Capt Tamar
JF-Expert Member
- Dec 15, 2011
- 13,054
- 18,021
Usisahau na Buibui!! Ila sisi wa mjini tulikuwa tunatumia karatasi flani hivi za kupasia!! Basi unakuta ina picha ya kijimaua,unanyunyiza maji kidogo kwenye shati Kisha unabandikia kipicha chako na kukipasi!! Oow! Those good old days!Na umeliweka kwenye wanga... mgongoni kuna malinda ya mraba, na mabegani pia....
Kuna wakati BLUEE ILIKUWA INAHUSIKA
Ilibidi nirudi home mbio huku nikiwa nahema kwanguvu, nilipo ulizwa tatizo, nikasema nimeijia tochi nikatafute pesa imeanguka. Tena nikajifanya nina haraka isije tokea mpintanjia akaiokota....Dah... Ulisalimika na kichapo siku hiyo??
Ahaa! Wewe ndiyo ulikuwa unanipiga makwenzi nikinyoa kipara eh? Halafu nikivaa safari buti zangu unanifanyia Wow wow kama mbwa! Nimeshakujua!! Sasa hivi mi msoja,njoo tena!Mm unitoe nilikuwa na miaka saba!!
Mwenzio akishang'ata akakupa nawe ung'ate eti unazungusha juu ya kichwa ndio njia ya kutoa mate ya mwenzio 😀😀Embe mnang'ata kwa zamu mpaka mnafikia kokwa.
Arusha-Moshi nilipanda kilimanjaro bus service! Nauli sh 75Pale tabora tulikuwa na KAUTA, wengine walikuwa na Kagera Retco, Kauma, Shinyanga Retco, Kaudo, Mbeya Retco, sijui nchi hii tulijikwaa wapi tu
Duuuuuh spasibaNilikuwa course urusi miaka hyo
Shikamoo mzee!Enzi hizo miaka ya 1977 pale ukumbi wa Savannah maeneo ya Ubungo, ukimilikiwa na Mzee Makao, Maquis Du Zaire walikua wakipiga mitindo ya Sanifu na Ogelea piga mbizi baadaye ukumbi huo ukaitwa White House. Nakumbuka siku zele Maquis pia ilikuwa ikipiga kwenye ukumbi wa Mpakani, maeneo ya Mwenge. Ukumbi wa Mpakani baadaye ulibadilishwa jina kuwa Silent Inn. Kisha baadae pakaja kua Kanisa.
Wengi humu hakuwepo duniani kipindi hicho.
Hapana mwaka huo hao walikuwa hawajaja. Alikuwapo mtu anaitwa Belesa Kakere. Hao walikuja kunako 1984
Mkuu Belesa Kakere wakati huo yuko na Marehemu Marijani Rajab namkumbuka kwenye kipande hiki cha wimbo nadhani unajua,
"Shangazi yakooo nae kakusihi sanaaaaaa, uje kumuona mama Magreti ukapuuza ". Aaah acha tu nyimbo zilikuwa zamani siku hizi kelele tu Mkuu!
Hiyo ilikuwa DAR INTERNATIONAL wana SUPER BOMBOKA na sio BIMA LEE. Hapo walikiwa pia na Cosmas na Fresh Jumbe...
Mkuu najua ndo maana nimesema akiwa na Marijani Rajab!
Marijan hakuwahi kukipiga Bima Lee mku
Haswa weweWengi humu hakuwepo duniani kipindi hicho.
Sema hatukuwepoWengi humu hakuwepo duniani kipindi hicho.
Marahaba kijana....Shikamoo mzee!
Daaaaaaaaaah basi mkuu apa nakumbuka ndo nilikua natimiza miaka 25 niko na bibi enu suluwali yangu ndefu panaaa af kichwani nina aflo moja ataliView attachment 452280Miaka ileeee!!
Watoto wa Mr and Mrs Daudi walikua wanaitwa Musa na Neema.Wakati vitabu vya Mr and Mrs Daudi vinaanza kuingia.