mbele yetu na kuruka kwa kasi na kuivamia gari yetu huku wakiwa kama nane na bunduki mkononi.

Tukapigwa sana na kubebwa juu juu na kupakizwa katika bodi la gari yao huku kipigo cha bakora, makofi na virungu vikiendelea, wakasema nimewasumbua sana na kufika pale walishakoki bunduki ili kutushambulia iwe ni matairi au hata sisi......wakasema kwamba moja kwa moja walihisi sisi ni magaidi toka mapangoni na kuniadhibu sana huku wakiniuliza kwa nini nikimbie wakati najua wazi hali ilivyo hapa Tanga hivyo tungekufa kwa uzembe! Pia wakanilaumu kwa wao kuwakosa kosa watu kuwagonga,

Wenzangu wakaendelea kupigwa huku wamelala kwenye bodi na mimi nikatolewa nje chini ya ulinzi na kuambiwa niiwashe gari yangu maana niliizima na kuiwasha inataka maujanja maana switch haifanyi kazi, nikaiwasha na wakaiendesha wao na mimi nikapakizwa mbele katika gari la polisi.

Hatua kadhaa mbele tukakutana na gari nyingine mbili za polisi zikitoka Tanga mjini na tukasimama, kumbe mawasiliano yalifanyika wakati nawatoka polisi hivyo hawa walikuja kuniwekea target.

Hapo gari ikafunguliwa buti na kuanza kuipekua wakakuta tu kigunia kidogo cha mkaa na vifaa vya mafundi, hawakuridhika mkaa wakaumwaga wote kujiridhisha, wakachukua spare tyre na kuitoa upepo ili kujiridhisha na pia wakaipekua gari yote kila mahali lakini hawajakuta chochote kibaya.

Wakasema wao wanakuwa doria kwa sababu ya hali ya usalama eneo lile na pia kuzuia mirungi toka Kenya.

Nilijikaza kiume kwa kuona 'nimeshayakanyaga' na kuomba tuyajenge ila ilikuwa mbinde maana walishakuwa si chini ya thelathini wanawake kwa wanaume maana wengine walikuja kwa gari ndogo aina ya Mark x.......muda wote huo mwanangu alikuwa akilia sana kuona babaake nikila makofi hali iliyopelekea askari wa kike kupatwa na huruma na kukaribisha mazungumzo.

Niliyamaliza ki utu uzima na tukapewa gari yetu na kuendelea na safari japo wenzangu kule kumbe walichezea virungu zaidi.

Najiuliza iwapo ningeitia gari darajani kwa mwendo ule pengine tungekuwa chumba cha maiti sasa......najiuliza iwapo wangemimina risasi kwa mimi kukaidi agizo lao la kusimama, saa hizi tungekuwa chumba cha maiti......najiuliza kwa nini nisinge simama pale pale tu!
Japo hapa nilipo masikio bado yana mwangwi kwa sababu ya makofi mazito ya mfululizo na magoti yanawaka moto kwa virungu lakini bado naona yangekuwa makubwa zaidi hivyo nimejifunza mengi na namshukuru Mungu kwa yote.

KWELI KUZALIWA SIKU MOJA NA KUFA SIKU MOJA.
Mkuu kwanza pole kwa kibano ulichopokea kutoka kwa chombo cha dola, Pia mshukuru huyo mwanao kwa kufanya maelezo yako yaeleweke kwa kupitia kilio chake. Mie hapo naona ulikosea sana kuna vitu unatakiwa ujiongeze mwenyewe kabla hujakutwa na majanga mimi sikuona sababu ya wewe kuwakimbia hao walinzi wetu wa amani. Ukweli ungekuweka kando na maswhibu yalokupata pia wewe kama baba unapopata tatizo ndiyo sehemu yakuonesha ukomavu yaani umeonesha kutojiamini kwako mbele ya Mwanao, Mjomba - Mtoto wa dada yako na hao mafundi wako.. Wewe umesema unatoka Dar sasa hiyo Gari yako huwa unaendesha kwa namna gani wakati haina vibali muhimu na huku ndiyo kuna Polisi wengi barabarani? Pia umewadhalilisha wanaume wa DAR kwa kukimbia Police. Siku nyingine hutapata muda wa kuja kushusha Uzi Maana utakuwa mgeni wa kuzimu. Kitu cha muhimu huna budi kufahamu kuwa Jeshi la Polisi lipo kwenye Changamoto za ulinzi na usalama Matukio kama ya Vikundi, Amboni, Mwanza, Mkuranga, Morogoro na Rufiji ni vitu vinavyolilfanya kuwa katika hali kama hiyo... Kwanza ulitakiwa uwapeleke Kituo cha mafuta ili ujazie mafuta magari yao yote yaliyotumika kwenye sekeseke ili liwe fundisho kwa wenzako wenye akili kama zako... Kachukue PF3 ukapate matibabu.
 
Ninachoweza kusema ni hiki, wewe ni mjinga!!! kwa kitendo ulichokifanya inaonyesha kabisa akili yako haiko sawa. Polisi wanakusimamisha usiku tena kwenye kizuizi na huna mzigo wowote wa hatari halafu unakimbia..
 
Siku nyingine usijaribu kuto tii sheria, unaposimamishwa na askari nawe ukakimbia hii humjengea asikari maswali mengi kichwani asilimia kubwa ya maswali hayo huwa ni kukutuhumu wewe kama mtu mwenye nia mbaya, unatakiwa "utii bila shuruti" USHU

Bunyebunye
 
Kwahyo ulikataa kusimama ili uonekane kidume au mjanja wa Dsm? Unafanya mambo kisela sela kama hujaoa vile, mwanao kapigwa na wewe ukapigwa, wajuaje kama mliumizwa huko ndani, hatahivyo huyo mtoto wako unamuandaa kuchukia jeshi la polisi bila sababu kumbe wewe ndiye mkosaji. kuwa makini brother mwanamme wa kweli anapokuwa na familia huishi kwa tahadhari.
 
Back
Top Bottom